Algeria vinara wa Kundi F katika kufuzu kwajili ya AFCON watawaalika Tanzania (Taifa Stars) katika mchezo utakaofanyika katika dimba la Annaba huko Algeria.
Taifa Stars yenye alama 7 inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili iweze kufuzu huku Algeria ikikamilisha ratiba ikiwa na alama zake 15.
Pia Taifa Stars itakuwa inaiombea mabaya Uganda (The Cranes) katika mchezo wake dhidi ya Niger. Ikumbukwe Uganda ina point 4 ikishinda kwa magoli mengi itaweka rehani nafasi ya Taifa Stars.
Mechi zote ni saa 4:00 usiku
Kila la heri Taifa Stars🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿🇹🇿