FT: Ivory Coast 1-2 Norway | World Cup 2026 | AT&T Stadium | 30 Juni, 2026 | Ivory Coast waaga mashindano

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Ivory Coast na Norway Wakutana kwa Mara ya Kwanza Hatua ya Mtoano ya Kombe la Dunia 2026

Timu mbili ambazo hazina uzoefu mkubwa katika hatua ya mtoano ya Kombe la Dunia, Ivory Coast na Norway, zitakutana katika Uwanja wa Arlington, Texas, kwenye mechi ya hatua ya 32 bora.

Ivory Coast imefuzu hatua hii kwa kumaliza nafasi ya pili katika Kundi E lenye ushindani mkubwa. Walikosa kuongoza kundi hilo kutokana na rekodi duni ya matokeo ya ana kwa ana dhidi ya Ujerumani, licha ya kuwa na alama sawa.

Kwa upande wa Norway, walipoteza nafasi ya kumaliza vinara wa Kundi I baada ya kufanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi chao kwa kubadilisha wachezaji 10 katika mchezo wa mwisho wa makundi dhidi ya Ufaransa. Hata hivyo, hatua hiyo imewapa nafasi ya kuwa na kikosi kilichopumzika vizuri kuelekea mchezo huu muhimu.

Rekodi ya Kukutana

Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Ivory Coast na Norway kukutana katika historia. Norway imeonyesha ubora dhidi ya timu za Afrika, ikipoteza mechi mbili pekee kati ya 19 walizocheza dhidi ya mataifa ya Afrika, huku ikishinda tisa na kutoka sare nane. Katika hatua ya makundi ya Kombe la Dunia 2026, Norway iliifunga Senegal mabao 3-2.
 
Mungu wa Africa awatunze
 
Ninawatakia Cote D'Ivoire kila la heri katika mechi yao ya leo dhidi ya Norway na ninawatahadharisha dhidi ya kucheza kwa kupaki basi hali ambayo inaweza kuwasababishia madhara makubwa sana.

Kulingana na uzoefu wangu wa muda mrefu kwenye mashindano haya ya kombe la dunia ni kwamba timu hizi za wazungu wakiona timu za Afrika zinashambulia sana zinapocheza nazo mara nyingi waga wanashikwa na kiwewe na kucheza kwa hofu kubwa sana hali ambayo hupelekea wao kuwa na wakati mgumu kushinda mechi.

Morocco ni moja ya timu za kiafrika zinazofahamu vizuri sana hiyo falsafa.
 
Back
Top Bottom