Kiganyi
JF-Expert Member
- Apr 30, 2012
- 1,242
- 765
Mtoto wa mwanasiasa mkongwe wa nchini John Malechela, William ameamua kuonesha upande wake wa pili kama muigizaji wa filamu.
William Malechela ambaye pia ni mwanasiasa, ameshiriki kuigiza kwenye filamu mpya ya Sintah, iitwayo The Return of JLO.
Kwa mujibu wa Sintah, Willam ameonesha uwezo mkubwa kwenye uigizaji wa filamu.
Mwezi April mwaka huu, William aligombea ubunge wa Afrika Mashariki lakini hakufanikiwa kuupata.
Jana kwenye uchaguzi wa Ubunge wa EAC nimeshindwa fairly na sina malalamiko, ninawapa hongera washindi wote walioshinda leo na hasa my best friends Shyrose, Dulla, na Makongoro, Mungu awaongezee na wakatumikie vyema taifa letu!
As for me sasa ni wakati wa kukaa chini na kutafakari nilipokosea na kuanza kujipanga upya, aliandika Willam kwenye mtandao wa Jamii Forums.
****
Mkuu Le Mutuz hii nimeiona katika Blog moja ya udaku! Mkuu sasa wewe una play character gani katika filamu hii?? Je ndio tukusahau katika Siasa au??
Hongera Mkuu!!
