Freemasons ndani ya Makanisa

ALIYEKWAMBIA UKISHUKIWA ROHO NDIO UNANENA KWA LUGHA NANI?


KWAHIYO WANAOSHUKIWA NA ROHO MTAKATIFU NDIO WANANENA KWA LUGHA?

MIMI NAZUNGUMZIA KUNENA KWA LUGHA , WEWE UNACHANGANYA MAFAILI ETI KUSHUKIWA ROHO, NI VITU VIWILI TOFAUTI

MATENDO 2
4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.

Hiyo ndo shida ya kusoma ili ujibu sio ili usome uelewe. Hayo maandiko hapo juu yanajibu hilo swali lako. Haya leta hoja sasa.
 
MATENDO 2
4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.

Hiyo ndo shida ya kusoma ili ujibu sio ili usome uelewe. Hayo maandiko hapo juu yanajibu hilo swali lako. Haya leta hoja sasa.
SIO KILA ANAYEJAZWA ROHO ANANENA KWA LUGHA


UNAELEWA HILO?

Matendo 7:55 NEN - Bible.com​



Lakini yeye Stefano, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alikaza macho mbinguni, akaona utukufu wa Mungu, na Yesu akiwa amesimama mkono wa kuume wa Mungu.
 
Wakati huo huo uzingatie kuwa wanafunzi wa Yesu wakati wananena kwa lugha mpya katika siku ya Pentekoste, wale ambao hawakuwa wanafunzi wa Yesu(Wayahudi wa ugenini) waliweza kuelewa kila mtu kwa lugha yake. Je mbona kunena kwa lugha kwa siku hizi si kama si kama siku ya Pentekoste?

TAFAKARI MASWALI YAFUATAYO:-

1)Kama lugha iliyonenwa siku ya pentekoste ndiyo ya sasa mbona tunaponena wenzetu hawatuelewi?
2)Kama lugha iliyonenwa siku ya pentekoste ndio lugha tunayonena leo mbona ni baadhi ya makanisa na ni baadhi ya Wakristo ndio wananena kwa lugha badala ya makanisa yote na wakristo wote kama walivyonena wote siku ya pentekoste?
3) Kama lugha ya pentekoste ndiyo ya nyakati za leo mbona hatuoni ndimi kama za moto?
4) Siku ya pentekoste hawakuwekewa mikono ila Roho aliwashukia tu na wakajawa na Roho na kuanza kunena kwa lugha mpya, baada ya kipindi cha pentekoste kupita waliofuatia kama KORNERIO, WASAMARIA, AKIDA WA ETHIOPIA nk wao waliwekewa mikono na mitume na walipoombewa tu lugha ikaanza ndani yao. Je nyakati za leo ndivyo tunavyoombea watu? Nyakati za leo badala ya kuwaombea wakristo ujazo wa Roho Mtakatifu tunawaombea ili wanene kwa lugha.
 
SIO KILA ANAYEJAZWA ROHO ANANENA KWA LUGHA


UNAELEWA HILO?

Matendo 7:55 NEN - Bible.com​



Lakini yeye Stefano, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alikaza macho mbinguni, akaona utukufu wa Mungu, na Yesu akiwa amesimama mkono wa kuume wa Mungu.

Kumbuka Stephano pale hakuwa kwenye maombi. Baada ya watu walipojaribu kushindana na hekina aliyonayo Stephano walipomshindwa walimpeleka mahakamani wakimsingizia mambo kadha wa kadha, na ndipo walipomuuliza Stephano je mambo hayo ndivyo yalivyo Stephano akaanza kuhubiri. Kazi moja wapo ya Roho Mtakatifu ni kutuongoza, Stephano yeye tayari alikuwa na Roho Mtakatifu ndani yake akimwongoza. Hakuwa anampokea pale Roho Mtakatifu wala hakuwa kwenye maombi.

