Freestyler Cado Kitengo yuko vizuri, ila arekebishe vitu kidogo

Freestyler Cado Kitengo yuko vizuri, ila arekebishe vitu kidogo

Jobless_Billionaire

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2022
Posts
3,106
Reaction score
8,101
Kwemaaaaaaaaa... Sauti ni kubwa japo nina swaumu

Kwa wapenzi wa hip hop, upande wa freestyles nadhani wengi wenu jina la Cado Kitengo, Cado nondo, Mzee wa Midamu au Mzee wa AYEEEEEE... nadhani hili jina sio geni kwa wengi wenu.

Nilianza kumfahamu rasmi nadhani ni 2017 kama sikosei katika kipindi cha CITY RAP BATTLE (CRB) Mi casa Lounge kilichokuwa kinahusisha mashindano ya watu kuchanana na mwisho wa siku judges wanatoa points na mshindi kupatikana. Judges kulikuwa na Songa, Mansu Li, One the Incredible na Wakazi na King Zilla sometimes.

Jina tajwa hapo juu (Cado Kitengo) ni mmoja ya washiriki ambao uwezo wao ulikuwa juu sana, ni good entertainer, anajua kuinvolve crowd, punchlines kali, anaweza kustay kwenye beat, anafikiri haraka sana, mpangilio wa vina, kistick kwenye mada n.k yaani kiufupi ni Emcee mzuri. Nilipenda sana kuhudhuria hiki kipindi hasa pale anapokuwa stage, unaweza kujikuta unacheka mwanzo mwisho jinsi anavyoshusha mistari.

Kuna session pia tofauti tofauti ambazo anafanya nje ya CRB, unakuta watu wanampa chochote walichoshika nae anatembea nacho kwenye beat huku vina vikiwa vimezingatiwa, can you imagine.. Ni uwezo mkubwa.

PIa EATV na Tv shows kadhaa alishakuwepo kuonyesha mautundu na akafanya poa vilevile.

SI mara zote alishinda mapambano, kuna baadhi ndani ya CRB alipoteza dhidi ya Jaco Geezy, Stan Rhymes, Mteganda n.k.

Changamoto ninayoiona kwake, mbali na kuwa na uwezo tajwa, kuna muda anapenda sana kutumia lugha zisizo za staha (matusi). Hiki kipengele hakinifurahishi mara nyingi. Kama atarekebisha hapa naamini kuna credit zitaongezeka kwake, anaweza kutumia ila kwa namna fulani na watu wakajiongeza, we all know about rhymes.

Cha pili ni Mood anazokuwa nazo sometimes.. anaweza kuhudhuria kipindi cha television, akaperform kwa kuonyesha mitindo mingi ila zile hang gestures zake unajikuta unawaza huyu mtu ni mzima kweli? Hii akiweka sawa pia naamini kuna kitu ataongeza..

Mbali na hapo, kuna watu kama Stan Rhymes.. Hiki nacho ni kichwa kingine. Ni namba chafu, ukipata time kama ni mpenzi unaweza kutembelea YouTube ukaandika City Rap Battle au majina husika ukaona kitu walifanya.


Kinachonistaabisha, asilimia kubwa ya freestylers wakitoa nyimbo zinakuwa za kawaida sana, yaani unasikiliza unakutana na ladha tofauti kabisa ndiyo maana hao niliowataja, nyimbo zao nazikubali kwa uchache sana.


Upande wako unawakubali nani? Watajeni ili nikawasearch nienjoy freestyles
 

Attachments

  • images (31).jpeg
    images (31).jpeg
    31.9 KB · Views: 2
  • images (30).jpeg
    images (30).jpeg
    38.5 KB · Views: 1
Upo sahihi sana enzi za city rap battle hawa jamaa ndo niliwakibali
1. Cado
2. Toxic Fuvu
3. Stan Rymes
4. Jaco Geezy
5. Mteganda

Japo kulikua na wengine pia wakali kama Man Side, Black Mc na wengine kibao..

Ila pambano ambalo sitalisahau lilikua kati ya Stan Rymes na Cado kitengo aisee [emoji1787] jamaa alichana huku anakata mauno..
(Stan najua unatokea Iringa, lakini bila shaka utakua unakalia mafinga...[emoji81]) Punchline Moja Kali sana

Pambano lingine ni kati ya
Stan Rymes vs Toxic Fuvu
Cado vs Big Simple ( hili lilikua noma)
Cado vs Zepa (hili liliishia njiani baada ya Zepa kususa)

Ila cado kweli ni Nondo
 
Back
Top Bottom