Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Nipo sehemu kijijini nimefungua kijiwe cha internet ,kuna kijana (anaonekana hayupo vizuri kimaisha) wiki iliopita alikuja kuniulizia mambo ya Freemasons kwenye internet nikamwambia anaweza akagoogle kupata taarifa zao .... sasa leo karudi amepata hela ya internet ,akanikabidhi hela na barua ndefu kawaandikia Freemasons anataka kujiunga wamsaidie maisha ni magumu na yupo tayari kwa chochote watakachotaka....hivi kama mtu yupo tayari kufanya chochote ili usaidiwe kuna usalama kweli!!!!
Nimeshindwa hata nimwambie nini huyu kijana.......!!!!!!!!!!!
Mwambie afanye kazi kwa bidii kwani mafanikio hayaji kirahisi kama anavyozani,
Hebu amshirikishe MUNGU katika mambo yake aangalie kama hatofanikiwa.
Hata walioko kwenye freemason wanafanya kazi kwa bidii,
hebu mwangalie Jay Z na Kanye wanavyojishughulisha huku na kule katika masuala yakutafuta chapaa.
Maisha yana vikwazo vingi ila Mungu pekee ndio kimbilio la walio wengi.
Huyu ni hatari sana kwa ustawi wa Jamii! maana hata 071... yake kaiweka rehani!!
Evelyn Salt na akishapata huo utajiri na anajua kabisa kuwa alimtoa mama yake kafara atakuwa na raha gani au ndo majuto ya milele
Mwambie aachane na hayo bana achacharike kivingine na azingatia ushauri wa Mzizi wa Mbuyu hapo juu
Hakika hajui anchokitaka/anachoongea, freemanson is real ila ni demonic services ambazo wanatoa kafara ya ndugu wa karibu kama sadaka....
Nipo sehemu kijijini nimefungua kijiwe cha internet ,kuna kijana (anaonekana hayupo vizuri kimaisha) wiki iliopita alikuja kuniulizia mambo ya Freemasons kwenye internet nikamwambia anaweza akagoogle kupata taarifa zao .... sasa leo karudi amepata hela ya internet ,akanikabidhi hela na barua ndefu kawaandikia Freemasons anataka kujiunga wamsaidie maisha ni magumu na yupo tayari kwa chochote watakachotaka....hivi kama mtu yupo tayari kufanya chochote ili usaidiwe kuna usalama kweli!!!!
Nimeshindwa hata nimwambie nini huyu kijana.......!!!!!!!!!!!
Evelyn Salt kaa nae na mweleze wazi hakuna njia nyepesi kwenye kufikia mafanikio na wala hakuna kitu kinachoitwa mafanikio ya harakasijui kama anaeza kuachana na hizo fikra, anaonekana amedhamiria kufanya hiyo kitu na barua inajieleza!!!
yani majamaa yatajisevia huyu kijana wa watu!!!!
Evelyn Salt kaa nae na mweleze wazi hakuna njia nyepesi kwenye kufikia mafanikio na wala hakuna kitu kinachoitwa mafanikio ya haraka
mweleze abc za maisha maana najua na wewe unazo za kwako
Watu wangu waqnaangamia kwa kukosa maarifa.
Hebu i scan hiyo barua kisha tutumie hapa jukwaani
Yani bahati mbaya kijiwe hakina scanner nilitamani niiscan niweke hapa mnisaidie kumuhurumia.....
mwambie ili awe freemason lazima waarabu wakague uone imani yake
Inabidi uwezeshwe ili uwe na kila kitu kijiweni
Kwasasa kuchange mind yake ni kazi sana, kasema anaendelea kuulizia kwa watu....
nikaona huyu hana lingine aliwazalo zaidi ya freemasons!!!!
Kawaandikia wapi kwenye address ipi na hao freemason wanapatikana wapi ?
Huenda hata research yake ya google haikufanikiwa mwambie aendelee ku-google ili aweze kupata pumba na mchele na sio kupotezeana muda na story za vijiweni
Muulize swali lakizushi, je akiambiwa ajitoe roho yake atakubali????
Maana amesema yuko tayari kwa lolote.
Sio kuwa aligoogle, alikuja hapa kuulizia akiitaji habari mbalimbali atapata?nikamjibu ndio nikampa na bei....
akaondoka akasema ngoja akatafute hela atarudi, imepita wiki ndo leo kaja, kanipa hela na barua
nikajua matokeo ya form four tayari labda kaandika namba yake hapo nimchekie kufungua ndo nakuta ameandika
"mimi flani (full name) umri, na mahali alipo anaomba kujiunga na freemasons yupo tayari kwa kiu chochote watakachotaka....nk.)
nikamuambia hawezi kupata anuani zao labda akigoogle tu atapata habari zao, akaonekana kunyong'onyea sana akaishia!