Ishara mojawapo kwamba umempokea Roho Mtakatifu au umejazwa Roho Mtakatifu ni kunena kwa lugha, ndo maana nimekuletea ushahidi wale wanafunzi walivyojazwa wote walinena. Ina maana hata Stephano alipohubiriwa kuokoka na kumpokea Roho Mtakatifu kwa mara ya kwanza lazima alinena kwa lugha. Ila pale kwenye Matendo 7 Stephano hakuwa kwenye maombi alikuwa anauawa. Na Roho Mtakatifu alikuwa anamwonyesha mauti yake na ndiyo maana akaanza kusema anaona mbingu zimefunguka, anamwona mwana wa Mungu ameketi mkono wa kuume n.k n.k ndipo wakampiga kwa mawe hadi kufa. Na Sauli (Paulo) alikuwa akishuhudia kabla neema yake ya kuokoka ikiwa bado haikumfikia.
 
ACHA KUDANGANYA ,SIO KILA MWENYE ROHO MTAKATIFU ANANENA KWA LUGHA

Matendo 7:55 NEN - Bible.com​



Lakini yeye Stefano, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alikaza macho mbinguni, akaona utukufu wa Mungu, na Yesu akiwa amesimama mkono wa kuume wa Mungu.

WAPI STEPHANO ALINENA KWA LUGHA?? NAOMBA ANDIKO

Yesu Kristo alijaa Roho mtakatifu ndani yake.

WAPI YESU ALINENA KWA LUGHA

Endapo tungemwuliza Mtume yule mkuu Paulo kwamba tamaa yake ilikuwa ni nini kwa muumini, yeye angeweza kusema: “Ufuateni upendo, na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu.” 1 Wakorintho14:1-5, KJV. Je, ingekuwa ni kuipanua sana hoja hiyo juu ya uwiano usio na maana kuhusu karama hiyo ya lugha iliyoleta usumbufu mwingi katika makanisa yale ya Kikorintho? Si kila mmoja wetu ambaye angeweza kunena kwa lugha, kwa mujibu wa Paulo. Hata wale waliotakiwa “kutaka sana karama za rohoni” walishauriwa hivi:

“Hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora.” 1 Wakorintho 12:31. Kuwapenda watu wote na kuhubiri bila kuona fahari katika kitu cho chote ila msalaba wake Kristo - hiyo ndiyo njia iliyo bora. Wagalatia 6:14.
 
Ishara mojawapo kwamba umempokea Roho Mtakatifu au umejazwa Roho Mtakatifu ni kunena kwa lugha, ndo maana nimekuletea ushahidi wale wanafunzi walivyojazwa wote walinena.
Si kila mmoja wetu ambaye angeweza kunena kwa lugha, kwa mujibu wa Paulo. Hata wale waliotakiwa “kutaka sana karama za rohoni” walishauriwa hivi:

“Hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora.” 1 Wakorintho 12:31.

Kuwapenda watu wote na kuhubiri bila kuona fahari katika kitu cho chote ila msalaba wake Kristo - hiyo ndiyo njia iliyo bora. Wagalatia 6:14.
 
Ishara mojawapo kwamba umempokea Roho Mtakatifu au umejazwa Roho Mtakatifu ni kunena kwa lugha, ndo maana nimekuletea ushahidi wale wanafunzi walivyojazwa wote walinena
UNADAGANYA SIJUI KWA MANUFAA YA NANI

SIKILIZA BIBLIA ISEMACHO

Kwa hiyo, waumini ni lazima wawe wanaume na wanawake waliojazwa Roho. Warumi 8:9.

Lakini basi, hakuna mahali po pote katika kumbukumbu hizo pamoja na nyinginezo nyingi zinazohusu kazi ya Roho Mtakatifu tunapopata hata dokezo moja dogo sana kuonyesha kwamba aina yo yote ya karama ya lugha ingekuwa ndilo tunda au kipawa cha Roho Mtakatifu ndani ya maisha ya kila muumini.

Badala yake, imeelezwa kwa wazi kabisa kwamba “tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi.” Wagalatia 5:22,23.
 
