Freemasons katika siasa na dini

Hivi sasa, biblia anaruhusiwa kila mtu.

Sasa basi nini ambacho Kanisa katoliki lilificha kimefichuliwa?
WAKATOLIKI wana mwanadamu waliempa jina lenye wadhifa na wasifu wa Mungu peke yake, yaani " Baba Mtakatifu"(PAPA) Soma: Yohana 17:11Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba Mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo.


Umeona hiyo aya inavobainisha kuwa "Baba Mtakatifu" ni jina la Mungu? Lakini Wakatoliki wana babao mtakatifu mwingine!!!!!? KUFURU!.
 
Usabato ndio ufreemason na wanatumika kuvurga dini nyingine
UFREEMASON NDANI YA MAKANISA

IBADA ZA SANAMU MAKANISANI
Zab 115:4-8 SUV
Sanamu zao ni fedha na dhahabu, Kazi ya mikono ya wanadamu. Zina vinywa lakini hazisemi, Zina macho lakini hazioni, Zina masikio lakini hazisikii, Zina pua lakini hazisikii harufu, Mikono lakini hazishiki, miguu lakini haziendi, Wala hazitoi sauti kwa koo zake. Wazifanyao watafanana nazo, Kila mmoja anayezitumainia.

Yeremia 10

2Mwenyezi-Mungu asema hivi:
“Msijifunze mienendo ya mataifa mengine,
wala msishangazwe na ishara za mbinguni;
yaacheni mataifa mengine yashangazwe nazo.
3Maana, mila za dini za watu hawa ni za uongo.
Mtu hukata mti msituni
fundi akachonga kinyago cha mungu kwa shoka.
4Kisha watu hukipamba kwa fedha na dhahabu
wakakipigilia misumari kwa nyundo
ili kisije kikaanguka.
5Vinyago vyao ni kama vinyago vya kutishia ndege

katika shamba la matango,

 
Woi, kama huijui vizuri dini ya mtu it's better ukae kimya! Unaweza laanika


“ ni marufuku kwa mtu wa kawaida kusoma agano la kale wala jipya. Wakuu wa wilaya watahusika kuwatafuta kwa umakini wazushi wote katika makazi yao na hata mafichoni ili kuwashughulikia kikamilifu”. Council Tolosanion, Pope Gregory IX, Anno.Chr.1229.

 
Wasabato wakishashiba maharage ya jumamosi daaaaah
“Mamlaka ya papa haina mwisho,na ni isiyozuilika; inaweza kuharibu na kumpoteza
yeyote, kama Innocent III alivyosema.Papa anaweza kumwadhibu mtu yeyote, na mamlaka yake hairuhusu kukata rufaa maana ndiyo ya mwisho katika utendaji; kwa maana papa ndiye mwenyemamlaka zote katika kifua chake kama alivyosema Boniface III.Na kwa kuwa hawezi kukosea, basi yeye ndiye mwamuzi wa kila jambo katika kanisa kwa kutunga miongozo, kuleta kila aina ya fundisho, kuamrisha kila aina ya matakwa yake katika maswala mazima ya imani. Hakuna haki yoyote inayoweza kusimama kinyume yake ikiwa ni ya mtu binafsi au shirika”
Ignaz von Dollinger, “A Letter Addressed to the Archbishop of Munich” 1871; as quoted in MacDoudall, The Action Newman Relations (Fordham University Press) pp.119,120.


Danieli 7:8, “Nikaziangalia sana pembe zake, na tazama, pembe nyingine ikazuka kati yao, nayo ilikuwa ndogo, ambayo mbele yake pembe tatu katika zile za kwanza zikang'olewa kabisa; na tazama, katika pembe hiyo mlikuwa na macho kama macho ya mwanadamu, na kinywa kilichokuwa kikinena maneno makuu.”


Andiko hili la kiunabii linatuonesha kwamba juu ya upapa ataketi mtu mmoja; yaani papa. Na huyu huchukuliwa kama mtu asiyekosea na mwenye mamlaka ya kuamuru chochote na ni lazima kitekelezwe.
 
