From Karimjee Hall: Public Hearing ya Kamati ya Bunge toka kwa wadau wa Dar es Salaam

From Karimjee Hall: Public Hearing ya Kamati ya Bunge toka kwa wadau wa Dar es Salaam

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Salaam,
Niko ndani ya ukumbi wa Karimjee Hall ambapo Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba, inakusanya maoni ya wadau wa Dar es Salaam kuhusu mchakato wa katiba.

Kikao kinaongozwa na Mwenyekiti mwenyewe wa Kamati, Mhe. Pindi Chana akiandamana na wajumbe wa kamati yake, akiwemo Mh. Tundu Lissu.

Hivi sasa anaetoa maoni ni Mwenyekiti wa Chadema, Dr. Wilbroad Slaa atafuatiwa na Jaji Joseph Warioba.

Ukumbi umefurika full juu na chini, watu wamekaa mpaka chini kwenye kapeti.
public hearing hii ilivunjika majira ya saa 7 mchana kufuatia zomea zomea ya msemaji wa CCM Tambwe Hiza.
 
kama unaweza kutupa na picha itakuwa safi mwana jf mwenzetu. mchakato unakwenda vp lakini hapo ukumbini..
 
Dr. Slaa anaubomoa muswada top down, left right, inside out, kwa hoja kuwa kama katiba ndio baba na ndio mama na katiba hiyo ni ya wananchi, rais ni zao la katiba, hivyo ni mtoto wa katiba husika, hivyo mchakato hauwezi kuongozwa na rais, kila kitu rais, ndio mwenye maamuzi ya mwisho, amesisitiza mamlaka yawe kwa wanachi kupitia wawakilishi wao waliowachagua bungeni.
 
kama unaweza kutupa na picha itakuwa safi mwana jf mwenzetu. mchakato unakwenda vp lakini hapo ukumbini..
Bahati mbaya mimi sio mwanahabari, ningekuwa mwanahabari, ningewamwagia na picha. Kwa humu ndani, mimi ni mwananchi tuu.
 
Nakubaliana na dr. moja kwa moja manake kwa style ya mswada ulivyo ni kwamba unaanzia na kumalizikia kwa rais huku uhuru wa kuhoji baadhi ya mambo ukifinywa. tupe picha kama inawezekana.
:help::help::help:
 
Humu ndani ya ukumbi, wana Chadema wanaonekana walijipanga, magwanda kibao, Rwakatare ndani ya nyumba, ila hata CCM hawako nyuma, Tambwe Hiza ndani ya nyumba.

Dr. Slaa anaendelea kuuchana muswada huo, anauliza hii haraka ya nini, ameomba turuhusiwe kukusanya maoni mpaka Mwezi Octoba.

Dr. Slaa kamaliza, sasa ni zamu ya Jaji Warioba atafuatiwa na Prof. Lipumba.
 
Asanteni sana waku leteni habari, maana wamebana hakuna chombo cha habari kinachorusha moja kwa moja.
 
Jaji Warioba, ameanza kwa kusema, hakujipanga kuzungumza bali alikuja ili kusikiliza tuu, maadam amepewa nafasi ya kuzungumza, basi bora azungumze.

Amesema, pamoja na muswada kumruhusu rais kuunda tume, muswada huo, unamlazimisha rais kupokea ushauri.

Ukumbi unapiga makofi ya ule mtindo wa Nkrumah Hall, watu wanaendelea kuleta fujo kwa kupiga makofi, hivyo Jaji Warioba anashindwa kuongea.

Pindi Chana anaomba ukimya, watu wanakaidi na kuendelea kupiga makofi.
 
Jaji Warioba amesema yale yaliyozuiliwa yasizungumziwe ndio mambo ya muhimu kabisa ya katiba. Ametaka wananchi waruhusiwe kujadili kila kitu bila bila kuzuiliwa.
 
Samahani mwenyekiti mjumbe wako nilichelewa kidogo foleni ya fisadi Lowassa pale Namanga; eehhhhee, hebu lete habari!! Nimependa sana utangulizi wako.

JF-Dodoma na nyie hebu tuwekeni online basi.
 
Warioba anasema hata Muungano, waacheni watu waseme, kuna watakaotaka muungano uvunjwe, waachwe waseme, wako watakaotaka muungano wa serikali moja, nao waachwe, wote waachwe ili serikali ijue wananchi wanataka nini.
 
Yes, naona leo Karemjee kunawaka moto..na sijui kama watayarishaji wamejiandaa kupokea maoni ya watu kwa sms au kupokea simu?
 
I salute you PASCO kwani umeamua kutumia muda wako kutujuza ambao hatuko kwenye eneo la tukio.Keep it up.
 
Mara nyingi mzee warioba huwa haogopi kusema ukweli.
Ni kweli huyu jamaa ni very bold, anamchana JK live bila zengwe, amesema, tukiamua kufanya constutuents assembly, then ni over and above level ya rais ku acent, constituent assembly ikishatoa mapendekezo yake, rais anapewa kwa utekelezaji.
 
Back
Top Bottom