Freemasons ndani ya Makanisa

Freemasons ndani ya Makanisa

Kunena kwa Lugha kumeelezewa kwenye Biblia, na mitume wa kwanza walikaa mahali pamoja mpaka siku Roho Mtakatifu alipowaita na wakanena kwa Lugha mbalimbali. Sasa wewe unapotosha uongo eti Ni kurap. Kwa hivyo hata Biblia inasema uongo?. Naona kanisa linapogwa Vita Kila mahali.
kunena kwa lugha kwa mujibu wa biblia sio huko mnakofanya ghasia makanisani kwa kufokafoka, lugha zisizoeleweka

Je, ni lugha ipi inayofaa kunena kanisani?​

“Lakini katika kanisa napenda kunena maneno matano kwa akili zangu, nipate kuwafudhisha wengine, zaidi ya kunena maneno kumi elfu kwa lugha.” 1 Kor. 14:19.

Ni afadhali kunena maneno machache yanayoeleweka kuliko elfu yasiyoeleweka.

Je, ni watu wangapi wanaruhusiwa kunena katika kusanyiko moja kanisani?​

“Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.” 1 Kor. 14:27.

Si zaidi ya watatu, tena wapeane zamu, na ni lazima ifasiriwe ili watu waelewe.
 
INAMUATHIRI KUWA MTUMWA WA WATU, KULISHWA MAFUNDISHO YA UONGO AKIDHANI YA UKWELI, NA MWISHO WAKE KUIPOKEA ALAMA YA MNYAMA​

WITO...

Ufu 18:4 SUV​

Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.

YOHANA 4​

22Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. 23Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. 24Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.​

Mt 15:9 SUV​

Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu.
Unamuabuduje Mungu katika roho na kweli?
 
UTANGULIZI

ISAYA 14
12 Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!
13 Nawe ulisema moyoni mwako, Nitapanda mpaka mbinguni, Nitakiinua kiti changu juu kuliko nyota za Mungu; Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini.
14 Nitapaa kupita vimo vya mawingu, Nitafanana na yeye Aliye juu.
15 Lakini utashushwa mpaka kuzimu; Mpaka pande za mwisho za shimo

Hapo tunaona Shetani akiapa kwa MUNGU akisema"Nami nitaketi juu ya mlima wa mkutano, Katika pande za mwisho za kaskazini."

UKISOMA

Zaburi 48​

1 Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima wake mtakatifu.

2 Kuinuka kwake ni mzuri sana, Ni furaha ya dunia yote. Mlima Sayuni pande za kaskazini, Mji wa Mfalme mkuu.

UTAONA PANDE ZA KASKAZI NDIPO LILIPOKUWEPO HEKALU PALE MLIMA SAYUNI NA NDIPO MAHALI PALIPOKUWA NA UWEPO WA MUNGU , HIVO SHETANI ALIAPA KUKAA NADNI YA MAKANISA KWA SIKU ZETU AMBAPO TUNAKUSANYIKA TUKIAMINI TUNAMUABUDU MUNGU

Tuanze mada yetu sasa, fatana nami....

Katika FREEMASON Degree ya 33 ( hii ndio hatua ya juu ya Fremason kwa ujumla Duniani, huitwa"Degree of the Craft", na mwanachama mwenye Degree 3, anaitwa Mastermasonry/Grand master, hawa ndio wapangaji wa mipango, hawa ndio wanao jua siri ya free masoni na hii degree unaipatia katika Blue Lodge.
Freemason, imegawanyika katika Vyama mbali mbali lakini vyote hujulikana kwa jina la freemason, na kila chama kina jiendesha kwa misingi yake, mfano York rite na scottish rite.
York rite, hii inapatikana marekani katika lodge za huko, na katika york rite , wao waliongeza degree 10, za ziada, lakini huwezi kupata hizi degree bila kuwa na degree tatu , ambazo ndio msingi wa freemason Duniani kwote..na katika York rite degree ya 10, na maanisha ya 13, ukijumlisha na zile degree tatu za msingi, hiyo ni hatua ya juu ambayo inaitwa the Order of the Temple, na mwanachama mwenye degree hizi anaitwa "Knight templar".

Katika Scottish rite, katika chama cha scotiland, kupitia Lodge zao, wao waliongeza Degree 30, na kuzifanya ziwe 33, na huwezi kupata hizi degree bila kuwa na degree 3, za msingi. katika hizi degre, degree ya 32, ndio degree ya juu kabisa ambayo mwana chama mwenye hatua hii anakuwa Master of the royal secreat, siri zote za freemason unapewa.