Unaandika kutoka kichwani kwako na sio uhalisia wa mambo! Just dig out mzee
 
Mimi sio Msabato na wala sio muislamu but chunguza kwa umakini sana, Roman Catholic sio dini, ile ni serikali inayoiendesha dunia; serikali yoyote duniani ikosane na RC then utauona mziki wake, ukichunguza sana utagundua ndio hao hao waliuanzisha na UISLAM pale mashariki ya kati. Waislamu watabisha but moja kati ya proves wanaoitumia kuhalalisha UTUME wa Mohamad ni maneno ya padree wa Roman Catholic wa enzi hizo akimuusia mjomba wa Mohamadi ambaye of course ndio alikua mlezi wake; kuna siri nyingi sana hatuzijui kwenye hizi dini zote za duniani
 
Kwaiyo hayo ndiyo yanakufanya useme ni satanic??
Kanisa Katoliki limebadilisha Amri Kumi za Mungu.

Wameondoa amri ya pili kwenye katekisimu ili Waabudu sanamu na kugawa ile ya kumi mara mbili. Pia, wameondoa sehemu ya amri ya nne. Pengine huu ndio udanganyifu mkuu zaidi katika historia ya ulimwengu. Licha ya hili, wapo wengi wanaoamini kwamba Kanisa Katoliki ni kanisa la Kikristo.

Lakini Mkristo lazima amfuate Kristo na wala si kubadilisha chochote ambacho Kristo amesema au kuandika; tofauti na kile ambacho Kanisa Katoliki limefanya, na si tu kuhusiana na sheria ya Mungu. Kwa hiyo tunakubaliana na Luther na Wanamatengenezo, walioona vyema kwamba papa anabeba sifa za mpingaKristo.

Martin Luther huliweka kwa namna: “Hapo awali nilisema kwamba papa alikuwa mwakilishi wa Kristo; sasa natangaza kwamba yeye ni adui mkuu wa Bwana wetu, mtume wa Ibilisi.” (D’Aubigne, kitabu cha 7, sura ya 6).

Ilani ya kipapa ilipomfikia Luther, alisema: “Naidharau na kuishambulia, kuwa ni yenye kufuru na uongo.... Kristo Mwenyewe ndiye anayeshutumiwa humo.... Nafurahia kwa kustahimili maovu hayo kwa ajili ya faida ya kazi bora zaidi. Tayari najisikia kuwa na uhuru mkubwa zaidi moyoni mwangu; kwa vile hatimaye najua kwamba PAPA NI MPINGAKRISTO, NA KWAMBA UTAWALA WAKE NI WA SHETANI MWENYEWE.” (D’Aubigne, kitabu cha 6, sura ya 9).
 
Unasema wameondoa amri ya pili, nakuuliza hivi niletee amri za waroma zote kumi wanazotumia afu na za hao wasabato nilinganishe kitu.. sitaki uniletee gazeti nataka amri kumi wanazotumia waroma na wanazotumia wasabato
 
Upo sahihi mkuu, sio wote watajua ,

ukweli ni kwamba ilifanyika DIVIDE AND RULE , wanaosoma historia wanajua uislamu umeanzishwa na Roma

Pia inajulikana wazi kwamba kiti cha upapa kilitoka katika upagani wa Uislamu; Alexander Hislop, akizungumza juu ya kiti cha enzi cha Petro au kiti cha enzi anachokalia Papa, anasema

“wakati askari wa Ufaransa chini ya Jemedari Bonaparte walipoimiliki Roma mwaka 1795, walikuta nyuma yake, kwa Kiarabu, sentensi hii inayojulikana sana kutoka kwenye Korani, “Hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu, na Mohhomed ni Mtume Wake” — (The Two Babylons, Page 213, Chapter 6, Religious Orders, Section L).
 
Unasema wameondoa amri ya pili, nakuuliza hivi niletee amri za waroma zote kumi wanazotumia afu na za hao wasabato nilinganishe kitu.. sitaki uniletee gazeti nataka amri kumi wanazotumia waroma na wanazotumia wasabato
NDUGU SOMA KWENYE KATEKISIMU, YAKO THEN UFANANISHE NA BIBLIA, HAPA NIPO MBALI NA KATEKISIMU AU SHAJARA NA MISALE, ZISOME HUMO UFANANISHE NA ZA KUTOKA 20:1-17

 
Unasema wameondoa amri ya pili, nakuuliza hivi niletee amri za waroma zote kumi wanazotumia afu na za hao wasabato nilinganishe kitu.. sitaki uniletee gazeti nataka amri kumi wanazotumia waroma na wanazotumia wasabato
Kwa mujibu wa katekisimu:-
1.Usiabudu miungu wengine.
2. Usiape bure kwa jina la Mungu wako.
3. Shika Kitakatifu Siku ya Mungu wako
4. Waheshimu Baba na Mama, upate miaka mingi na heri duniani.
5. Usiue
6. Usizini
7. Usiibe
8. Usiseme uongo
9. Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10. Usitamani mali ya watu.

