'Nafasi ya tatu wanang'ang'ania' kwani hao Uto ndio walioandaa hizo rank?
USMA kusumbuana na Al Ahly ni credit kwa Yanga kwasababu inaonesha kweli fainali alicheza na timu bora na hata kumfunga USMA nyumbani kwake ni kipimo bora kwa Yanga kwamba kamfunga timu iliyobora na sasa ndiye kidume cha mashindano yote ya CAF huyo.
Tuje sasa kwenye ishu ya rank maana imewatoa watu mapovu leo lakini kipindi Simba anawekwa kwenye ubora kumzidi Sevilla hamkuwa mnahoji.
Ipo hivi,. IFFHS inajihususha na namba pekee na ndio maana wanaitwa international federation of football history and statistics, wao wana deal na overall performance ya timu katika michuano yote anayoshiriki ( michezo ya kitaifa na kimataifa) kisha wana record kila kitu kwanzia magoli ya kufunga, idadi ya magoli ya kufungwa, idadi za clean sheet, idadi ya michezo uliyoshinda, n.k wanachukua kila data inayohusiana na performance kisha vinawekwa katika asilimia ndipo unaona mwisho wa siku wanaweka rank na point. USMA kafanya vizuri kwa kuchukua kombe la shirikisho lakini je kwenye hilo kombe la shirikisho anatakwimu nzuri kuizidi Yanga? Na vipi katika mashindano ya ndani je ana takwimu bora kumzidi Yanga?