Japo katika scottish rite , kuna jumla ya degree 33, lakini freemason wana amini degree ya 33, haipo, kwasababu ni adimu sana , labda mtu mwenye IQ, kubwa kama 160, na kama wapo basi wana fahamika na freemasoni wenye degree za juu kabisa.
wapo watu wanao amini labda hii degree ya 33, hii ndio degree inayo muhusu Lucifer.. pia baadhi wana amini Albert pike, mwandishi wa kitabu cha "Morals and dogma" alikuwa na degree 33, lakini wapo ambao wana amini hakufikia hatua hiyo.
Freemason ni chama ambacho kina daiwa kuwa na mambo ya siri mengi, na hawa inasemekana wanachama wake wengi wenye degree za juu , wapo katika chama cha Illuminat.

Unaweza kuona aina za digrii hizo; kwa mfano digrii ya 18 inayoitwa ‘Knight of Rose Croix’ hushughulika na elimu ya aina za misalaba na jinsi ya kufanisha kuziingiza ndani ya taasisi na madhehebu mbalimbali kwa imani ya Illuminati na freemason na kwa kweli freemason wa digrii hiyo wamefanikiwa kwa kiwango cha juu kabisa kuingiza aina nyingizi za misalaba ndani ya makanisa na taasisi bila ya waumini kujua maana ya misalaba hiyo.

NAKUPA MFANO HAPA CHINI
View attachment 2104330

NI chama cha Prieure de Sion (Priory de Sion) kilichoanzishwa na familia ya 11 ya Illuminati inayoitwa Freeman Illuminati bloodlines ndicho kilichosababisha kuanzishwa kwa ‘Uprotestant’ au ‘Upinzani’ ndani ya dini. Wakainuka mashujaa wengi waliopinga mafundisho machafu yaliyoingizwa ndani ya imani ya kweli ili kutetea neno la Mungu litawale tofauti na mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu. Miongoni mwa mashujaa walioinuka kupingana na mafundisho ya chama cha Prieure de Sion alikuwa Martin Luther.

Kumbuka kwamba wapinzani ‘Protestants’hawa walikuwa wanapinga mafundisho wakiwa ndani ya mifumo ya dini zao. Hata hivyo hawakufanikiwa kuleta matokeo mazuri ya upinzani wao na hivyo wakaamua kutoka na kujitenga na dini wakiwa na baadhi ya mafundisho machafu waliyoyarithi kutoka kwenye mifumo potofu ya kidini. Wakiwa wamejitenga, sasa waliamua kufanya ‘matengenezo’ kwa lengo la kuondoa mafundisho machafu na kubaki na mafundisho safi kama ilivyoagizwa na Mungu. Hivyo jina lao wakaitwa‘Reformers’ au ‘Wanamatengenezo’ badala ya ‘Protestants’ au ‘wapinzani’.‘Waprotestants’ wa awali walijua maana ya kanisa na ndio maana hawakuona shida kujitenga na mifumo iliyokuwa inadhaniwa kuwa ndiyo kanisa.Lakini je, nani aliyeanzisha ‘Uprotestant’na ‘matengenezo’? Ellen White anasema: “Christ was a protestant...TheReformersdate back to Christ and the apostles. They came out and separated themselves from a religion of forms and ceremonies. Lutherand his followers did not invent the reformed religion. They simply accepted it as presented by Christ and the apostles." E.G. White, Review and Herald, vol. 2, 48, col. 2.

Hapo anamaanisha kwamba ‘Kristo (Yesu) alikuwa ni Mprotestant….wanamatengenezo waliiga kutoka kwa Kristo na mitume. Walijitenga na dini ya desturi na sherehe. Luther na wafuasi wake hawakuanzisha dini ya matengenezo. Waliikubali kama ilivyoonyeshwa na Kristo na mitume’ [rejea: R&H, Vol. 2, 48, col.2].

Ni kwa namna gani Kristo alijitenga? E. White anaendelea kusema: “Pharisees and Sadducees were alike silenced.Jesus summoned His disciples, and prepared to leave the temple, not as one defeated and forced from the presence of his adversaries, but as one whose work was accomplished. He retired a victor from the contest”. {DA 620.2}

‘Mafarisayo na masadukayo walinyamazishwa. Yesu aliwakusanya wanafunzi wake, na akawaandaa kuliacha hekalu, sio kama aliyeshindwa na kulazimishwa kuondoka kwa maadui zake, bali kama ambaye kazi yake ilikuwa imekamilika. Alikuwa ni mshindi katika mashindano”. {DA 620.2}

Biblia inasema kwamba Yesu alijitahidi kupingana na mafarisayo na masadukayo akiwa ndani ya mfumo wa dini ya kiyahudi na sasa alikuwa amefikia mwisho wa upinzani wake na akaamua kujitenga moja kwa moja na mfumo wa dini hiyo ili awafundishe vizuri wanafunzi wake ambao walikuwa tayari kukubali mafundisho safi.