Kwa mujibu wa biblia:
Kutoka 20:1-17
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹ Mungu akanena maneno haya yote akasema,
² Mimi ni Bwana, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.
³ Usiwe na miungu mingine ila mimi.
Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
⁵ Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
⁶ nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako, maana Bwana hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.
⁸ Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.

⁹ Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
¹⁰ lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
¹¹ Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
¹² Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wako.
¹³ Usiue.
¹⁴ Usizini.
¹⁵ Usiibe.
¹⁶ Usimshuhudie jirani yako uongo.
¹⁷ Usiitamani nyumba ya jirani yako, usimtamani mke wa jirani yako; wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala cho chote alicho nacho jirani yako
.
 
Wewe si mtu anayejifunza. Umejibu ambacho sijakuuliza. Pia ulichojibu si sahihi.

Jaribu kujifunza, tafuta elimu ya vitu. Mambo yako wazi sio kufanya ubishi.
 
Wakati mwingine unahoji ukidhani jamii ya humu itakuona GT kumbe unafunua upumbavu wako...yote uliyohoji yako wazi soma theolojia ya RC soma ufunuo (bei bible 7000)
 
Wakati mwingine unahoji ukidhani jamii ya humu itakuona GT kumbe unafunua upumbavu wako...yote uliyohoji yako wazi soma theolojia ya RC soma ufunuo (bei bible 7000)
Mimi naifahamu theolojia ndio maana natoa hayo maswali. Kwasababu imani si sayansi lakini teolojia ni sayansi ya imani.

Wewe umeruhusu mwili ushinde akili ndio sababu unasema hayo unaoyasema.

Watu wanaofanya mambo ili jamii iwaone ni wapumbavu.

Mtu anaefahamu mambo hawezi kusema "soma teolojia ya RC." Duniani hakuna kitu kinaitwa Roman Catholic (RC), ila Catholic Church.
 
Asante kwa Mada nzito

Ktk hoja za unabii biblia inajitafsiri yenyewe. Naomba majibu ya maswali yangu

1. Mnyama mana yake ni utawala au dola, Pembe ni mfalme je na Kichwa ni nini? Kwanini unataja vichwa saba ktk yulr mnyama wa Ufunuo kama tawala za ulaya? Je kichwa maana yake ni utawala?

2. Yule mnyama afananae na Mwanakondoo,anayeinuka kutoka ktk nchi ..niambie ni wapi katika biblia imeandikwa kwamba ni Marekani?? Kwani nini isiwe Djibout au Ethiopia.

3. Kwa sasa nyakati hizi yunazoishi sisi tuko ktk utawala upi wa dunia? Yaani mnyama yupi kati ya Simba, Dubu, chui na huyo mwingine anayetodautiana na wengine wote mwenye meno kama ya chuma na nguvu nyingi?

5. Ktk biblia ni wapi imeandikwa kuwa Mnyama wa kwanza wa Ufunuo anayepewa Nguvu na kiti cha enzi na yule Joka ni Rumi? Maana tujuavyo sasa hatuna utawala wa rumi unaotawala dunia.

6. Freemason, illuminat vimetajwa wapi ktk biblia?? Umeongeza mwenyewe au?

7. Huyu Nabii wa uongo anayetajwa kuunda sanamu ya mnyama na kuipulizia pumzi hadi ikanena; kauli hii ina maana gani? Kwamba sanamu kweli itaundwa na Nabii wa uongo?

8. Mnyama wa kwnza ktk ufunuo ni mtu au ufalme? Nabii wa uongo ni Mtu au ufalme?
 
Mwinjilisti Machota umeibukia huku?
 
