Tayari Congo imepoteza hiyo mechi kwa kufungwa bao 1-0 na Colombia na hivyo kujiweka katika mazingira magumu ya kufuzu katika hatua ya mtoano.
Inabidi sasa piga ua Congo iifunge Uzbekistan katika mechi yao ya mwisho ili ione kama inaweza kufuzu kama best loser.
Katika mchezo huo mkali Colombia ilionekana kuishambulia zaidi Congo kwa sehemu kubwa ya mchezo na kama isingekuwa umahiri wa mlinda mlango wao Lionel Mpasi aliyeokoa mikwaju minane ya hatari basi Congo ingeweza kuchapwa mabao mengi katika mchezo huo.