E.G. White anasema:" Hitherto He had called the temple His Father's house; but now, as the Son of God should pass out from those walls, God's presence would be withdrawn forever from the temple built to His glory. Henceforth its ceremonies would be meaningless, its services a mockery. {DA 620.4}Hatimaye Yesu na wanafunzi wake walijitenga na hekalu lililokuwa mpendwa wao. Lakini kwa sababu viongozi wa hekalu walikataa kufuata mafundisho ya neno la Mungu peke yake, Mwana wa Mungu hakuona sababu ya kuendelea kubaki ndani ya hekalu ingawa “Alikuwa akiliita hekalu kuwa ni nyumba ya Baba yake; lakini sasa, kama Mwana wa Mungu ambavyo akipita kutoka katika kuta hizo, uwepo wa Mungu ungeondolewa milele usionekane ndani ya hekalu lililojengwa kwa utukufu Wake. Hivyo sherehe zilizofanyika ndani ya hekalu hazikuwa na maana, huduma zake zikawa dhihaka”. {DA 620.4}. Hivyo ndivyo alivyofanya Martin Luther na wafuasi wake.

Baada ya kifo cha Martin Luther, wafuasi wake waliendelea katika kufanya matengenezo. Hata hivyo kwa sababu freemasons hawakati tamaa, matengenezo yalikoma na kuanza kurudi nyuma taratibu ambapo leo hii wale wanaoitwa ‘Walutheri’ wameungana tena na mfumo ambao mwanzilishi wao, Martin Luther, aliuiita ‘mfumo mchafu’.

Wakati matengenezo yanaendelea, ulikuwa ni wakati wa kutimizwa kwa unabii wa siku 1260 sawa na miaka 1260 kama ilivyotabiriwa na nabii Yohana. Wakati huo kulianzishwa matengenezo mengi na kupelekea kuanzishwa kwa mifumo mingine ya makanisa. Baadhi ya makanisa yaliyoanzishwa yalikuwa haya:

Anglican: Lilianzishwa huko England na mfalme wa Uingereza ili kupinga kanisa la Roma. Kiongozi mkuu wa kanisa hilo ni Malkia wa Uingereza. Hata hivyo wachunguzi wa dini ya freemasons wanasema kwamba familia ya Malkia ni familia mojawapo kati ya familia 13 za waumini wa Freemasons.

Presbyterian: Mwanzilishi ni John Calvin mwaka 1509 – 1564 na John Knox 1505 – 1572. Kanisa hili lilijitenga na Roma likiwa na motto “Chunguza maandiko” maana liliona kwamba kanisa la Roma linakwenda kinyume na maandiko. Hata hivyo wafuasi wa John Calvin na John Knox wameshindwa kufikia malengo ya kuyachunguza maandiko na kufuata kile asemacho Mungu na badala yake wamekubali kurudi walikotoka!

MENNONITE: Lilizaliwa rasmi mwaka 1525 – 1530 na Conrad Grebel na wenzake akiwemo Zwingli Ulrich aliyetofautiana na Martin Luther juu ya somo la pasaka. Hawa walikataa ubatizo wa Roma wa kunyunyizia maji na jina jingine wanaitwa “Meno Knights” majina ambayo yanafanana na vikundi vya Freemason kama vile “The knights of Eulogia”(Skull and Bones), “The knights of Malta”. Ingawa lengo la Zwingli Ulrich lilikuwa zuri, baada ya kifo chake wafuasi wake walikubali kuingiliwa na freemasons na hivyo kushindwa kufikia lengo lililokusudiwa.

LUTHERAN: Mwanzilishi ni Martin Luther mwaka 1517. Alikuwa ni Mjerumani aliyesomea ukasisi wa kanisa la Roma na mwaka 1511 akapata Phd katika chuo kikuu cha Wattenberg. Alipingana na kanisa lake la Roma na kuandika sababu 95 zinazopinga mafundisho ya Roma ndipo akajitenga na Roma na hivyo wafuasi wake wakaendelea kutumia jina la Lutheran, yaani wafuasi wa Luther. Wafuasi wa Luther hawakuendelea mbele na sasa wamerudi kwenye makosa aliyokuwa akiyapinga Luther. Je, Lutheran wa leo wanafuata kweli nyayo za Martin Luther? Au wametekwa kwa matumizi ya njama ya “Following Gurus”yaani kufuata kila wasemacho viongozi? Tafakari!

Moravian: Mwanzilishi ni John Huss aliyezaliwa mwaka 1366 na kuchomwa moto na papa hadi kufa mwaka 1416 baada ya kulipinga kanisa la Roma. Wafuasi wake hadi leo wanaitwa kanisa la Moravian. Kwa bahati mbaya wafuasi wa John Huss hawakuendelea kufanya matengezo ili kusonga mbele zaidi ya Huss na kibaya zaidi ni kwamba wanarudi nyuma badala ya kusonga mbele. Leo Huss akifufuka atashangaa kuona jinsi wafuasi wake walivyoacha kanuni alizozianzisha. Je, wamoravian wa leo wako tayari kuchomwa moto kwa kutetea ukweli kama John Huss? Tafakari!