Ishara mojawapo kwamba umempokea Roho Mtakatifu au umejazwa Roho Mtakatifu ni kunena kwa lugha, ndo maana nimekuletea ushahidi wale wanafunzi walivyojazwa wote walinena.
hebu chukua wahusika waliojitokeza sana katika kitabu hicho cha Matendo, mbali na Paulo na Petro. Hao, kwa mfano, walikuwa ni Stefano, Yakobo, Agabo, Simeoni, Filipo, Sila, Timotheo, Barnaba, Lidia, Dorka, Krispo, Apolo, Akwila, Prisila, kuwataja wachache tu. Hao walifanya kazi kubwa kwa ajili ya Mungu, lakini hatujui habari yo yote kuhusu uzoefu wao wa “kunena kwa lugha,” zile zinazojulikana au zile zisizojulikana, ndani ya mmojawapo miongoni mwao
 

Ndiyo maana kila mda nasema Roho Mtakatifu hana limitation wala huwezi ukampangia Roho Mtakatifu unenaje.

Matendo 2

4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.

Tafakari tena huo mstari unasema hapo mwishoni "kama Roho alivyowajalia kutamka"

Je, ni kazi yako wewe mwanadamu kumkosoa Roho Mtakatifu kwa jinsi alivyomjalia mwingine kutamka kisa tu wewe huelewi au umeshindwa kutafsiri? Jibu ni Hapana.

Roho Mtakatifu anaweza akakujalia leo utamke kifaransa na akaruhusu mtu anayejua kifaransa atafsiri. Kesho akakujalia kutamka vingine kabisa katika maombi yako labda akataka unene iwe siri yake yeye tu na Baba ( Mungu Baba )

Maana maandiko yanasema Roho Mtakatifu hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa (sikumbuki ni kitabu gani) na kama nilivyosema Roho Mtakatifu anakujalia kwa kadri apendavyo yeye.

Ndipo Paulo akashauri ili basi ufahamu wako uwe na matunda (akiwa na maana kwamba wakati mwingine unanena kwa lugha wewe mwenyewe huelewi wala hakuna wakukutafsiria), akashauri tutenge muda wa kuomba kawaida kwa maneno tunayoyaelewa na vilevile tuwe na muda wa kuomba kwa Roho au kunena kwa lugha ya Roho Mtakatifu.

Hivyo siyo kazi yetu sisi wanadamu kumkosoa Roho Mtakatifu kwa jinsi alivyopenda kujalia mwingine kunena eti kwa kuwa hatuelewi au kwa kuwa tunataka kumlazimisha Roho Mtakatifu amjalie mwingine kunena kwa namna ambayo tunataka sisi.

Tumwache Roho Mtakatifu afanye kazi yake.
 
MATENDO 2
4 Wote wakajazwa Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia kutamka.

Hiyo ndo shida ya kusoma ili ujibu sio ili usome uelewe. Hayo maandiko hapo juu yanajibu hilo swali lako. Haya leta hoja sasa.
UNADOKOA KAMSTARI EE, SIO KILA MWENYE ROHO MTAKATIFU LAZIMA ANENE KWA LUGHA, HIYO NI MOJA TU YA KARAMA , NDIO MAANA TUNASHANGAA NINYI WOTE MNASEMA MNANENA,

Roho Mtakatifu hugawa karama kwa kila mtu kama apendavyo yeye, lakini hawapatii watu wote karama moja, zinatofautiana.

TWENDE KWENYE MAANDIKO

Lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.” “Je! wote ni mitume? wote ni manabii? wote ni waalimu? wote wanatenda miujiza? wote wana karama za kuponya wagonjwa? wote wanena kwa lugha? wote wafasiri? Takeni sana karama zilizo kuu. Hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora.” “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.” 1 Kor. 12:11, 29-31; 13:1-3.
 
KUNENA KWA LUGHA HUKU TUNAKOKUONA LEO HUO UTARATIBU WAMETOA WAPI?

HIZO LUGHA MNAZIJUA MAANA YAKE?

HIYO KARAMA ROHO HUITOA APENDAVYO, MBONA KILA MMOJA ANAIKIMBILIA NA KUNENA?

