Friendly Match: Simba Sports Club kupapatuana na Big Bullets FC Uwanja wa Taifa, Dar es salaam

Friendly Match: Simba Sports Club kupapatuana na Big Bullets FC Uwanja wa Taifa, Dar es salaam

Jeshi la kocha Patrick Aussems hili
IMG_20181116_160812_761.jpeg
 
Mabingwa wa nchi ya Tanzania Simba Sports Club inatarajia kukwaruzana na Klabu ya Nyasa Big Bullets FC ambao ni vinara wa ligi kuu nchini Malawi Ijumaa ya Novemba 16, 2018 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Simba SC katika mchezo huo wa kirafiki na Nyasa Big Bullets FC, ni katika kuendelea kuwa sawa kwenye kikosi hicho, pia ni maandalizi ya kujiandaa katika michuano ya kimataifa kwa mchezo wa Novemba 27/28 dhidi Mbabane Swallows kutoka Swaziland, katika michuano ya klabu Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.View attachment 931240
Ahsante mkuu kwa kuwakumbusha wadau....Mnyama anaingia mawindoni tena kwa mtego mkali.
 
Hizi sasa sifa jamanini..Yaani hata mechi ya kirafiki lazima timu itoke nje ya nchi [emoji3][emoji3][emoji3]
Bwana Aussems alipendekeza timu ya nje moja na ya ndani moja.Sijajua ya ndani itakuwa ni ipi.Kama MBUTEMBUTE FC wangekubali, tungewanyoosha uzuuuri kabisa.
 
15' mchezo wa kirafiki uwanja wa Taifa

Simba SC 0-0 Nyasa Big Bullets FC
 
Back
Top Bottom