Baptist: Ni kanisa lililoanzishwa na wafuasi wa Martin Luther ambao walijitenga na Lutheran mwaka 1600 huko Uholanzi na Uingereza baada ya kuona kwamba wafuasi wenzao wameacha kanuni alizoziweka Martin Luther. Hata hivyo kanisa la Baptist la leo haliendeleza jitihada za Luther na sasa badala ya kusonga mbele linapiga ‘marktime’ likiwa limegeuka nyuma.

Salvation Army (Jeshi la Wokovu): Mwanzilishi ni Booth mwaka 1878. Kanisa hili lilianzishwa na wafuasi wa freemasons kwa lengo la kuchafua matengenezo ya kweli. Kumbuka kwamba Shetani hutumia fursa inayotolewa na Mungu akiwa na lengo la kuwafanya watu washindwe kujua kipi ni cha kweli na kipi sio. Katika kila matengenezo ya kweli, pamekuwepo na matengenezo bandia.

Marmon church: Mwanzilishi ni Joseph Smith (1805 – 1844). Kanisa hili linajulikana pia kama The church of Jesus Christ of later day saints. Kanisa la Mormon lilianzishwa na wafuasi wa freemason wakiwa na lengo la kuchafua matengenezo ya kweli. Mitt Romney ni muumini wa kanisa la Mormon.

Methodist: Kiongozi Mwanzilishi ni John Wesley. Lilianzishwa na watu 17 wa familia moja mwaka 1738 likiwa na lengo la kupinga mafundisho ya freemasons. Kanisa hilo halijakamilisha lengo la matengenezo kutokana na ukweli kwamba wafuasi wake hawana mwamko aliokuwa nao John Wesley.

Watch Tower/Mashahidi wa YEHOVA : Mwanzilishi ni Charles T. Russel 1852 – 1916 na mwenzake J. Lutheford 1869 – 1942. Baba yake Charles T. Russel alikuwa ni mchungaji wa Prebyterian. Mnamo mwaka 1932 huko Marekani jina la kanisa hilo lilibadilishwa na kuitwa Mashahidi wa Yehova. Markus Mpangala ameelezea kwa kirefu chanzo cha dhehebu hili akiainisha kwamba waanzilishi walikuwa ni Freemasons kutoka kwenye familia ya Illuminati inayoitwa Russel illuminati bloodline ambayo nimeshaielezea kwenye makala zilizopita.

Brethen Assemblies: Mwanzilishi ni ndg. Dabi 1800 – 1882 ambaye alikuwa ni muumini wa Anglican na akajitenga na kanisa hilo na kuanzisha kanisa lake. Dabi aliamua kujitenga na Anglican kutokana na kanisa hilo kutawaliwa na familia ya freemasons.

Makanisa ya Kipentekoste au kilokole: Ni makanisa yaliyoanzishwa miaka ya hivi karibuni. Makanisa haya yalianzishwa huko Kansas City Marekani mwaka 1901kwa lengo la kupata nguvu ya kile kinachoaminiwa kuwa roho mtakatifu. Je, unajua uhusiano uliopo kati ya muziki wa‘rap’ au ‘kufoka’ na uvuvio wa kunena kwa lugha kutoka kwa kile kinachoaminiwa kuwa ni nguvu za roho mtakatifu wakati waumini wa kilokole wanapokuwa wakiomba? Kumbuka kwamba Muziki wa rap ulianzia huko Kansas City Marekani, mahali ambako makanisa ya kipentekoste yalianzishwa. Panapo majaaliwa, nitakuwa na makala ndefu kuhusu asili, lengo na nguvu inayoonekana kwa viongozi wa makanisa ya kilokole kama kina mwamposa. Kwa wakati huu nasema,‘Soma Biblia na Tafakari’!

Gospel terbenacle: Mwanzilishi ni Pastor A.B. Simpson mwaka 1881 akitokea Presybiterian.

Christian Churches: Mwanzilishi ni Thomas Chapel mwaka 1807 akitokea Presybiterian.

Seventh –Day Advetist Church: Mwaka 1844 baada ya kutokurejea kwa Yesu duniani kama ilivyohubiriwa na muhubiri mashuhuri aitwaye William Miller, watu wengi walivunjika moyo isipokuwa watu 50 tu ndio walioendelea kujifunza Biblia miongoni mwao akiwa ni Ellen G. White. Watu hao waliendelea kuchunguza makosa yaliyofanywa na William Miller maana wao pia waliamini juu ya marejeo ya Yesu tarehe 22/10/1844. Hatimaye mwaka 1863 kanisa hilo likapewa jina la Seventh –Day Adventists Church huku likiwa na motto au kauli mbiu ya “Amri za Mungu na imani ya Yesu na Ujumbe wa malaika watatu” na baadaye kanisa hilo likawa chini ya rais wa General Conference ya SDA makao makuu yake yakiwa huko Marekani. Rais huyo ndiye kiongozi (kichwa) mkuu wa kanisa hilo duniani na huchaguliwa kila baada ya miaka mitano. Wakati viongozi wa kanisa walipokutana ili kujadili mambo ya kanisa, palikuwa na ‘Mwenyekiti’(Chairman of General Conference) ambaye aliongoza kikao hadi mwisho. Baada ya kikao kumalizika, mwenyekiti huyo alimaliza muda na kazi yake.

