Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 23,620
- 52,790
Majira ya Saa 10:00 Alasiri kwa masaa ya Afrika Mashariki, Ihefu Fc itawakaribisha Simba Sc katika dimba lao la Highland Estates katika muendelezo wa Ligi Kuu ya NBC.
Habari kubwa leo, nani wa kumzuia Jean Baleke ambaye amekuwa hazuiliki sasa, kwa taarifa yako Baleke kwasasa anafunga kila mechi, alifunga mecho iliyopita hat trick na atafunga leo na mechi ijayo atafunga kama ilivyoada.
Ihefu iliyopo nafasi ya 8 itajaribu kulipa kisasi baada ya kufanyiwa mauaji ya Sharubela juzi dhidi ya Mnyama mkubwa mwituni, Simba SC, Ihefu aliloa mabao 4-1.
Simba iliyopo nafasi ya pili, itajaribu kupunguza alama dhidi ya Yanga wanaoongoza ligi kwa tofauti ya alama 8 huku ikisalia michezo sita kabla ya ligi kutamatika.
Ewe mwanasimba uliyepo Dodoma, Nakuru, Bukoba, Mwanakwerekwe, Jinja, Eldoret, Kivu na maeneo mengine usipitwe na mchezo huu mtamu.
Mchezo utakuwa mubashara Azam Sports 1HD na tutakuletea updates hapa JamiiForums kupitia uzi huu...
Mchezo umeanza
2' Wenyeji wanamiliki mpira muda mwingi
8' Bado Ihefu wanaonekana kuwa na nguvu zaidi kuliko Simba
16' Simba wanafanya shambulizi kali, Baleke anapaisha mpira juu licha ya kufanya kazi nzuri ya kuwatoka walinzi
19' Shuti la Sakho linatoka nje kidogo ya lango
21' Mabadiliko kwa Simba, Sawadogo anatoka, anaingia Kapama
33' Gadiel Michael wa Simba anapata kadi ya njano kwa kucheza faulo
35' Mchezo una kasi na timu zinashambuliana kwa zamu
38' Yakouba anapata nafasi nzuri anashindwa kuitumia
45' Inaongezwa dakika moja ya nyongeza
MAPUMZIKO
Kipindi cha pili kimeanza
50' Simba wameanza mchezo kwa kasi na wanafika mara kwa mara langoni kwa Ihefu
60' Ihefu nao wanajibu mashambulizi
66' Simba wanapata faulo baada ya Mzamiru kuchezewa faulo
72' Yakouba anapiga kichwa kipa wa Simba anapangua inakuwa kona
81' Baleke anachezewa faulo karibu na lango la Ihefu
84' Jean Baleke anafunga goli la kwanza kwa Simba
87' Baleke anafunga goli la pili akimalizia kazi ya Kibu Denis
90' Mwamuzi anaongeza dakika 4 za nyongeza
FULL TIME