Dr. Slaa anaubomoa muswada top down, left right, inside out, kwa hoja kuwa kama katiba ndio baba na ndio mama na katiba hiyo ni ya wananchi, rais ni zao la katiba, hivyo ni mtoto wa katiba husika, hivyo mchakato hauwezi kuongozwa na rais, kila kitu rais, ndio mwenye maamuzi ya mwisho, amesisitiza mamlaka yawe kwa wanachi kupitia wawakilishi wao waliowachagua bungeni.
Nakubaliana kuwa mamlaka juu ya katiba mpya yawe kwa wananchi lakini siafiki kuwa kazi hiyo wananchi wakasimu kwa bunge hili ambalo wabunge wake wengi wanatoka chama cha mafisadi; kufanya hivyo ni sawa na kumuachia nyani akulindie shamba lako la mahindi!! The best way forward is to have a constituent assembly representing different stakeholders in our country ndio wafanye hiyo kazi kwa niaba ya wananchi.