FT: Colombia 1-0 D.R. Congo | World Cup 2026| Estadio Akron | 24 Juni, 2026 | 11:00 Alfajiri

FT: Colombia 1-0 D.R. Congo | World Cup 2026| Estadio Akron | 24 Juni, 2026 | 11:00 Alfajiri

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Kama washindi pekee wa Kundi K katika michezo ya kwanza, Colombia watakuwa wanatafuta nafasi ya kujihakikishia ushiriki wao katika hatua ya 32 bora watakapochuana na DR Congo kwenye Uwanja wa Guadalajara nchini Mexico.

Fomu ya Timu na Habari Zilizopo​

  • Colombia: Walifungua ukurasa wao wa Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2026 kwa mtindo wa kuvutia baada ya kuichapa Uzbekistan mabao 3-1. Ushindi katika mchezo wa sasa utawawezesha La Tri kutinga hatua ya mtoano kwa mara ya tatu mfululizo katika michuano hii ya Kombe la Dunia.
  • DR Congo: Walijikuta wakiwa nyuma mapema dhidi ya Portugal katika mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Dunia, lakini walionyesha ari na kusawazisha goli hilo kabla ya mapumziko na kufanikiwa kulazimisha sare ya 1-1 hadi mwisho wa mchezo.
 
Tayari Congo imepoteza hiyo mechi kwa kufungwa bao 1-0 na Colombia na hivyo kujiweka katika mazingira magumu ya kufuzu katika hatua ya mtoano.

Inabidi sasa piga ua Congo iifunge Uzbekistan katika mechi yao ya mwisho ili ione kama inaweza kufuzu kama best loser.

Katika mchezo huo mkali Colombia ilionekana kuishambulia zaidi Congo kwa sehemu kubwa ya mchezo na kama isingekuwa umahiri wa mlinda mlango wao Lionel Mpasi aliyeokoa mikwaju minane ya hatari basi Congo ingeweza kuchapwa mabao mengi katika mchezo huo.
 
Back
Top Bottom