Hata hivyo kulitokea mabadiliko kutoka mwenyekiti wa baraza kuu hadi na rais wa kanisa ulimwenguni. Kila baada ya miaka mitano hufanyika uchaguzi wa kumpata rais wa kanisa hilo. Tofauti na makanisa mengine, kanisa hili linaabudu siku ya Jumamosi wakati makanisa mengine yanaabudu siku ya jumapili. Sasa hivi kuna makanisa mengi ya SDA ambayo yametoka ndani ya kanisa la ‘General conference of Seventh-Day Adventists’(GCSDA) kwa madai kwamba kanisa hilo limeingiliwa na freemasons.

Wengi wa waumini wa SDA waliojitenga na GCSDA wanasema kwamba walikuwa wakipinga‘protest’ mafundisho machafu huku wakiendelea kuwa ndani ya GCSDA lakini hawakuweza kuleta mabadiliko yoyote maana hali ilikuwa inazidi kuwa mbaya. Hatimaye waumini hao waliamua kufuata nyayo za akina Luther za kujitenga na sasa wanafanya ‘reformation’ au ‘matengenezo’ hatua kwa hatua maana walitoka na mafundisho machafu ambayo waliyapokea kama kweli wakiwa ndani ya GCSDA.Waumini hao wanadai kwamba walijitenga na GCSDA kwa sababu,

tukio kubwa ikiwa ni freemason kuingiza nembo yao,huku wakiiondoa ile nembo ya UJUMBE WA MALAIKA WATATU,Freemeson huingiza mafundisho, au alama zao kupitia viongozi wa juu wa kanisa kama ilivyo kawaida ya makanisa yote uyajuayo.

NEMBO YA AWALI YA SDA
View attachment 2104350
NEMBO YA SASA YA SDA
View attachment 2104361
View attachment 2104363
Je, madai hayo ni kweli? Tafakari!

Msingi wa kanisa la SDA au ‘Wasabato’ kama inavyojulikana kwa wengi,kuabudu siku ya jumamosi, ni kile kilichoandikwa na Mungu wakati wa uumbaji, kwamba aliumba kwa siku 6 na siku ya 7 akastarehe, akaibariki na akapumzika kisha akawaambia waisraeli: “Ikumbuke siku ya Sabatou itakase….” Kutoka 20:8.

Kutokana na kazi ya chama cha Priory de Sion kwa kuingiza mafundisho machafu ndani ya imani safi, kulitokea utitiri wa makanisa mengi ambayo yanadai kupinga uchafu huo. Hata hivyo wengi wa waumini wa madhehebu hayo ama hawajui asili ya dhehebu lao au hawajui asili ya kile wanachokiabudu. Wengi wamefundishwa na waalimu wa dini na kuwaamini bila hata ya kutaka kuhakikisha kwa akili zao kile wanachofundhishwa. Mungu ametoa nafasi ya kufahamu ukweli kwa kila mmoja wetu bila ya kutegemea viongozi wa dini. Umewahi kufikiri kwamba kama ungekuwa unaishi duniani wewe peke yako, ungemtegemea nani? Tafakari!

Mkuu nikushauri tu we kama unasali sali tu lakn ukitaka kujichanganya utapata unachokitaka usipende kufatilia mambo ya nje ya imani yako…
 
"Question religion,question it all.Questions exist untill them questions are solved"-JAY Z mnaemuita grandmaster.
 
Chief, is Elon Musk a member of the United Grand Lodge of England and a member of the Ancient and Accepted Scottish Rite of Freemasonry?
The United Grand Lodge of England is the highest degree of Freemasonry. The Ancient and Accepted Scottish Rite of Freemasonry is a degree that requires at least 3 years of study in a lodge of the Scottish Rite to be initiated.

The Scottish Rite is the oldest and largest international fraternal organization in the world. If that is the case, he is in a position to have in-depth knowledge of what is going in the planet Mars.
wewe ni mfuatiliaji mzuri, dunia ya sasa imebaki na watu wanaoshikiwa akili , na ni moja ya mafanikio ya freemason,
 
Chief, is Elon Musk a member of the United Grand Lodge of England and a member of the Ancient and Accepted Scottish Rite of Freemasonry?
The United Grand Lodge of England is the highest degree of Freemasonry. The Ancient and Accepted Scottish Rite of Freemasonry is a degree that requires at least 3 years of study in a lodge of the Scottish Rite to be initiated.

