FT: ASEC Mimosas 3-0 Simba SC | CAF Confederation Cup | Stade de L' amitie General

FT: ASEC Mimosas 3-0 Simba SC | CAF Confederation Cup | Stade de L' amitie General

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Klabu ya Simba leo Jumapili March 20, 2022 inashuka kwenye Dimba la Stade de L'amitie General Nchini Benin kukiwasha na ASEC Mimosas kutoka Ivory Coast kwenye mchezo wa marudiano hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAFCC.

Huenda mchezo ukawa mkali na wa kusisimua kwa vile kila timu kutaka kushinda ili kuweka mazingira safi ya kufuzu hatua ya robo fainali, ambapo katika mchezo wa awali uliofanyika Jijini Dar es salaam, Simba SC waliibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Kocha Pablo Franco amesema ASEC Mimosas ni timu nzuri lakini wapo tayari kuvunja mwiko kwenye Dimba la Stade de L'amitie General, ambalo wanalitumia kama Uwanja wa Nyumbani kikanuni.

"ASEC Mimosas ni timu nzuri na wanaweza kufanya chochote, lakini tumekuja kupambana kubadili historia yao ya kutofungwa nyumbani, tunataka kuwa wa kwanza", alisema Pablo.

Simba ndo kinara kwenye kundi D' akiwa na alama 7 huku ASEC akiwa na alama 6, na RS Berkane alama 6 huku Gendarmerie wakiwa na alama 4.

Nani kuibuka na ushindi kwenye mchezo huu wa leo CAFCC?.Usikose Ukaambiwa..Kuanzia saa 1:00 Usiku.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana


FB_IMG_1647781915951.jpg


============================

Updates;

Kikosi cha Simba SC kimefika kwenye Dimba la Stade de L'amitie General tayari kuwakabili ASEC Mimosas.

Vikosi vyote vinaingia uwanjani tayari kwa ukaguzi pamoja na kupiga picha za kumbukumbu.

Wakati wowote mpira utaanza Uwanja wa Stade de L'amitie General

00' Naaam mpira umeanza ASEC Mimosas Vs Simba SC ni michuano ya CAFCC.

05' ASEC Mimosas wanacheza eneo lao kujaribu kuwavuta Simba SC ambao nao wanausoma mchezo.

10' mpira upo kati na kati huku Simba wakipata Kona mbili ambazo hazikuzaa matunda, ASEC ni hatari zaidi kwa upande huu ambao yupo Hussein.

15' baada ya gonga safi kwa Simba, shuti kali la Mzamir linapaa nje ya lango.

16' Goooooooooooooaaal gooal

Kramo Aubin anaipatia ASEC Mimosas bao la kuongoza akipokea Krosi kutoka winga ya kulia.. ASEC Mimosas 1-0 Simba SC.

20' Shambulizi la ASEC lakini golikipa Manula anadaka shuti lile bila presha, na kuanzisha mashambulizi.

25' ASEC wanajenga mashambulizi lango la Simba... Goooooooooooooaaal gooal

Ki Aziz anahesabu bao la pili upande wa ASEC Mimosas kwa shuti kali na kumuacha Manula akiruka bila mafaniko... ASEC Mimosas 2-0 Simba SC.

Kagere anapiga kombora kali, lakini golikipa wa ASEC Mimosas anaruka na kupangua na kuwa Kona ambayo haikuzaa matunda.

30' Umiliki wa mpira ni wa Simba SC wakijaribu kuongeza pressure kwa ASEC Mimosas, lakini ASEC wanajilinda na kucheza kwa malengo.

35' Wanapata ASEC Mimosas penalty baada ya Aishi Manula kumfanyia madhambi mchezaji wa ASEC Kramo Aubin.. Tuone itakuwaje..!

Anakwenda kupiga mkwaju ni Konate Karim.. Anakwendaaa Ooooh anakosaaaaaa penalty..Aishi Manula anacheza mpira na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao.

40' Simba SC wapo nyuma kwa mabao mawili kwa bila, huku ASEC wakicheza kwa kujiamini na kutumia nafasi.

45+1' Kuelekea kuwa mapumziko

Naaam mpira ni mapumziko ambapo ASEC Mimosas wanatoka wakiwa mbele ya mabao mawili kwa bila..!