1. Mnyama mana yake ni utawala au dola, Pembe ni mfalme je na Kichwa ni nini? Kwanini unataja vichwa saba ktk yulr mnyama wa Ufunuo kama tawala za ulaya? Je kichwa maana yake ni utawala?
KWANZA ASANTE KWA MASWALI MAZURI

Ufunuo 17:9-11 “Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo. Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache. Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu.”


Katika siku chache nyuma, wakati nilipojaribu kutafsiri unabii huu sikuzingatia wakati/muda sahihi. Na siyo mimi pekee yangu, kuna watu wengi wanaokosea kutafsiri unabii huu kwa sababu ya kutozingatia wakati/muda sahihi ambao unabii huu unahusika.

Jinsi nilivyotafsiri unabii huu, kama vile ambavyo na watu wengi hutafsiri. Nilitumia wakati ambao Yohana alikuwa akiishi, na wakati huo ufalme uliokuwa ukitawala ulikuwa ni ufalme wa dola la Rumi ya kipagani. Hivyo jibu la unabii huu ambalo ningepata lilikuwa kama ifuatavyo.

Ufunuo 17:10 “Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache.”

Ukichukulia wakati/muda ambao Yohana aliona maono haya, utaona kuwa yule mfalme anayetajwa kuwa “na mmoja yupo” ni ufalme wa Rumi ya kipagani, ambao ulikuwa ukitawala wakati yohana alipoona maono haya. Hivyo, wale wafalme watano walioanguka watakuwa ni falme tano zilizokuwa zimepita ambazo ni Misri, Ashuru, Babeli, Umedi&Uajemi, na Ugiriki. Na yule mfalme mwingine ambaye hajaja bado atakuwa ni utawala wa Upapa uliopata nguvu kuanzia 538 BK., nao baada ya kuanza ungetawala kwa muda mchache.

Ufunuo 17:11 “Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu.”

Mnyama aliyekuwako naye hayuko ni upapa ambao ulitawala tangu 538 BK, hadi ulipopata jeraha la mauti mwaka 1798 BK.,

Mnyama aliyekuwako, ni upapa uliotawala tangu mwaka 538BK hadi 1798BK, ulipopata jeraha la mauti.

…naye hayuko, tangu mwaka 1798BK ulipopata jeraha la mauti hadi 1929BK wakati wa kusaini katika ikulu ya Leteran.

Hivyo, kwa jinsi kama hii ingeonyesha kwamba mfalme wa nane angekuwa ni Upapa baada ya kupona jeraha lake la mauti mwaka 1929 BK.
2. Yule mnyama afananae na Mwanakondoo,anayeinuka kutoka ktk nchi ..niambie ni wapi katika biblia imeandikwa kwamba ni Marekani?? Kwani nini isiwe Djibout au Ethiopia.
KIPINDI YOHANA ANAONESHWA HAYA MAAONO TAIFA LA USA LILIKUWA HALIJAANZISHWA WALA KUPEWA JINA, SASA TUTAJUAJE NI USA NA SIO ETHIOPIA AU DJIBOUT? Twende tufatilie sifa zitakazotusaidia ambazo zitafiti kwa USA tu...

Ufunuo 13:11-12 “Kisha nikaona mnyama mwingine, akipanda juu kutoka katika nchi; naye alikuwa na pembe mbili mfano wa Mwana-Kondoo, akanena kama joka. Naye atumia uwezo wote wa mnyama yule wa kwanza mbele yake. Naye aifanya dunia na wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama wa kwanza, ambaye jeraha lake la mauti lilipona.”


Je mnyama huyu wa pili anaeifanya dunia na wote waikaao wamsujudie yule mnyama wa kwanza aliyepata jeraha la mauti ni nani? Ili kumtambua mnyama wa pili, ni lazima kwanza tumtambue kwanza mnyama wa kwanza.

Mnyama wa kwanza aliyepata jeraha la mauti ni kanisa la Romani Katoliki na Upapa.

Kutoka katika nchi(sehemu kavu) ni kinyume cha kutoka katika bahari(sehemu yenye maji). “bahari” inawakilisha “sehemu yenye watu wengi tofauti”, hivyo “nchi” ni kinyume chake na inawakilisha “eneo lisilo na watu wengi.” Jambo hili linafaa kwa taifa la Marekani, liliinuka mwishoni mwa karne ya 18, miaka ya 1776BK likiwa na watu wachache. Mwandishi mmoja aliandika kuwa taifa la Marekani…

“Siri ya kuja kwake kutoka katika sehemu tupu, kama mbengu ya kimya kimya tulikua hadi kufikia kuwa dola.” -Vandeman, GeorgeDestination Life, (Mountain View: Pacific Press Pub. Assoc., 1980), p. 74

…Angekuwa na sifa za mwana-kondoo, lakini angenena kama joka.