The Scottish Rite is the oldest and largest international fraternal organization in the world. If that is the case, he is in a position to have in-depth knowledge of what is going in the planet Mars.
Evidence unayo mkuu juu ya hili...
 
mimi sifungwi na dini au dhehebu, nimeshatoka huko , sishikiwi akili na viongoz wa dini,

Kufungwa kidini ni weww kuamua kwako na kiongozi wa dini ni mtu tu ambae hana maana yoyote kwa unachokiabudu,,sijui we unawachukuliaje freemason kwa ufupi ni watu tu ambao anaweza ata asiwe kiongozi ila yupo kanisani kama kawaida au msikitini.
 
Wewe Ni muongo Sana. Na unadhani wewe ndio upo sahihi. Huwezi kuongelea imani ambayo huiishi. Kama hujawahi kunena kwa Lugha utawezaje kuongelea kuhusu kunena kwa Lugha.

Mnawatukuza free Mason kana kwamba ndio Mungu. Acheni ujinga, unajua historia ya upentekoste ilovyoaanza au unaongea tu kwa sababu umeshiba ugali?. Mnawwbudu free Mason mpaka hata Maisha yenu wenyewe mnayaona hayana dhamamni.
Nyinyi hamneni kwa lugha, ila mnadanganywa, hiyo ni kazi ya kikundi ndani ya freemason, kiitwacho KNIGHT OF TEMPLAR,

ni sawa tu na digrii ya 18 ya freemason iliyoingiza misalaba ndani ya madhehebu ya kikristo, na waumini kudhani inamuwakilisha YESU

MNAVYONENA NINYI NI TOFAUTI KABISA NA BIBLIA INAVYOSEMA, ILA KWAKUWA TAYARI MMESHAPANDIKIZWA MAFUNDISHO YA UONGO

Je, ni watu wangapi wanaruhusiwa kunena katika kusanyiko moja kanisani?​

“Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.” 1 Kor. 14:27.

Si zaidi ya watatu, tena wapeane zamu, na ni lazima ifasiriwe ili watu waelewe.

Je, hawa watatu wanaweza kunena maneno yasiyoeleweka?​

“Lakini na asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa.” 1 Kor. 14:28. “Haya! ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga na wasioamini, je! hawatasema ya kwamba mna wazimu?” 1 Kor. 14:23.

Hairuhusiwi kupiga makelele yasiyoeleweka kanisani! “Anyamaze kanisani!”

Lakini sasa, kwa nini watu wananena Lugha kinyume na utaratibu unaoelezwa na Biblia?​

“Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.” Ufu. 16:14.

Je, nitatofautishaje kati ya roho za mashetani na Roho Mtakatifu?​

“Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.” 1 Yoh. 4:1. “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.” Isa. 8:20.

Biblia inasema, “Na roho za manabii huwatii manabii. Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani, vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu” 1 Kor. 14:32,33.
 
Kufungwa kidini ni weww kuamua kwako na kiongozi wa dini ni mtu tu ambae hana maana yoyote kwa unachokiabudu,,sijui we unawachukuliaje freemason kwa ufupi ni watu tu ambao anaweza ata asiwe kiongozi ila yupo kanisani kama kawaida au msikitini.
Kwaaaahiyo nimebisha? au hoja yako ni ipi ndugu
 
natamani sana kuijua..kama hutojali.
Ngoja nieleze kidogo
Kumwabudu Mungu katika Roho: Inamaanisha kuwa na Roho Mtakatifu katika maisha yetu.

Kumwabudu Mungu katika kweli: Roho Mtakatifu, kama alivyosema Yesu kwamba, “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.” Yohana 14:26. Roho Mtakatifu ndiye hutufundisha na kutuwezesha kukaa katika ukweli, na ndio maana anaitwa Roho wa kweli.

Yn 14:16-17 “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.”

Mtu hawezi yeye mwenyewe kwa nguvu zake kumwabudu Mungu kwa kuifuata kweli. Ni lazima iwepo nguvu zaidi ambayo ni Roho ya Mungu itakayokaa ndani yake na kumwezesha kuitii kweli yote. Bila Roho Mtakatifu, mtu huwa hana bidii ya kumtafuta Mungu, huwa na chuki dhidi ya Mungu pale anapokutana na dhiki flani, huwa ni mwenye tamaa, huwa ni mwenye kila aina ya uovu.

