Wawakilishi wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho barani Africa, Simba SC leo wataingia uwanjani kupambana na CS Constantine kutokea Algeria kwenye mechi ya mwisho ya makundi
Mechi hiyo ni muhimu kwa timu zote mbili kwani ndio itakayoamua nani ataongoza kundi lao. CS Constantine wapo nafasi ya kwanza na Simba wapo nafasi ya pili
Kabumbu hilo ambalo litapigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam litaanza saa kumi jioni
Ungana nami katika kufuatilia mpambano huo
Ubaya Ubwela
Full Time: Timu ya Simba imefanikiwa kushinda kwa magoli 2-0 dhidi ya CS Constantine
Magoli ya Simba yalifungwa na Kibu Denis na Ateba