From Mo's Blog: Exclusive Interview With January Makamba

From Mo's Blog: Exclusive Interview With January Makamba

Respect mkuu MTM

Kwa haraka haraka;what was the really motive behind of January's article?Alikuwa anajaribu kutuambia jinsi alivyopata shida utotoni kabla ya baba yake kuwa afisa wa serikali ya TZ?Alikuwa anajaribu kutuonyesha mlolongo wa elimu yake na vyuo alivyosoma au alikuwa anajaribu kutuambia uzoefu wake kwenye kazi za kutatua migogoro ya kimataifa?Kwa kweli sijajua hasa lengo lake alikuwa anataka kutufundisha nini!!

Tuache utani malafyale, kuna mtu huwa anasema "mimi niliishi kwa raha sana utotoni"??? kwa taifa kama tanzania lenye miaka kama arobaini na kitu, majority walianza kuvaa viatu late na sie wa early 70s wazazi wetu walikuwa bado ndio wanajiadjust na kupata redio na photo album, baada ya hapo ndio wakaanza hata kufanya birthday parties...

In short historia ya January ni very generic kwa watanzania wengi... lazma aseme hivyo!!

Ila la msingi hapo ndugu yangu Malafyale ni kwamba, Mo na January wanaleta usanii wa kisiasa, "strategic partnership hiyo" - Mo anajiuza kwa watanzania na Makamba na circle ya JK [marketing tu hiyo!!!] angekuwa anaipenda sana tanzania angehoji wauguzi, walimu, wakulima, wachumi, washauri nasaha, ma-engineer, nk... na Huyo January anapima maji ya siasa yakoje {wrong move January, ni bora abaki kama advisor wa "core" kuliko kwenda kupoteza muda dodoma... atadumaa akili tu pale na kuondoa exposure yake nzuri)

Anyways,namtakia mafanikio mema kwenye gurudumu lake la kujitafutia maisha,lkn namshauri kuwa kama anataka Ubunge wa Lushoto aanze kuwekeza sasa huko na hizi habari za kuuza Lubisi Kyaka au kulala nyumba za kuvuja hazitamsaidia!Namshauri aanzishe mradi wowote au Saccos kuwakopesha wakulima,vijana,akina mama na wanafunzi kwa riba nafuu huko kwenye jimbo analolimezea mate la Lushoto;sisi huku KYELA ni lzm ufanye hiyo kama mtu anataka kugombea udiwani au ubunge!

Hapo ndio January atakuwa amekosea kugombea ubunge, he is in a very good position kuanza kwenda kupiga magoti, kugawa kanga na vibaba vya mchele... halafu bado kijana mwache abaki kule aendeleze diplomatic status, hasa kwa sasa EAF inakaribia kuwa kweli

Karibu Kyela uone tunavyofanya kuwavutia wapiga kura mheshimiwa MTM!

Huwa napita hapo sana tu kwenda itete (ile hydro power safi sana) na matema (wagonjwa waache kuoga ziwani), mambo yenu shwari, ila sasa mngezidisha kilimo wa vijiji kwa kutumia ultramodern financing mechanism halafu mapato mnaweka percentage (kwa uongozi wa vijiji, wakulima - yaani nyie wenye nguvu, halafu albaki mnagawa divident kwa wote hata kama ni elfu hamsini kwa kila mtu, hiyo ni kampeni tosha na haitahitaji takrima kwani watu watakula walichopanda.... matreka 100 tu yanatosha hapo na hayana kodi, zuka hapo benki mazee

Nitakusapoti kwa maombi mkuu
 
sasa January Swali moja. Wewe umesoma conflict resolution na Diplomasia...Mbona unaitwa mshauri wa Uchumi wa raisi? Unajua uchumi gani kaka au ndo Rich-monduli? Hamna kitu hapa umebebwa na huna lolote (nukta). Sijaona jambo lolote la maana uliloongea kweli mtoto wa nyoka ni nyoka!

Wewe kweli ni mchapakazi... Huo ndio mfumo tuliojiwekea kama watanzania, tunapachika tu!!! hata fenicha zetu homu unaweza kukuta friji kwenye chumba cha watoto, bila kujali athari, mingurumo na disturbance za usingizi wao, ipo kwenye "genes" zetu mkuu

I hope hili swali litapatiwa jibu la ukweli toka kwa Jannuaru, maana huwa anapeep humu!!!!
 
Have a baby by me and be a millionare.......oops no this is what i meant to say right...inamaana mimi nikatokea kumu interview lets say Invisible na ni mshikaji wangu wa karibu sana (huu ni mfano) kuna tatizo gani?....Nimeona upeo wake na nikaona why not na watu wengine wasimjue...msiwe na roho za kwa nini vijana wenzangu wa kitanzania....