Katika hali kama hiyo mtu hawezi kumwabudu Mungu katika kweli, wala hawezi kumpendeza Mungu hata kidogo, ingawa anaweza kujitahidi kwa kiasi flani na kujilazimisha kutii matakwa ya Mungu, lakini bado moyo wake unaichukia sheria ya Mungu, na kazi zote anazozifanya ili kutii matakwa ya Mungu, zinakuwa ni matendo ya kimwili tu, ambayo ni bure na hayampendezi Mungu, bali yanaongeza hasira kali ya Mungu juu yake. Hii ndiyo hali ya kutaka kuwa mwema mbele za Mungu kwa kuifanyia kazi sheria, kitu ambacho ni laana kwa mtu yeyote anayekifanya.

Lazima tujue kwamba “kumwabudu Mungu katika kweli”; hapa Yesu anamaanisha kumwabudu Mungu katika matakwa, au mapenzi yake yote; au kumwabudu kwa kuifuata haki yake yote ambayo ni sheria yake takatifu.

Kabla hatujaendelea zaidi kwanza tujue maana sahihi ya maneno haki, sheria, na kweli. Vinginevyo hakuna faida yoyote ya kujifunza somo hili.

“Haki” ni mambo yote yanayomfurahisha au yanayompendeza Mungu. “Sheria” ni njia ambayo Mungu anaitumia kuwajulisha watu haki yake, hivyo sheria ni maandishi, au maneno ambayo Mungu ameyaamuru yatekelezwe maana ndiyo yampendezayo au ndiyo haki yake. Wakati “Kweli” ni matokeo ya tendo lolote la haki ambalo tayari limekwishafanyika, hii ni kwa sababu ukweli hupatikana baada ya vipimo flani vya haki kufanyika. Kwa mfano: ukweli ni mafungu ya Maandiko yaliyokusanywa kwa pamoja ili kupata uwiano au balansi sahihi ya kitu kinacholengwa, na hiyo ni njia ya kupata kitu kwa njia ya haki, na kile kitu kinapopatikana ndio kinakuwa ni ukweli. Kwa kifupi ukweli ni tendo lolote la haki ambalo limehitimishwa, pia ukweli ni jambo lolote ambalo lipo, na liko sahihi.

Hivyo ukiangalia kwa makini utaona kuwa maneno, haki, sheria na kweli, hayatofautishwi katika maana moja kuu ambayo yote yanailenga, na maana hiyo ni kumpendeza Mungu au kufanya mambo ambayo Mungu anayapenda. Zaburi 119:151 inasema, “Ee Bwana. . .maagizo yako yote ni kweli” ikimaanisha sheria ya Mungu ndiyo kweli, lakini aya 172 inaongeza kwamba: “. . .Maagizo yako yote ni ya haki.” Hapa mwandishi anatambua kwamba sheria ndiyo kweli na haki ya Mungu, lakini katika aya 149 akaongeza tena kwamba: “Haki yako ni Haki ya milele, Na Sheria yako ni Kweli”. Haiwezi kusemwa wazi zaidi ya hapa, inaonekana wazi sana Biblia inayaunganisha maneno yote matatu kuwa kitu kimoja.
 
Nyinyi hamneni kwa lugha, ila mnadanganywa, hiyo ni kazi ya kikundi ndani ya freemason, kiitwacho KNIGHT OF TEMPLAR,

ni sawa tu na digrii ya 18 ya freemason iliyoingiza misalaba ndani ya madhehebu ya kikristo, na waumini kudhani inamuwakilisha YESU

MNAVYONENA NINYI NI TOFAUTI KABISA NA BIBLIA INAVYOSEMA, ILA KWAKUWA TAYARI MMESHAPANDIKIZWA MAFUNDISHO YA UONGO

Je, ni watu wangapi wanaruhusiwa kunena katika kusanyiko moja kanisani?​

“Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri.” 1 Kor. 14:27.

Si zaidi ya watatu, tena wapeane zamu, na ni lazima ifasiriwe ili watu waelewe.

Je, hawa watatu wanaweza kunena maneno yasiyoeleweka?​

“Lakini na asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa.” 1 Kor. 14:28. “Haya! ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja, na wote wanene kwa lugha, kisha ikawa wameingia watu wajinga na wasioamini, je! hawatasema ya kwamba mna wazimu?” 1 Kor. 14:23.

Hairuhusiwi kupiga makelele yasiyoeleweka kanisani! “Anyamaze kanisani!”

Lakini sasa, kwa nini watu wananena Lugha kinyume na utaratibu unaoelezwa na Biblia?​

“Hizo ndizo roho za mashetani, zifanyazo ishara, zitokazo na kuwaendea wafalme wa ulimwengu wote kuwakusanya kwa vita ya siku ile kuu ya Mungu Mwenyezi.” Ufu. 16:14.

Je, nitatofautishaje kati ya roho za mashetani na Roho Mtakatifu?​

“Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.” 1 Yoh. 4:1. “Na waende kwa sheria na ushuhuda; ikiwa hawasemi sawasawa na neno hili, bila shaka kwa hao hapana asubuhi.” Isa. 8:20.

