Frolent Ibenge awasainisha Kisinda na Mukoko Yanga SC

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Hongereni watani zangu a.k.a Utopolo.

Sajili zenu zinatushangaza sana ukizingatia hali yenu ya kiuchumi hivi sasa.

Ila tutakutana uwanjani tuwagonge bao 10.

 
Hivi hawanaga sehemu nzuri ya kukaa wakati wanawasainisha?kila saini wanafanya kwenye makorido na nyumba za watu ndo maana mikataba inakuwa feki

Mkuu kwa mpira wetu wa kiafrika hata hakuna sababu ya kuenenda kisasa. Maana hata sisi tulikimbiwa na Senzo mtu ambaye alikuwa na wajibu wa kusimika mizizi wa uweledi klabuni, na ndio maana tukaona ni sawa kukimbiwa na mtu kama yeye hata kama itatugharimu kusajili wachezaji walioshindikana kwa nidhamu pahala pengine.
 
Hivi hawanaga sehemu nzuri ya kukaa wakati wanawasainisha?kila saini wanafanya kwenye makorido na nyumba za watu ndo maana mikataba inakuwa feki

Halafu kibongo bongo ubora wa mchezaji haushuki au kupanda endapo akisajiliwa sebuleni kwa Mo/GSM au kwenye ukuta wa makaratasi ya nembo ya klabu au kwenye uchchoro wa Bar.
 
Senzo Double Agent ni mweledi? Mizizi ipi hiyo? unayosema wewe Simba ile si kakuta kila kitu, kipi kakiasisi yeye?
 
GSM ilikuwa ndio muda wao wa kujitangaza vzr Sasa sjui huwa wanafeli wapi kuweka bango kwa nyuma. Hawamuoni Muhammed anachofanyaga
Angalia quality ya wachezaji. Hizo formalities zitakuja baadaye. Hata Ulaya kuna wachezaji wanasainishwa hotelini lakini kunakuwa na formal presentation baadaye.

Mikia ingieni sokoni tena. Au mnasubirini msimu wa embe Mwamedi auze juice zake?
 
Tuisila na Mukoko wako vizuri, hakika ni usajili mzuri
Wafuatilie stats zao, Tuisila hajafunga wala kutoa assist msimu huu. Inaonekana alikuwa anakaa benchi muda mrefu sana.
 
Katika hili nawaapongeza sana Yanga.

Upande wa pili kuna namna na inawezekana ndo sababu Senzo aliondoka.

Kuna watu kazi yao ni kupiga pesa za Mo.kipindi cha usajili.
 
Sisi bayarn munshen wa Tanzania wakifanya vizuri kama kawaida yetu tunapita nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…