Je, ni karama ipi ambayo tunatakiwa kuitafuta zaidi?​

“Ufuateni upendo, na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu.” 1 Kor. 14:1.
 

Nilijua utakuja kutaka andiko Stephano alinena wapi kwa lugha. Na mimi nikuulize Je, unaamini Stephano aliokoka na kumpokea Yesu? Ni nani aliyemhumbiria akaokoka nipe historia yake kwenye maandiko.

Ukijudge Bible that way hutatafakari ukaielewa, utakariri. Sio kila kitu lazima kiandikwe Vitabu visingetosha kama Yohana alivyoandika kwenye Ufunuo.

Ila ukitafakari Bible utaielewa utaweza kugundua Aha, kwahiyo hii Matendo 7 inasema Stephano akajaa Roho, kumbe inamaana aliokoka na kumwamini Yesu. Utagundua pia Aha kumbe ina maana kuna siku na yeye aliamini uwepo wa Roho Mtakatifu na akampokea kwa mara ya kwanza.

Utagundua pia, kama Biblia inawataja wanafunzi walipompokea mara ya kwanza Roho Mtakatifu walinena kwa lugha mpya kama ishara, hivyo kwa vyovyote vile Stephano alipitia hii ishara.

Bible ndo inavyotafakariwa hivyo siyo kila kitu lazima uandikiwe. Kwahiyo utataka hadi Biblia iandike jinsi Stephano alivyozaliwa ndo uamini ni kweli alizaliwa na wazazi wake ni flani na flani. Hivyo hatutafika.
 
NARUDIA ACHA KUDANGANYA ,SIO KILA MWENYE ROHO MTAKATIFU ANANENA KWA LUGHA

Roho Mtakatifu hugawa karama kwa kila mtu kama apendavyo yeye, lakini hawapatii watu wote karama moja, zinatofautiana.

TWENDE KWENYE MAANDIKO

Lakini kazi hizi zote huzitenda Roho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye.” “Je! wote ni mitume? wote ni manabii? wote ni waalimu? wote wanatenda miujiza? wote wana karama za kuponya wagonjwa? wote wanena kwa lugha? wote wafasiri? Takeni sana karama zilizo kuu. Hata hivyo nawaonyesha njia iliyo bora.” “Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.” 1 Kor. 12:11, 29-31; 13:1-3.

Je, ni karama ipi ambayo tunatakiwa kuitafuta zaidi?​

“Ufuateni upendo, na kutaka sana karama za rohoni, lakini zaidi kwamba mpate kuhutubu.” 1 Kor. 14:1.
 
Utagundua pia, kama Biblia inawataja wanafunzi walipompokea mara ya kwanza Roho Mtakatifu walinena kwa lugha mpya kama ishara, hivyo kwa vyovyote vile Stephano alipitia hii ishara.
Tunaambiwa kwamba kila muumini katika Kristo ana Roho Mtakatifu (Warumi 8:9, 1 Wakorintho 12:13; Waefeso 1:13-14 ), lakini si kila muumini hunena lugha ngeni (1 Wakorintho 12:29-31).


1 Wakorintho 12:29-31 BHN​

Je, wote ni mitume? Wote ni manabii? Wote ni waalimu? Wote ni wenye kipaji cha kufanya miujiza? Je, wote ni wenye kipaji cha kuponya? Je, wote ni wenye kipaji cha kusema lugha ngeni? Je, wote hufafanua lugha? Muwe basi, na tamaa ya kupata vipaji muhimu zaidi. Nami sasa nitawaonesheni njia bora zaidi kuliko hizi zote
 
Kuzungumza katika lugha hakuna mahali kumewazilishwa kama kitu Wakristo wote wanapaswa kutarajia wakati wao wanampokea Yesu Kristo kama Mwokozi wao na hivyo kubatizwa katika Roho Mtakatifu. Kwa kweli, kati ya matukio yote kubadilika katika Agano Jipya, ni rekodi mbili tu zinazungumzia mazingira ya kunena katika lugha. Lugha ilikuwa zawadi ya kimiujiza ambayo ilikuwa na kusudi maalum kwa muda maalum. Haikuwa na kamwe haitakuwa, ushahidi pekee wa kupokea Roho Mtakatifu.
 