“‘’ Pembe mfano wa mwana-kondoo zinaashiria ujana, na umakini, na zinawakilisha uhuru wa kiraia na kidini.

Karibu kila mmoja anafahamu historia hii. Wakati wa utawala wa Upapa mwaka 538-1798BK, uliua Wakristo wa Kiprotestanti zaidi ya milioni 100,000000, hivyo wakati wa miaka ya 1776BK Wakristo wengi walikimbilia katika nchi ya Marekani ambako kulikuwa na uhuru wa kuabudu. Kwa hakika hali hii ya uhuru wa kuabudu, na kutetea haki na uhuru wa dini, ndiyo inawakilishwa na kuwa na “pembe mbili mfano wa mwana-kondoo.” Karibu kila mmoja anajua Wakristo wa kweli katika Maandiko huwakilishwa kama “kondoo,” lakini Wakristo wa uongo huwakilishwa kama “mbwa-mwitu.” Hivyo, taifa la marekani liliwakilishwa kwa mfano wa mwana-kondoo kwa kitendo kabisa cha Wakristo wa kweli walioteswa na Upapa kukimbilia huko, na kwa kitendo cha taifa lenyewe kulinda uhuru wa dini kwa ajili ya watu wa Mungu.

Lakini Ufunuo 13:11 inasema tena kuwa, taifa hili hili lenye mfano wa mwana-kondoo litanena kama joka.

Joka = Shetani/ibilisi

Ufunuo 13:9 “Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.”

Kama taifa la Marekani lingekuja kunena kama joka, hii inaashiria kwamba lingekuja kufanya mambo ya kishetani yasiyopendeza mbele za Mungu. Taifa la Marekani lina pembe mbili kama za mwana-kondo, lakini linanena kama joka. Ukiangalia hatua za taifa la Marekani; matendo yake, na maneno yake utaona kabisa kuwa taifa hili linanena kama joka. Jinsi linavyoua watu katika vita, linavyoua watu kwa kutumia sumu, linavyotoa amri kwa mataifa mengine yafanye kama linavyotaka lenyewe, hii ni wazi taifa la Marekani linafanya mambo mengi ya kishetani. Lakini unabii hauishii hapa, bali unasema zaidi kuwa taifa la Marekani (mnyama wa 2), na Vaticani (mnyama wa 1) wataungana ili kulazimisha alama ya mnyama.

NITAENDELEA BAADAE NA MASWALI ,MENGINE
 
3. Kwa sasa nyakati hizi yunazoishi sisi tuko ktk utawala upi wa dunia? Yaani mnyama yupi kati ya Simba, Dubu, chui na huyo mwingine anayetodautiana na wengine wote mwenye meno kama ya chuma na nguvu nyingi?
ZILE TAWALA NNE KUTOKA BABELI HADI RUMI YA KIPAGANI ZILIPITA, LAKINI KUMBUKA BAADA YA RUMI YA KIPAGANI INATOKEA KATIKATI YAKE PEMBE NDOGO AMBAYO NDIYO RUMI YA KIDINI.... BAADA YA HAPO UFALME WA MWISHO KABISA NI UFALME WA YESU AMBAO DANIELI ALIONA JIWE LISILOFANYWA KWA MIKONO LINASAMBARATISHA FALME ZOTE






KUJUA TUPO KIPINDI GANI ITAKUBIDI USOME Ufunuo 17:7-18

Hapa pia tunaona Yohana anaonyeshwa siri ya yule mnyama ambaye ndio yule yule aliyeonyeshwa katika ile sura ya 13 ambaye ana vichwa 7 na pembe 10, isipokuwa hapa zile pembe 10 zinaonanekana hazina vilemba ikiwa na maana hazijapokea ufalme bado, na ndio maana tukisoma mstari wa 12 inasema watakuja kupokea ufalme(yaani kuvikwa vilemba) saa moja na yule mnyama.

