From the book 'I am the State' (Mimi ni Dola)

Huo ni upambavu wa kiwango cha SGR na kuna mtu kawalipa.Waongee lingine, kwenye suala la miradi hapo wamechemka!
Reli ya SGR inaenda Chato?Mradi wa Umeme Rufiji upo Chato?Bandari kavu ya Kwala ipo Chato?Mradi Ujenzi wa mji Mkuu wa serikali upo Chato?Ujenzi wa vituo vya Afya zaidi ya 300 vipo Chato?Kijazi Flyover ipo Chato?Mfugale Flyover ipo Chato?Barabara ya njia nne Kimara mpaka Kibaha ipo Chato?
Kwa uchache,Waandishi wameongozwa na chuki zaidi ya uhalisia.
JK mwenyewe alipeleka umeme Kijiji cha Hoyoyo, Mkuranga ambapo hakuna mradi wowote bali Umeme alipata Mkwewe Baba yake na Salma na shambani kwa mkewe!
Ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo ambao alizindua mwaka 2014!
Inshort Kibanda na Ngurumo kama wamo humu jukwaani wajue wamejidharirisha akiwemo na Baba Askofu!.Ila Ngurumo nadhani stress za kukimbia nchi zinamsumbua!
 
Aachwe apumzike! Kama serikali ya SSH itaendelea kuruhusu udhalilishaji huu dhidi ya kiongozi mkuu wa nchi mzalendo aliyetangulia mbele za haki basi wajue wanawakwaza watu wengi sana.
Wewe kweli ni mzalendo uchwara! Acha watanzania wazalendo wa kweli waendelee kuweka wazi madudu ya yule kiongozi mwovu. Kama wewe unajua mazuri yake andika kitabu pia!
 
System ikianza kuwashughulikia mnaanza kulialia!!
 

Tujulisheni hicho kitabu kinapatikana wapi hapa Dar, wengine tuko tayari kukinunua kwa gharama yoyote.
 
Aachwe apumzike! Kama serikali ya SSH itaendelea kuruhusu udhalilishaji huu dhidi ya kiongozi mkuu wa nchi mzalendo aliyetangulia mbele za haki basi wajue wanawakwaza watu wengi sana.

Usinunue ww hicho kitabu, na au andika kitakachokuwa na ukweli ili kuondoa huo udhalilishaji utakao kuwa kwenye hicho kitabu.
 
Unachanganya mambo sana daah!..
 


Waandishi nguli wa habari nchini Tanzania wamezindua kitabu 'I am the State' (Mimi ni Dola) chenye kuonyesha maendeleo ya miradi ya uwekezaji yaliyofanyika wilayani Chato mkoani Geita na ukiukwaji wa sheria uliofanyika ndani ya utawala wa hayati Rais Dk John Magufuli wakati wa utekelezaji wa miradi hiyo.

Akizindua kitabu hicho Askofu wa Jimbo la Karagwe mkoani Kagera, Dk Benson Bagonza amesema uandishi wa kitabu hicho uwe chachu kwa viongozi wastaafu na walio madarakani kuandikiwa vitabu kulingana na mazuri na mabaya yao.

Amesema kitabu cha I am the State kinaonyesha namna fedha za umma zilivyotumika nje ya bajeti ya bajeti ya serikali.

"Mambo yaliyotajwa katika kitabu hiki yalitendeka nchi ikiwa gizani na watu walinyamazishwa na haya yaliyoandikwa ni sehemu ndogo ya yaliyotendeka nchi ikiwa gizani"amesema.
 
Hawa jamaa wameliwahi jopo la wasomi ambao wanafahamika nchini ambapo hivi karibuni watatoa kitabu cha maisha na utumishi wa JPM katika nchi ya mafisadi papa hapa Tanzania

Kunatarajiwa kuzinduliwa kitabu kinachoelezea uajabu wa serikali ya Tano chini ya nchi iliyokuwa ikiitwa nchi masikini kumbe ni janja za wapigaji na mafisadi ya ccm

Ndani yake ipo miradi yote iliyobuniwa na kuanzishwa na serikali yake

Ndani yake wapo mafisadi waliowahi kusoteshwa kwenye serikali yake

Wapo pia wapanga mipango wa kuidhofisha serikali yake

Wapo pia ambao walilikuwa wakipanga mipango ya hatari zaidi dhidi yak
 
Non sense!
Kosa la JPM ni kuwekeza nchini kwake? Kwahiyo na yeye angeenda kujenga makasri huko ulaya?

Na kwa ujinga wa watanzania watazidi kumchukia ilihali wapo waliowekeza nje. Ni vile tu wao hatuwezi kuwa na ushahidi wa wazi kama ilivyo kwa hayati.


Kwa mfano mwizi anayeiba anajenga shule, anasaidia jamii hawzi kuwa sawa na mwizi anayeend akuhonga bar. ( Imenikumbusha korean movie-iljimae)πŸ˜€πŸ‘
 
Amesema kitabu cha I am the State kinaonyesha namna fedha za umma zilivyotumika nje ya bajeti ya bajeti ya serikali.
Huu muhtasari uliotoa ndio umesababisha nijibu kwa namna hiyo. Kitabu tutakisoma tu.
Relax relax relax. Kasome kitabu uelewe ujibu hoja zake. acha kupayuka unatupigia kelele
 
Yeye na hao wanaojenga huko nje hawana tofauti. Huwezi ukachukua kodi za wananchi eti ukajenge kwenu afu ulete implication kuwa wewe ni bora kuliko hao wezi wanaojenga nje. Wote ni wezi. Unataka kwenda kufanya massive investments kwenu, nenda kachukue hela za babako ufanye hivyo maninax sio kodi za wananchi
 
Waandishi wenyewe hao wanajulikana sio waadilifu ni watu wa madili. Wamehongwa kwenda kumchafua marehemu ili wapate ulaji. Majizi yanajuana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…