Kuhusu swali lako wapi Yesu alinena kwa lugha nalijibu kama ifuatavyo.

Mungu, ameiongoza dunia hata sasa kwa maongozi matatu ambayo ni

1. Maongozi ya Mungu Baba mwenyewe.

Hii ni agano la kale, na aliiongoza dunia kwa sheria kama tunavyoona wana wa Israel walivyopewa torati iliyojaa sheria.

2. Wakati wa Yesu Kristo. Sheria na Neema.

3. Wakati wa Roho Mtakatifu. Baada ya Yesu kuondoka.

Sasa nijibu, kipindi Yesu yupo Roho Mtakatifu wakati wake ulikuwa bado wa kudhihirishwa duniani. Ikumbukwe Yesu ni nafsi ya Mungu hivyo ni kawaida Roho kuwa ndani yake kwa sababu wote ni kitu kimoja.

Kama Yesu angekuwepo duniani hata sasa Roho Mtakatifu asingekuja, ila Yesu mwenyewe alisema hatatuacha peke yetu, atatuletea msaidizi ambaye ni Roho Mtakatifu, hivyo Roho Mtakatifu asingekuja kama Yesu tunaye hapa duniani wao ni kitu kimoja hawana sababu ya kuja kukinzana hapa duniani.

Hivyo Yesu asingeweza kufanya huo ukichaa wa kunena kwa lugha wakati majira ya Roho Mtakatifu yalikuwa bado, kwa sababu yeye bado alikuwepo. Ikumbukwe kunena kwa lugha ni ishara kwetu sisi wanadamu kuthibitisha tumempokea Roho Mtakatifu. Yesu yeye Roho yupo naye kila siku kabla hata ya kuumbwa kwa ulimwengu na wao ni mmoja, sasa kulikuwa na haja gani ya Yesu kufanya ukichaa wa kunena kwa lugha, haina haja.
 
My friend, pentecostalism (makanisa yoote ya evangelistic uliyoorodhesha hapo) yalianza wakati wa uamsho wa azusa street, hapo Roho Mtakatifu aliposhuka tena kwa karne nyingi sana baada ya kupotea. elewa kwamba, makanisa kama ya catholic waumini wake wa awali kabisa walikuwa wale wa mlengo wa mitume (Petro, hata ukienda pale vatican panaitwa st.Peter/santa puetro), Paul, Petro etc walianzisha.baadaye ile imani ya mitume ilikuja kupotea kabisa na Mungu akawa haabudiwi ila dini. trust me, hayo mnayoamini leo kweney catholic, sio yale walikuwa wanaamini na kuabudu mitume.

1. Mitume waliamini ujazo wa Roho Mtakatifu na kunena kwa lugha, ninyi hamuamini na hakuna aliyejazwa.
2. Mitume hawajawahi hata siku moja kuabudu wafu, ninyi mnaabudu na kuomba kwa wafu.
3. Mitume hawajawahi kuabudu Maria, ninyi Maria anaheshimiwa kuliko hata Mungu.
4. Mitume waliombea na kufukuza pepo wachafu. hakuna hata padre mwenye uwezo kukemea pepo leo. na wengi wanaenda kwa waganga
5. Mitume walizunguka dunia nzima kuhubiri injili, ninyi mnahubiri dini.
6. Mitume walijazwa na kutembea na nguvu za Mungu. ninyi hakuna nguvu za Mungu kwa padre wala askofu. ni dini tu.

kuna mengi. kitu pekee mlichoisaidia dunia ni kusambaza elimu dunia/mashule na vyuo. ila hata nikihudhuria misiba yenu padre ambaye amesoma miaka mingi mno akianza kuhubiri huwa nawaonea huruma kwasababu hajui Biblia na hana hata nguvu ya Mungu.

ushauri kwako. jua kwamba ,leo hii Yesu Kristo akirudi, kama wewe hauna Roho Mtakatifu, unaachwa.

