A
Anonymous
Guest
Nimekuwa nikifika katika uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge kuangalia mechi, lakini nimekuwa nikishangazwa na hali ya fremu zinazozunguka uwanja huo. Karibu zote zimefungwa na hazitumiki, hali ambayo nimekuwa nikiiona kwa takribani mwaka mzima.
Nilijaribu kufuatilia na kutaka kujua ni nani anayesimamia fremu hizo, ambapo nilielezwa kuwa zinamilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, ambayo inadaiwa iliziuza kupitia mfumo wa TAUSI.
Hali hiyo inanifanya kujiuliza, ni kina nani waliochukua fremu hizo na kwa nini kwa kipindi cha mwaka mzima hawajazifungua wala kuanza kuzitumia? Pia, ni hatua gani zimechukuliwa dhidi ya wale ambao hawajazitumia kwa muda wote huo?
Katika eneo la stendi, hali ilikuwa karibu kufanana, ingawa kwa sasa baadhi ya fremu zimeanza kufunguliwa na kutumika. Hata hivyo, swali linabaki; endapo wahusika hawana mpango wa kuzitumia, kwa nini hatua zisichukuliwe ili fursa hizo wapewe watu wengine wenye nia na uwezo wa kuzitumia, kwa lengo la kuchochea maendeleo na shughuli za kiuchumi katika eneo hilo la kimkakati?
Aidha, hali hii inazua maswali kuhusu namna fursa zinavyopatikana kupitia mfumo wa TAUSI. Kuna haja ya kufahamu iwapo mfumo huo unatoa fursa sawa kwa wananchi wote au kama kuna uwezekano baadhi ya watu wenye taarifa au uwezo wa kupata taarifa mapema kutumia fursa hizo kwa kujinufaisha, ikiwemo kuchukua fremu nyingi bila kuwa na mpango wa kuziendeleza au kuzitumia kwa wakati.
Kwa msingi huo, nashauri TAKUKURU Kinondoni ichunguze suala hili ili kubaini ukweli kuhusu umiliki wa fremu hizo, sababu za kutotumika kwa muda mrefu na iwapo taratibu zilizotumika katika utoaji wa fursa hizo zilifuata utaratibu unaostahili.
Pia, Serikali inaweza kutathmini namna mfumo wa TAUSI unavyotumika ili kuhakikisha unakuwa rafiki, wazi na unatoa fursa kwa usawa, pamoja na kuzuia uwezekano wa kutumiwa vibaya na watu wachache kwa lengo la kujilimbikizia mali bila kuzitumia.
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni nayo inapaswa kutoa ufafanuzi kwa umma kuhusu sababu zinazofanya fremu hizo zibaki zimefungwa hadi sasa, hatua ambazo imewachukulia wahusika ambao hawajazitumia, pamoja na mipango yake ya kuhakikisha fremu hizo zinatumika kwa shughuli za kiuchumi na maendeleo ya eneo hilo.