FT: Ecuador 2-1 Germany | Worl Cup 2026 | MetLife Stadium | 25 Juni, 2026 | 5:00 Usiku

FT: Ecuador 2-1 Germany | Worl Cup 2026 | MetLife Stadium | 25 Juni, 2026 | 5:00 Usiku

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Ecuador na Ujerumani wanashuka kwenye dimba la New York New Jersey Stadium, huku Waamerika Kusini hao (Ecuador) wakipambana kufa na pona kupata nafasi ya kutinga hatua ya mtoano dhidi ya Wazungu (Ujerumani) ambao tayari wameshafuzu.

Ecuador waliingia kwenye mashindano haya ya Kombe la Dunia la FIFA wakiwa na rekodi ya kucheza mechi 19 mfululizo bila kupoteza (Ushindi 8, Sare 11). Hata hivyo, wamejikatisha tamaa wenyewe kwenye michuano ya mwaka huu hadi sasa baada ya kufungwa 1-0 na Ivory Coast na kisha kutoka sare ya 0-0 na Curaçao.

Kwa upande wao, Ujerumani walianza kwa kuiponda Curaçao mabao 7-1. Katika mechi iliyofuata dhidi ya Ivory Coast, walijikuta nyuma kwa goli 1-0 hadi mapumziko, kabla ya mabadiliko na kiwango bora kwenye kipindi ya pili kuwasaidia kushinda mabao 2-1, huku goli la ushindi likipatikana katika dakika ya 94 ya mchezo.

Historia ya Timu Hizi (Uso kwa Uso)​

Ujerumani imeshinda mechi zote mbili zilizopita walizokutana: walishinda 3-0 katika hatua ya makundi ya Kombe la Dunia mwaka 2006, na kisha kushinda mabao 4-2 katika mechi ya kirafiki mwezi Mei 2013.
 
ECUADOR 2 - 1 GERMANY

Ecuador pamoja na Germany wote wanapata nafasi ya kusonga mbele katika hatua ya mtoano ya kombe hili la dunia 2026 itakayohusisha nchi 32 zilizoongoza ndani ya makundi yao.
 
Back
Top Bottom