FT: Kagera sugar FC 0-0 Yanga SC | NBC premier League | Kaitaba stadium | 02.2.2024

FT: Kagera sugar FC 0-0 Yanga SC | NBC premier League | Kaitaba stadium | 02.2.2024

Katika wachezaji Yanga tulijua tumelamba dume na tulimuimba sana ni Max nzengeli, lakini cha ajabu kashuka kiwango vibaya mno. Kawa wa kawaida mno
Huyu jamaa sijui kimemkuta nini

Ila tatizo lake ambalo tangu mwanzo sikukubakiana naye ni kukaa na mpira muda mwingi mguuni.

Mchezaji wa aina hii huwa anaichelewesha sana timu
 
Dah! Aliyemroga Max Nzengeli ana roho mbaya sana. πŸ™
Hajarogwa

Sometimes mpira una muda unakukataa kabisa ni kama ilivyomtokea Baleke.

Sasa kama Club ndio itafanya tathmini kuwa kwa kipindi tulichonacho na uhitaji wa kufikia malengo yetu je anaweza kuwa sehemu ya kukwamisha mchakato wa kutimiza malengo?

Club iendelee kumpa muda mpaka arudi kwenye ubora wake ikiamini ni mchezaji mzuri ila yupo kwenye kipindi cha mpito?

Au kutokana na wakati ambao upo saizi haumudu kuwa na mchezaji mwenye kiwango hiki kwasababu Club ina malengo ya kufika mbali?
 
Kwa Camera gani?

Mechi za mkoani inapelekwa Camera moja tu nayo ina lensi ya Infinix

Ikitokea incident mchezaji kaipa mgongo Camera na kuhitaji Camera ya mbele iweze kukupa tukio linaloendelea hauwezi kupata ni mpaka usubirie jamaa ageuke na mpira kui face Camera

Sasa in that case ikafanyika faulo maana yake hauwezi kujua nini kimefanyika hata kama wakienda na hizo Tablets.

Mechi za hapo kwa Mkapa at least walikuwa aanaweka Camera nyuma ya goli lakini nazo mara kibao zimekuwa useless.

Ni nadra sana kuona zikitumika kwenye marejeo ya mpira.

Kingine ni mfumo wa replay kwa Azam unashida.

Replay za Azam zina mnato wa kama ku scratch yani hazipo proper kiukweli.
Afadhali, ingesaidia kidogo.
Tukio kama la leo, goli la kagera.
Yanga mtu kudaka nje ya box kuwekwa penati, kagere kukwatuliwa nje ya box simba kupewa penati na mengine mengi, ingesaidia saana sababu pamoja na kamera yao mbovu, na replay yao mbovu still sisi watizamaji wa runingani huwa tunaona kilichotokea.

Kwa ubovu wa waamuzi wetu ni aheri tutumie hizo hizo replays mbovu.
 
Back
Top Bottom