HT: ASEC Mimosas 2-0 Simba SC

Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Stade de L'amitie General huku Simba wakifanya mabadikio.

Ametoka Mzamir, Kibu, Bwalya na nafasi zao zimechukuliwa na Lwanga, Banda, Morrison.

46' Shambulizi kuelekea ASEC, lakini golikipa wa ASEC anadaka shuti lile bila presha, ilikuwa nafasi nzuri kwa Simba SC.

Taddeo Lwanga anaonyeshwa KADI ya Njano kwa kumchezea madhambi mchezaji ASEC.

55' Simba wanajaribu kuwavuta ASEC, lakini bado matumaini ya kupata bao, huku Kagere akionyeshwa KADI ya Njano kwa kumchezea madhambi mchezaji ASEC

57' ASEC wapo lango la Simba SC, inapigwa kulee Goooooooooooooaaal gooal

ASEC Mimosas wanaandika bao la tatu kupitia kwa Konate Karim kwa kichwa safi Manula hakuambilia kitu.. ASEC 3-0 Simba SC.

ASEC wapo vizuri sana kwa kutumia nafasi wanazopata kuliko Simba SC.

Jonas Mkude anatoka na nafasi yake anaingia Chris Mugalu upande wa Simba SC

66' Morrison anatandika shuti la mbali, lakini mpira unatoka nje, namna gani Simba wanashindwa kupata walau bao.

70' ASEC Mimosas 3-0 Simba SC Shughuli bado ni ngumu, haya kwake Inonga anapiga mbele kumtafuta Morrison lakini mpira unatolewa na kuwa Kona.

74' Aka anaingia upande wa ASEC Mimosas badala ya Zougrana Mohamed

76' Inonga anatoka na nafasi ya inachukua na Wawa upande wa Simba SC, ASEC wanapata Free Kick kuelekea Simba SC eneo la hatari, wacha tuone.

Golikipa wa ASEC Cisse anafoka anawambia mabeki wake nini mnafanya, baada ya kosa kosa kwenye lango lake, huku Wawa akionyeshwa KADI ya Njano.

80' Almanusura ASEC wapate bao, ilikuwa nafasi nzuri kwa ASEC na hatari kwa Simba SC..Namna gani Simba hapa.


85' Wawa anapiga mbele kwake Mugalu, kwake Kagereeee shutii na kumbabatiza mchezaji wa ASEC na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao..!

Morrison anamjaribu golikipa wa ASEC Mimosas Cisse Karim kwa kupiga kichwa lakini mpira unatoka nje...huku ASEC wakifanya mabadikio Pokou anaingia badala ya Ki Aziz.

88' Onyango anafanya madhambi eneo la 18 ni penalty kuendelea Simba SC, anakwenda kupiga mkwaju wa penalty anapigaaaaa... Manula anacheza kwa mara nyingine tena.

Anakuwa shujaa kwa kuokoa mikwaju miwili ya Penalty kutoka kwa ASEC Mimosas.

90+4' Kuelekea kumalizika kwa mchezo wa CAF Confederation Cup.

Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo ASEC Mimosas wanaibuka na ushindi wa mabao matatu kwa bila dhidi ya Simba SC.

FT: ASEC Mimosas 3-0 Simba SC

...... Ghazwat......
 
Kinachoendelea...!

Sasa chache kabla ya mchezo Simba SC wamepata mashabiki 100 ambao wataishangilia mchezo wa leo, ambapo CAF wameruhusu mashabiki 3500 Uwanjani kwenye mchezo huu wa leo.

Na kwa kudhamini mchango na utayari wao kuwashangilia, Simba SC wamewaandalia tisheti zenye ujumbe ALLES LES SIMBA SC... maana yake LET'S GO SIMBA SC.

Ahmed Ally Meneja Habari na Mawasiliano Simba SC.
 
Kikosi walichokitaja ASEC Mimosas dhidi ya Simba SC.. Kombe la Shirikisho Barani Afrika CAFCC.
%2523Actionnaires%252C_voici_les_%2523Mimos_convoqu%25C3%25A9s_par_Julien_Chevalier._%2523CIVs...jpg
 
Back
Top Bottom