Rum 8:9 Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.​


Matendo 19:1 1Wakati Apolo alipokuwa Korintho, Paulo alisafiri sehemu za bara, akafika Efeso ambako aliwakuta wanafunzi kadhaa. 2Akauliza, “Je, mlipopata kuwa waumini mlipokea Roho Mtakatifu?” Nao wakamjibu, “La! Hata hatujasikia kwamba kuna Roho Mtakatifu.” 3Naye akasema, “Sasa mlipata ubatizo wa namna gani?” Wakamjibu, “Ubatizo wa Yohane.” 4Naye Paulo akasema, “Ubatizo wa Yohane ulikuwa wa kuonesha kwamba watu wametubu. Yohane aliwaambia watu wamwamini yule ambaye alikuwa anakuja baada yake, yaani Yesu.” 5Baada ya kusikia hayo, walibatizwa kwa jina la Bwana Yesu. 6Basi, Paulo akawawekea mikono, na Roho Mtakatifu akawashukia, wakaanza kusema lugha ngeni na kutangaza ujumbe wa Mungu. 7Wote jumla walikuwa watu wapatao kumi na wawili.

"Na ishara hizi zitafuatana na hao waaminio; kwa jina langu watatoa pepo; watasema kwa lugha mpya, watashika nyoka; hata wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya." (Marko 16:17-18)

DISCLAIMER: pamoja na yote hayo niliyoandika, siungi mkono manabii wa kisasa wa kuuza mafuta, maji na chumvi badala ya kutumia Jina la Yesu. pia uwepo wao na kujifanya kwao kama ndio walokole hakumaanishi kwamba katika dunia hii hakuan walokole. kuna watu waliookoka wanaotembea na nguvu za Mungu hata leo hii, ila hao wachache wanaotafuta pesa kwa mgongo wa imani ni kama kenge kwenye kundi la mamba.
 

Sasa niweke CONCLUSION nipishe na wengine waje kujadili mada. Maana bado nina mengi na naona sitayamaliza.

CONCLUSION YANGU NI KAMA IFUATAVYO:

Roho Mtakatifu ndiyo ni kweli anamgawia mtu kadri anavyopenda yeye, hata karama za rohoni kuna atakayepewa nyingi kuna atakayepewa chache, ni kadri Roho atakavyopenda mwenyewe, hapangiwi. Hata kunena, kuna atakaye nena sana na kuna atakaye nena kidogo, ni kadri Roho atakavyopenda mwenyewe.


Roho Mtakatifu vilevile hana limitation, sio jukumu letu kumpangia Roho Mtakatifu utendaji na kumpangia idadi ya watu wanaopaswa kunena kwa lugha, akiamua watu wote wanene na asiwepo mtafsiri, wote watanena na hakuna atakaye tafsiri, akiamua wanene kumi na watafsiriwe itakuwa hivyo. Hivyo hatupaswi kumwingilia.


Kuhusu namna gani tunene, hilo pia sio jukumu letu kumpangia Roho Mtakatifu kwamba tunene kwa mfumo gani, ni kumruhusu tu atutumie tunene kama atakavyopenda yeye mwenyewe.


Mwisho kabisa, muhimu injili kusonga mbele na mwili wa Kristo uzidi kujengwa. Hayo mengine kuhusiana na Roho Mtakatifu ni sisi kuwa na utayari na kumruhusu Roho Mtakatifu mioyoni mwetu atutumie na kutupa karama zake mbalimbali kama atakavyopenda yeye mwenyewe.

Usikosoe wengine ila mwache Roho Mtakatifu afanye kazi yake na awatumie kama apendavyo yeye.
 
mkuu toka nje ya box, usibebwe na mafundisho usiyojua msingi wake, hivi kule unakoambiwa ni kunena kwa lugha, ulishafatilia vzr msingi wake?
"Nijaposema Kwa lugha za wanadamuna za malaika....".
Unazijua lugha za malaika utuambie zikoje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…