From series msimu wa 3 umetoka

Sio kwa ubaya, ila hii series ya kiwaki sana😥

Kila nikijitahidi naona chenga, hivi hatuwezi kurudi kwenye zama za series zilizoenda shule kama lost, breaking bad, GOT, vampire diaries, prison break etc.

Kama kuna series yoyote kali kwa sasa, kindly recommend hizi zingine tunaangalia sababu ndio zilizopo ila kiuhalisia za kawaida sana
 
Aiseee umepita mule mule hongera sana,
Tabitha ni Miranda na Jade ni Christopher, walikua mke na mume na wana mtoto mmoja katika wale watoto wa kwenye cave,

Sijapenda kabisa Jimmy kuuliwa japo alikua ananikera wakati mwingine lakini alijitahidi sana kuishape familia yake, namuhurumia Ethan, nina wasi wasi asije aka end up like Victor
 
Nenda thread ya Series, hii ni sehemu yetu sisi tunaoangalia series yetu ya kiwaki
 
Yaani mngeniona nilivyoruka ruka baada ya kumuona Smiley aiseee jamaa anapendwa yule na mashabiki wengi tulishinikiza arudi, finally wametusikiliza, 😂😂😆
Kuna kile kidem ni ki monster kinachovaa kama nesi sijui mpishi ep 9 kilimfuata Boyd kikagonga dirishani na kumuuliza Boyd "everything okay in there" Boyd alimaind
 
Jibu moja ambalo nimepata, nikwamba hilo eneo lipo mda mrefu sana, na hiyo hali ni ya kujirudia, wazazi wanatoa sadaka watoto zao ili wao wapate kuishi milele, episode ya 10 imezalisha maswali mengi sana

1. Je ni mtoto wake yupi ambaye anamzungumzia Tabitha kwamba ni miongoni mwa watoto wanaohitajika kuokolewa

2. Yule mzee kabla ya kumuua Jim anamwambia "ni bora mke wako asingechimba lile shimo"

3. Mnakumbuka kuna vision ya Boyd kunasa kwenye shimo, kama kisima na kila akirushiwa kamba inakuwa kama imekatika... Hili ni tukio litakalokuja tokea mbeleni, linaanza pale alipoingia kwenye handaki,

4. Je kutakuwa na vita kati ya Monsters wa mchana na usiku,

5. Ule mziki ni key ya kuwafingua monster wale wa mchana, jamaa alicrack zile code in a reverse, je kuwafunga ni hivyo hivyo...

6. Ni nini hatma ya wale watatu (Randol, Nesi na Mtoto wa Tabitha)

7. Chini ya ardhi eneo lile kuna siri kubwa sana, je chanzo ni nn

8. Swali kubwa la msingi inakuwaje hawa monsters wanawafahamu watu wanaokuja pale ( je wote wapo connected na matukio ya miaka iliyopita pale)

9. Julie anaenda kurekebisha kurasa kwenye kitabu cha historia ya hilo eneo, atafanikiwa kubadilisha hadithi?





"Knowledge comes with cost"
 
Hayo yote tutayajua season 4, sijui itakuwa mwakani au watapiga miaka miwili wailete 2026
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…