Biblia inasema, “Na roho za manabii huwatii manabii. Kwa maana Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani, vile vile kama ilivyo katika makanisa yote ya watakatifu” 1 Kor. 14:32,33.

Kunena kwa lugha ni ujinga wa hao wanao nena kwa lugha zao za ajabu ajabu biblia imeweka wazi kama utanena kwa lugha basi unene palipo na mtu ambae ataifasiri hiyo lugha unayonena we waambie tu ukweli hawa watu wa kunena kwa lugha ni siasa za kidini nawez ita ivo
 
Ngoja nieleze kidogo
Kumwabudu Mungu katika Roho: Inamaanisha kuwa na Roho Mtakatifu katika maisha yetu.

Kumwabudu Mungu katika kweli: Roho Mtakatifu, kama alivyosema Yesu kwamba, “Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.” Yohana 14:26. Roho Mtakatifu ndiye hutufundisha na kutuwezesha kukaa katika ukweli, na ndio maana anaitwa Roho wa kweli.

Yn 14:16-17 “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.”

Mtu hawezi yeye mwenyewe kwa nguvu zake kumwabudu Mungu kwa kuifuata kweli. Ni lazima iwepo nguvu zaidi ambayo ni Roho ya Mungu itakayokaa ndani yake na kumwezesha kuitii kweli yote. Bila Roho Mtakatifu, mtu huwa hana bidii ya kumtafuta Mungu, huwa na chuki dhidi ya Mungu pale anapokutana na dhiki flani, huwa ni mwenye tamaa, huwa ni mwenye kila aina ya uovu.

Katika hali kama hiyo mtu hawezi kumwabudu Mungu katika kweli, wala hawezi kumpendeza Mungu hata kidogo, ingawa anaweza kujitahidi kwa kiasi flani na kujilazimisha kutii matakwa ya Mungu, lakini bado moyo wake unaichukia sheria ya Mungu, na kazi zote anazozifanya ili kutii matakwa ya Mungu, zinakuwa ni matendo ya kimwili tu, ambayo ni bure na hayampendezi Mungu, bali yanaongeza hasira kali ya Mungu juu yake. Hii ndiyo hali ya kutaka kuwa mwema mbele za Mungu kwa kuifanyia kazi sheria, kitu ambacho ni laana kwa mtu yeyote anayekifanya.

Lazima tujue kwamba “kumwabudu Mungu katika kweli”; hapa Yesu anamaanisha kumwabudu Mungu katika matakwa, au mapenzi yake yote; au kumwabudu kwa kuifuata haki yake yote ambayo ni sheria yake takatifu.

Kabla hatujaendelea zaidi kwanza tujue maana sahihi ya maneno haki, sheria, na kweli. Vinginevyo hakuna faida yoyote ya kujifunza somo hili.

“Haki” ni mambo yote yanayomfurahisha au yanayompendeza Mungu. “Sheria” ni njia ambayo Mungu anaitumia kuwajulisha watu haki yake, hivyo sheria ni maandishi, au maneno ambayo Mungu ameyaamuru yatekelezwe maana ndiyo yampendezayo au ndiyo haki yake. Wakati “Kweli” ni matokeo ya tendo lolote la haki ambalo tayari limekwishafanyika, hii ni kwa sababu ukweli hupatikana baada ya vipimo flani vya haki kufanyika. Kwa mfano: ukweli ni mafungu ya Maandiko yaliyokusanywa kwa pamoja ili kupata uwiano au balansi sahihi ya kitu kinacholengwa, na hiyo ni njia ya kupata kitu kwa njia ya haki, na kile kitu kinapopatikana ndio kinakuwa ni ukweli. Kwa kifupi ukweli ni tendo lolote la haki ambalo limehitimishwa, pia ukweli ni jambo lolote ambalo lipo, na liko sahihi.

Hivyo ukiangalia kwa makini utaona kuwa maneno, haki, sheria na kweli, hayatofautishwi katika maana moja kuu ambayo yote yanailenga, na maana hiyo ni kumpendeza Mungu au kufanya mambo ambayo Mungu anayapenda. Zaburi 119:151 inasema, “Ee Bwana. . .maagizo yako yote ni kweli” ikimaanisha sheria ya Mungu ndiyo kweli, lakini aya 172 inaongeza kwamba: “. . .Maagizo yako yote ni ya haki.” Hapa mwandishi anatambua kwamba sheria ndiyo kweli na haki ya Mungu, lakini katika aya 149 akaongeza tena kwamba: “Haki yako ni Haki ya milele, Na Sheria yako ni Kweli”. Haiwezi kusemwa wazi zaidi ya hapa, inaonekana wazi sana Biblia inayaunganisha maneno yote matatu kuwa kitu kimoja.
Asanthe kwa kuchukua mda wako kuelezea hili..roho mtakatifu anakujaje ndani yako?and hw will you know it.?
 
Back
Top Bottom