FT: Kagera sugar FC 0-0 Yanga SC | NBC premier League | Kaitaba stadium | 02.2.2024

Katika wachezaji Yanga tulijua tumelamba dume na tulimuimba sana ni Max nzengeli, lakini cha ajabu kashuka kiwango vibaya mno. Kawa wa kawaida mno
Huyu jamaa sijui kimemkuta nini

Ila tatizo lake ambalo tangu mwanzo sikukubakiana naye ni kukaa na mpira muda mwingi mguuni.

Mchezaji wa aina hii huwa anaichelewesha sana timu
 
Dah! Aliyemroga Max Nzengeli ana roho mbaya sana. πŸ™
Hajarogwa

Sometimes mpira una muda unakukataa kabisa ni kama ilivyomtokea Baleke.

Sasa kama Club ndio itafanya tathmini kuwa kwa kipindi tulichonacho na uhitaji wa kufikia malengo yetu je anaweza kuwa sehemu ya kukwamisha mchakato wa kutimiza malengo?

Club iendelee kumpa muda mpaka arudi kwenye ubora wake ikiamini ni mchezaji mzuri ila yupo kwenye kipindi cha mpito?

Au kutokana na wakati ambao upo saizi haumudu kuwa na mchezaji mwenye kiwango hiki kwasababu Club ina malengo ya kufika mbali?
 
Afadhali, ingesaidia kidogo.
Tukio kama la leo, goli la kagera.
Yanga mtu kudaka nje ya box kuwekwa penati, kagere kukwatuliwa nje ya box simba kupewa penati na mengine mengi, ingesaidia saana sababu pamoja na kamera yao mbovu, na replay yao mbovu still sisi watizamaji wa runingani huwa tunaona kilichotokea.

Kwa ubovu wa waamuzi wetu ni aheri tutumie hizo hizo replays mbovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…