Frolent Ibenge awasainisha Kisinda na Mukoko Yanga SC

Katika hili nawaapongeza sana Yanga... Upande wa pili kuna namna na inawezekana ndo sababu Senzo aliondoka
Kuna watu kazi yao ni kupiga pesa za Mo.kipindi cha usajili
Kwa mtazamo wako Simba haijafanya usajili mzuri? Morrison, Bwalya na Mugalu unawajua vizuri? hao waliokuwapo wanasajiliwa pia. Chama, Miquissone, Manula, Mkude, eeh, haya wee njoo na Waziri Junior wako Oktoba
 
Haka kajamaa kambea na kaongo, tena katuambie Mwamedi kashakusanya shilingi ngapi kwenye mauzo ya jezi.
Mauzo ya jezi ya kazi gani? Kuna mzigo wa maana ukiingia makundi na robo fainali CAF
 
Angalia quality ya wachezaji. Hizo formalities zitakuja baadaye. Hata Ulaya kuna wachezaji wanasainishwa hotelini lakini kunakuwa na formal presentation baadaye.
Mikia ingieni sokoni tena. Au mnasubirini msimu wa embe Mwamedi auze juice zake?

Mna mbwembwe na pesa za kuuza masufuria na mabeseni
 
Reactions: Tui
Mna mbwembwe na pesa za kuuza masufuria na mabeseni
Maana yake si Yanga wala Simba ina hela zake yenyewe. Bado matajiri wameshika hatamu. Nje ya pesa za matajiri, hakuna timu inaingiza pesa kukidhi mahitaji yake ya uendeshaji ikiwwmo mishahara.
 
Acha umbea wako, tulia ligi ianze hapo ndio tutajua kama wana uwezo au hawana.
Sawa ila duniani kote wanasajili based on performance zilizopita, husajili ili uone kama mchezaji atafaa au hafai.
 
Unajua maana ya professionalism?
Halafu kibongo bongo ubora wa mchezaji haushuki au kupanda endapo akisajiliwa sebuleni kwa Mo/GSM au kwenye ukuta wa makaratasi ya nembo ya klabu au kwenye uchchoro wa Bar.
 
Hivi hawanaga sehemu nzuri ya kukaa wakati wanawasainisha?kila saini wanafanya kwenye makorido na nyumba za watu ndo maana mikataba inakuwa feki
Mikataba anasainiwa kwenye goti la mguu kwa kichuchumaa kisha inawekwa kwenye stuli,,,!!!
Pamoja na kumchukua Mazingiza lakini bado Yanga wanafanya mambo kienyeji sana.View attachment 1541025View attachment 1541026
 
Sikudanganyi mabadiliko unayoona yanga ni kwa vile wanaiga kwa simba baada ya kuona aibu ,vitu vingi vya maendeleo yanga ni simba ndo wameanzisha ,wakikejeliwa na wao ndo wanaiga
Mikataba anasainiwa kwenye goti la mguu kwa kichuchumaa kisha inawekwa kwenye stuli,,,!!!
Pamoja na kumchukua Mazingiza lakini bado Yanga wanafanya mambo kienyeji sana.
 
Kwa yanga hii ya GSM hata akija BACCA anakufa nyingi tu
 
Kwa yanga hii ya GSM hata akija BACCA anakufa nyingi tu
Mlisema haya hata walipokuja akina Yikpe na Molinga.

Ukiangalia quality ya players waliopo Simba ambao tumewaona wakicheza kwenye ligi utakubali kuwa Yanga wana kazi ya ziada.

Wachezaji wapya wa Yanga hasa wa kigeni hatuwezi kuwaongelea kwa sababu hatujawaona wakicheza hapa kwetu.
 
Subiri uone kiongozi kwa sasa yanga inanunua wachezaji haiokoti kama zamani naamini na wewe utaona jinsi yanga itakavyo kuwa tishio
 
Vitu gani hivyo?
Sikudanganyi mabadiliko unayoona yanga ni kwa vile wanaiga kwa simba baada ya kuona aibu ,vitu vingi vya maendeleo yanga ni simba ndo wameanzisha ,wakikejeliwa na wao ndo wanaiga
 
Kwa Kisinda yule niliemuona kwenye mechi za CAF watani mmepata mchezaji mzuri jamaa ni skilfull, na kwa ile kasi yake aliyokua nayo, anapiga mbali na mara zote anavamia goli. Labda kama amebadilika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…