FT: CAF Champions League | Raja Casablanca 3-1 Simba S.C | Stade Muhammed V | 01.04.2023

Yes, na hiyo ipo hadi kwenye maisha ya kawaida.
Ndiyo maana miye kwenye mashindano ya Afrika,Huwa sishabiikii timu za chini ya Jangwa la Sahara

Miye siku zote hushangilia za Waarabu
Nakumbuka Kuna gemu moja ya Afcon kama sikosei ilikuwa fainali kati ya Misri na Kameruni,nakumbuka ni kiipindi nipo A-Level Lindi Sekondari kati ya 206-2008

Nakumbuka shule nzima pale bwaloni tuliokuwa tunashbiikia timu za Waarabu tuliokuwa Mimi na shombeshombe mmoja hivi wa kiaarbu

Masela Kwa asira walipanga kumwagia magodoro yetu maji iwapo Kameruni wangeshinda Ile fainali


Aaahahahaah

Nakumbuka dakika za lala salama Kuna boya mmoja anaitwa Robert Song alichomesha yeye akiwa pekee yake na kipa wake ndipo mchezaji wa Misri akaenda akafunga goli rahisi kama like la Gerrard alilompa Drogba Ili Man Utd tusichukue kombe dah
 
Kila siku nasema hapa, Onyango ana ubeki wa kizamani sana yaani modern football inamkataa kabisa.

Huyu ni wa kimtafutia bek mwingine wa kati kisha anakula benchi bila kumuonea aibu.

Mjunga sana huyu.
Basi inatosha, tuwashukuru wachezaji wetu, hatua hii wametufikisha hawa hawa
 
Naikumbuka sana hiyo match. Rigobert Song alishusha CV yake sana.
 
Basi inatosha, tuwashukuru wachezaji wetu, hatua hii wametufikisha hawa hawa
Ni kweli ndugu ila kuna makosa mengine yanatokea kwa uzembe sana. Hebu angalia penalt aliyosabisha Onyango. Makosa ni yale yale yani.
 
Kila siku nasema hapa, Onyango ana ubeki wa kizamani sana yaani modern football inamkataa kabisa.

Huyu ni wa kimtafutia bek mwingine wa kati kisha anakula benchi bila kumuonea aibu.

Mjunga sana huyu.
Mechi ya yatu hii anasababisha penati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…