January yoo listen m2wangu...miye nakufagiliya kinoma yaani interview iko very alright...na hata kama ukiwa unahitaji ina wewe akina Carl Rowe tupo hapa yaani mimi nakufagiliya all the way....wee nicheki mimi on the video phone......(i meant pivate hapa wachawi wengi)..or i will Gps YOU!

sasa binti mbona unaleta za "when i was, just arrived, leaving soon, aaaiight, yoo, GPS, check-check yoo, wasape nyingi mamaaa??
 
Kilikuwa ni Chuo cha Wakatoliki in a real sense (ingawa dini nyingine walikuwa wanasoma na mtu hukulazimishwa kusoma theology na kwenda kanisani), kwa maana ya kwamba kulikuwa na
Seminary pale pale lakini kubwa zaidi kulikuwa na Monastery pamoja na monks wa Benedictine na majoho yao meusi. Zaidi ya nusu ya wahadhiri wangu walikuwa monks. Kwahiyo haya mazingira yalikuwa kidogo na “utakatifu”.



Hukushawishika ku-convert to Christianity kweli?
 
Mwangalie Januari kama Januari. Hii ya kulinganisha na baba zao kwa kuwa tunawajua, sie ambao baba zetu hawajulikani tungekubali kulinganishwa nao?
'judge the content.......'

Zitto, etal
This is all part of that political game. It is a game involving two opportunistic young politicians. Januari pops himself up into limelight (this interview), sounding as humble as he can (which any actor can do). Am sure u all know who is backing the Makamba's economically and politically. Without even a blink of an eye Zitto shows up anamsifia mno Januari (sina uhakika sana ni baada ya Zitto kufanya analysis yoyote au la). Now the clincher.........Already there's a suscipicion thru this forum (mama Zitto) kuwa kuna (wa)mtu wa nje ya Chadema (w)amekuwa (w)akiwatumia watu ndani ya Chadema kumgonganisha Zitto na vigogo wenziwe, jambo ambalo Zitto amempinga mama yake. So logically, these two youngmen appear have a common "friend" anaye-back political ambitions zao. Just speculating....
 
Zitto, etal
This is all part of that political game. It is a game involving two opportunistic young politicians. Januari pops himself up into limelight (this interview), sounding as humble as he can (which any actor can do). Am sure u all know who is backing the Makamba's economically and politically. Without even a blink of an eye Zitto shows up anamsifia mno Januari (sina uhakika sana ni baada ya Zitto kufanya analysis yoyote au la).

Mkuu nilipost hapa kwamba hawa ni opportunists fulani wanajipia mapande kivyao, nitafurahi nikisikia Mo anahoji watanzania halisi kama wakulima, walimu, wauguzi, machinga, wanamichezo, wanamuziki nk.

Lakini yote kheri kwani tumejua January alisoma wapi!!
 
huuni upumbavu tu who is january to me by the way......si bora nipate mahojiano ya mzee mwanankijiji walau ana endesha vuguvugu la mabadiriko!!

Kila siku makamba makamba......what do we get from them?? Mbona hamwendi kuwahoji wabeba magunia ya mkaa kule mvomero ambao wananyanyaswa na serikali ati wasichome mkaa.....watakula nini??

Makamba amekuwa rc dar miaka lukuki na jiji likaendelea kunuka uchafu....alafu mnaniletea interview ya january........tena mkome, haya mambo pelekeni kwenye celebrities.


lol!
 
Mtoto wa nyoka ni nyoka.. Asanteni sana. Na kuniambia watoto wa wakubwa wa Tanzania wanasoma kwa shida kama akina Kayumba siamini.
 
Ukianza kusoma tu, kitu cha kwanza unachoona ni kwamba interview haina credibility, ni mtu na crony wake wameamua kufanya mchezo wa kuigiza.Hicho ndicho kitu cha kwanza kabisa unachoona, kabla ya kingine chochote.


They are testing the water! 2010 is arround the corner. Need I say more?
 
Kama haya ni kweli basi ndio maana Makamba anashindwa kukiongoza chama ,kwani hata maisha yake ameshindwa kuyaongoza atawezaje kuongoza chama kizima?
Kama amekuwa mkuu wa Mkoa, amefanya kazi jeshini akashindwa hata kujenga nyumba atawezaje kujenga CCM?

Mshahara wake alikuwa anafanyia kazi gani?
Nini kilikuwa kitu cha msingi kwake?
Ina maana nyumba kwake sio priority?

Hilo nalo jambo...uongozi mzuri huanzia nyumbani.
 
Form Five na Six nikawa Forest Hill Secondary School, Morogoro, ambapo siku ya graduation nilitunikiwa cheti cha Overall Best Student.

hahahahahh yani unamaanisha ulikua mkali kati ya vilaza, hyo shule wanaosomaga hapo kwa mr. patel huwa ni wasanii tupu, ungeniambia ulikua best student ilboru,kibaha au mzumbe niliposoma mimi ningekupa kauzito flani lakini forest.....? aggrrrrr.......
 
Phew! leo nimemaliza kuisoma hii interview

I dont see anything wrong with it

UNLESS KUNA LINGINE MNALO zaidi ya Sir name yake
 
Back
Top Bottom