Freemasons ndani ya Makanisa

kunena kwa lugha kwa mujibu wa biblia sio huko mnakofanya ghasia makanisani kwa kufokafoka, lugha zisizoeleweka

Je, ni lugha ipi inayofaa kunena kanisani?​

“Lakini katika kanisa napenda kunena maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafudhisha wengine, zaidi ya kunena maneno kumi elfu kwa lugha.” 1 Kor. 14:19.

Ni afadhali kunena maneno machache yanayoeleweka kuliko elfu yasiyoeleweka.

Je, ni watu wangapi wanaruhusiwa kunena katika kusanyiko moja kanisani?​

“Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.” 1 Kor. 14:27.

Si zaidi ya watatu, tena wapeane zamu, na ni lazima ifasiriwe ili watu waelewe.
 
Unamuabuduje Mungu katika roho na kweli?
 

Mkuu nikushauri tu we kama unasali sali tu lakn ukitaka kujichanganya utapata unachokitaka usipende kufatilia mambo ya nje ya imani yako…
 
"Question religion,question it all.Questions exist untill them questions are solved"-JAY Z mnaemuita grandmaster.
 
Mkuu nikushauri tu we kama unasali sali tu lakn ukitaka kujichanganya utapata unachokitaka usipende kufatilia mambo ya nje ya imani yako…
mimi sifungwi na dini au dhehebu, nimeshatoka huko , sishikiwi akili na viongoz wa dini,
 
wewe ni mfuatiliaji mzuri, dunia ya sasa imebaki na watu wanaoshikiwa akili , na ni moja ya mafanikio ya freemason,
 
Evidence unayo mkuu juu ya hili...
 
mimi sifungwi na dini au dhehebu, nimeshatoka huko , sishikiwi akili na viongoz wa dini,

Kufungwa kidini ni weww kuamua kwako na kiongozi wa dini ni mtu tu ambae hana maana yoyote kwa unachokiabudu,,sijui we unawachukuliaje freemason kwa ufupi ni watu tu ambao anaweza ata asiwe kiongozi ila yupo kanisani kama kawaida au msikitini.
 
Nyinyi hamneni kwa lugha, ila mnadanganywa, hiyo ni kazi ya kikundi ndani ya freemason, kiitwacho KNIGHT OF TEMPLAR,

ni sawa tu na digrii ya 18 ya freemason iliyoingiza misalaba ndani ya madhehebu ya kikristo, na waumini kudhani inamuwakilisha YESU

MNAVYONENA NINYI NI TOFAUTI KABISA NA BIBLIA INAVYOSEMA, ILA KWAKUWA TAYARI MMESHAPANDIKIZWA MAFUNDISHO YA UONGO

Je, ni watu wangapi wanaruhusiwa kunena katika kusanyiko moja kanisani?​

“Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.” 1 Kor. 14:27.

Si zaidi ya watatu, tena wapeane zamu, na ni lazima ifasiriwe ili watu waelewe.

Je, hawa watatu wanaweza kunena maneno yasiyoeleweka?​

“Lakini na asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa.” 1 Kor. 14:28. “Haya! ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga na wasioamini, je! hawatasema ya kwamba mna wazimu?” 1 Kor. 14:23.

Hairuhusiwi kupiga makelele yasiyoeleweka kanisani! “Anyamaze kanisani!”

Lakini sasa, kwa nini watu wananena Lugha kinyume na utaratibu unaoelezwa na Biblia?​

“Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.” Ufu. 16:14.

Je, nitatofautishaje kati ya roho za mashetani na Roho Mtakatifu?​

“Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.” 1 Yoh. 4:1. “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.” Isa. 8:20.

Biblia inasema, “Na roho za manabii huwatii manabii. Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani, vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu” 1 Kor. 14:32,33.
 
Kufungwa kidini ni weww kuamua kwako na kiongozi wa dini ni mtu tu ambae hana maana yoyote kwa unachokiabudu,,sijui we unawachukuliaje freemason kwa ufupi ni watu tu ambao anaweza ata asiwe kiongozi ila yupo kanisani kama kawaida au msikitini.
Kwaaaahiyo nimebisha? au hoja yako ni ipi ndugu
 
natamani sana kuijua..kama hutojali.
Ngoja nieleze kidogo
Kumwabudu Mungu katika Roho: Inamaanisha kuwa na Roho Mtakatifu katika maisha yetu.