Kumbuka vile vichwa saba, ni FALME 7, ambazo shetani alizikalia kuutesa au kutaka kuungamiza kabisa uzao wa Mungu, ambazo ni 1) MISRI 2)ASHURU 3)BABELI 4)UMEDI & UAJEMI 5) UYUNANI 6) RUMI-ya-KIPAGANI 7) RUMI-ya KIPAPA...



Lakini tunaona hapo wakati Yohana anaonyeshwa maono hayo aliona watano wameshakwisha anguka, na mmoja yupo na mwingine hajaja bado. Kumbuka wakati ule Yohana anapewa haya maono AD 90 ,utawala uliokuwa unaitawala dunia wakati ule ni RUMI ya kipagani, kwahiyo zile tawala tano za kwanza zilikuwa zimeshapita yaani Misri, Ashuru, Babeli, Umedi&uajemi pamoja na Uyunani. Hivyo ule wa Urumi ndio uliokuwepo na ndio ule uliomsulibisha KRISTO.

Na kama alivyoambiwa mmoja bado hajaja(ambaye ni wa 7), Na kwamba atakapokuja itampasa akae muda mchache, sasa huo si mwingine bali ni ule utawala wa RUMI ya kidini chini ya upapa ulioongoza dunia nzima kuanzia kile kipindi cha karne ya 4, ni ule ule tu wa RUMI sema hapa umegeuka ukawa wa kidini chini ya upapa.

Tukiendelea kusoma mstari wa 11 inasema.." Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu.".Hivyo tunaona mnyama mwingine wa 8 anajitokeza hapo, lakini biblia inasema huyu wa 8 ndio yule yule wa 7, hii ikiwa na maana kuwa ni kile kile kichwa cha saba isipokuwa kimebadilisha taswira, kwasababu yule mnyama tayari anavyo vichwa saba hawezi akawa tena na vichwa nane,

Na huyu mnyama wa 8 biblia inasema ambaye alikuwako naye hayupo naye anaenda kwenye uharibifu, tukirudi kwenye historia tunamwona huyu mnyama (ambaye ndio kile kichwa cha 7 -Rumi ya kidini chini ya Upapa wa Kanisa Katoliki) ulikuwa na nguvu kipindi kile cha utawala wake, lakini baadaye ulikuja kutiwa jeraha la mauti na wale wanamatengezo, hivyo nguvu zake za kutawala dunia nzima zilikufa, lakini tunaona lile jeraha lilianza kupona tena, kuanzia kile kipindi cha vita vya pili vya dunia mpaka leo linaendelea kupona, utakapofika wakati atakaporejeshewa nguvu zake tena alizopoteza ndipo atakapoingia katika UHARIBIFU, naye ataitawala dunia kwa kipindi kifupi cha miaka mitatu na nusu ndio kile kipindi cha dhiki kuu, ndio maana biblia inasema alikuwepo naye hayupo, naye anajiandaa kwenda kwenye uharibifu. Kwasababu hapo mwanzo alishawahi kutawala na atakuja kutawala tena.

Sasa Zile pembe 10 za yule mnyama ambayo ni yale mataifa 10 ya ULAYA(EU), Biblia inasema yatakuja kupata nguvu wakati mmoja na yule mnyama. Na haya ndiyo mpinga-kristo PAPA atakayoyatumia kuwatesa wale ambao hawataipokea chapa ya mnyama katika kile kipindi cha dhiki kuu.

Lakini mstari 16 tunaona jambo lingine.." Na zile pembe kumi ulizoziona, na huyo mnyama, hao watamchukia yule kahaba, nao watamfanya kuwa mkiwa na uchi, watamla nyama yake, watamteketeza kabisa kwa moto."

Mwisho wa yote baada ya dhiki kuu kukaribia kuisha yale mataifa 10 ya Ulaya yatagundua kuwa utawala wa mpinga-kristo(PAPA) Chini ya kanisa katoliki hauna manufaa yoyote wala haujasaidia chochote kutimiza matakwa yao, na suluhu zao za AMANI, sasa kwa pamoja yatamchukia yule mwanamke(yaani PAPA) na Makao yake VATICAN na kumwangamiza kabisa, hiyo ndio HUKUMU ya YULE KAHABA MKUU kama mstari wa kwanza unavyosema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…