Kumwabudu Mungu katika kweli: Roho Mtakatifu, kama alivyosema Yesu kwamba, “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.” Yohana 14:26. Roho Mtakatifu ndiye hutufundisha na kutuwezesha kukaa katika ukweli, na ndio maana anaitwa Roho wa kweli.

Yn 14:16-17 “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.”

Mtu hawezi yeye mwenyewe kwa nguvu zake kumwabudu Mungu kwa kuifuata kweli. Ni lazima iwepo nguvu zaidi ambayo ni Roho ya Mungu itakayokaa ndani yake na kumwezesha kuitii kweli yote. Bila Roho Mtakatifu, mtu huwa hana bidii ya kumtafuta Mungu, huwa na chuki dhidi ya Mungu pale anapokutana na dhiki flani, huwa ni mwenye tamaa, huwa ni mwenye kila aina ya uovu.

Katika hali kama hiyo mtu hawezi kumwabudu Mungu katika kweli, wala hawezi kumpendeza Mungu hata kidogo, ingawa anaweza kujitahidi kwa kiasi flani na kujilazimisha kutii matakwa ya Mungu, lakini bado moyo wake unaichukia sheria ya Mungu, na kazi zote anazozifanya ili kutii matakwa ya Mungu, zinakuwa ni matendo ya kimwili tu, ambayo ni bure na hayampendezi Mungu, bali yanaongeza hasira kali ya Mungu juu yake. Hii ndiyo hali ya kutaka kuwa mwema mbele za Mungu kwa kuifanyia kazi sheria, kitu ambacho ni laana kwa mtu yeyote anayekifanya.

Lazima tujue kwamba “kumwabudu Mungu katika kweli”; hapa Yesu anamaanisha kumwabudu Mungu katika matakwa, au mapenzi yake yote; au kumwabudu kwa kuifuata haki yake yote ambayo ni sheria yake takatifu.

Kabla hatujaendelea zaidi kwanza tujue maana sahihi ya maneno haki, sheria, na kweli. Vinginevyo hakuna faida yoyote ya kujifunza somo hili.

“Haki” ni mambo yote yanayomfurahisha au yanayompendeza Mungu. “Sheria” ni njia ambayo Mungu anaitumia kuwajulisha watu haki yake, hivyo sheria ni maandishi, au maneno ambayo Mungu ameyaamuru yatekelezwe maana ndiyo yampendezayo au ndiyo haki yake. Wakati “Kweli” ni matokeo ya tendo lolote la haki ambalo tayari limekwishafanyika, hii ni kwa sababu ukweli hupatikana baada ya vipimo flani vya haki kufanyika. Kwa mfano: ukweli ni mafungu ya Maandiko yaliyokusanywa kwa pamoja ili kupata uwiano au balansi sahihi ya kitu kinacholengwa, na hiyo ni njia ya kupata kitu kwa njia ya haki, na kile kitu kinapopatikana ndio kinakuwa ni ukweli. Kwa kifupi ukweli ni tendo lolote la haki ambalo limehitimishwa, pia ukweli ni jambo lolote ambalo lipo, na liko sahihi.

Hivyo ukiangalia kwa makini utaona kuwa maneno, haki, sheria na kweli, hayatofautishwi katika maana moja kuu ambayo yote yanailenga, na maana hiyo ni kumpendeza Mungu au kufanya mambo ambayo Mungu anayapenda. Zaburi 119:151 inasema, “Ee Bwana. . .maagizo yako yote ni kweli” ikimaanisha sheria ya Mungu ndiyo kweli, lakini aya 172 inaongeza kwamba: “. . .Maagizo yako yote ni ya haki.” Hapa mwandishi anatambua kwamba sheria ndiyo kweli na haki ya Mungu, lakini katika aya 149 akaongeza tena kwamba: “Haki yako ni Haki ya milele, Na Sheria yako ni Kweli”. Haiwezi kusemwa wazi zaidi ya hapa, inaonekana wazi sana Biblia inayaunganisha maneno yote matatu kuwa kitu kimoja.
 

Kunena kwa lugha ni ujinga wa hao wanao nena kwa lugha zao za ajabu ajabu biblia imeweka wazi kama utanena kwa lugha basi unene palipo na mtu ambae ataifasiri hiyo lugha unayonena we waambie tu ukweli hawa watu wa kunena kwa lugha ni siasa za kidini nawez ita ivo
 
Asanthe kwa kuchukua mda wako kuelezea hili..roho mtakatifu anakujaje ndani yako?and hw will you know it.?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…