FT: Ligi Kuu Bara | Simba SC 2-0 Kagera Sugar | Uwanja wa Mkapa | Agosti 20, 2022

FT: Ligi Kuu Bara | Simba SC 2-0 Kagera Sugar | Uwanja wa Mkapa | Agosti 20, 2022

Goli la mzungu limeshangiliwa sana inaonekana lilikuwa linasubiriwa kwa hamu Tanzania nzima, hata ndugu zangu wa uto naamini nao wameshangilia walikuwa wakimlilia mzungu...
Hapana,ni kwa sababu ni goli nusuduara.
 
Naaam..Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo Agosti 20, 2022 ambapo Wataalamu wa kusakata Kabumbu la viwango vya CAF Simba SC, Wekundu wa Msimbazi wanatunishana misuli na Kagera Sugar Wanankurukumbi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Mbiringe hii huenda ikawa ya hatari na ya kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 hasa ukizingatia Simba anataka kuendelea na ushindi baada ya kutakata mchezo wa kwanza kwa ushindi murua wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold huku Kagera Sugar wakihitaji ushindi baada ya kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza 2-1 dhidi ya Azam FC.

Kocha Msaidizi wa Simba SC, Suleiman Matola amesema kuwa mchezo wa kesho (leo) utakuwa mchezo nzuri na bora zaidi, na watahakikisha wanafanya kitu ambacho wanasimba wanahitaji, timu inapreform na kupata matokeo ya ushindi.

Naye Kocha wa Kagera Sugar Francis Baraza amesema kuwa, Simba SC ni timu kubwa na wanawapa heshima yao, wao wanakwenda kwenye mchezo wa Kesho (leo) kama Underdog, lakini mwisho wa siku mchezo ni dakika 90 ndo zitaamua matokeo.

Anayecheka mwisho ndiye anayefurahi zaidi...Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 Usiku. Usikose Ukapata Simulizi.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana



00' Mpira umeanza Uwanja wa Mkapa | Simba SC 0-0 Kagera Sugar

05' Simba SC wamepata Kona ambayo haikuzaa bao, huku mashambulizi yakiwa makali kwa timu zote.

10' Free Kick kuelekea Kagera Sugar, inapigwa lakini golikipa Kipao anatokea na kudaka mpira ule.

15' mchezaji wa Kagera yupo chini akipatiwa matibabu, bado safari ya kusaka ushindi inaendelea kwa pande zote mbili

Meshack anapiga shutii lakini linapaa nje ya lango, mpira umechangamka

19' Sakho anashindwa kufunga baada ya mpira kumbabatiza golikipa Kipao, ilikuwa nafasi sana lango la Kagera

Mfuko anacheza maridadi kabisa kuokoa hatari langoni kwake, ilikuwa hatari nyingine lango la Kagera.

25' Hussein anapiga Krosi dhaifu, golikipa Kipao anatokea na kudaka bila wasiwasi.

32' Peter anapiga Krosi lakini Mohamed Ouattara anacheza Krosi na kuondosha hatari ile

34' Mbaraka anapiga shutii, linambabatiza Henock na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao.

31' Okrah anapiga shutii kali, lakini golikipa Kipao anasafiri na kupangua na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao.

Aziz anapiga dochi na golikipa Manula anaokoa na kudaka bila wasiwasi.

41' [emoji460] Phiri Goooooooooooooaaal gooal

Moses Phiri anahesabu bao la kwanza baada ya free kick iliyopigwa na Chama kugonga mwamba na Phiri kumalizia.

Banda anakosa nafasi nzuri ya kufunga ilikuwa Shambulizi kali kuelekea lango la Kagera, namna gani Simba

Ouattara anafanya Kazi nzuri ya kuhakikisha hakuna madhara langoni kwake, anaubetua mpira na kuondosha hatari ile

45+2' Kagera wanakwenda sasa, lakini mpira ni mapumziko ambapo Simba wapo mbele ya bao moja kwa moja dhidi ya Kagera Sugar.

HT: Simba SC 1-0 Kagera Sugar

Naaam kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Mkapa, hakuna mabadiliko kwa pande zote mbili

49' Mwijage anapiga shutii lakini linapaa nje ya lango la Simba, huku Sakho akipaisha shuti lango la Kagera.

54' Kona kuelekea Kagera, Ouattara anakosa bao, baada ya shutii lake kuchezwa na golikipa Kipao.

Mashambulizi kwa pande zote, Kagera wanapata Kona ambayo inaondoshwa na walinzi wa Simba SC.

Sakho yupo chini baada ya kugongana na Beki wa Kagera Sugar.

61' Idd ameingia akichukua nafasi ya Mwijage, na Seseme akichukua nafasi ya mtu vile vile.

65' Phiri anapiga shutii linagonga mwamba na kumkuta Chama anaweka chini eneo la box refa anakataa.

Ametoka Phiri na ameingia Dejan Georgijevic, na ametoka Kapombe na ameingia Israel

Hamisi Kiiza ameingia, badala ya Makame, upande wa Kagera Sugar

Dejan Georgijevic anafanya balaa, anapiga chenga mbaya na kumpa Banda, Banda anapoteza

72' Mohamed Ouattara anaonyeshwa KADI ya Njano kwa mchezo mbaya.

Mbaraka anapoteza mpira, shutii lake linatoka sentimita chache ya lango.

Dejan, anatuliza kwa kifua kwake Banda, lakini anapoteza nafasi nzuri

78' Peter Banda anatoka na ameingia Mzamiru upande wa Simba SC.

Sakho anakosa nafasi nzuri ya kufunga ilikuwa Shambulizi kali mno, Kipao anatokea na kuokoa.

Dejan Georgijevic [emoji460]Goooooooooooooaaal gooal, Dejan anaipatia Simba SC bao la pili, bao murua kabisa.

84' ametoka, Okrah na Sakho na wameingia Kyombo na Okwa Simba SC.

89' Abeid anapiga shutii la chini chini, lakini golikipa Manula anadaka, huku Ouattara akiwa yupo chini baada ya kupata rabsha.

90+4' Kuelekea kumalizika kwa mchezo

Okwa anapiga Krosi lakini mpira unaokolewa na mabeki wa Kagera Sugar

Mpira upo Katikati ya uwanja kwake Chama anamtafuta Dejan Georgijevic

Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya Kagera Sugar

FT: Simba SC 2-0 Kagera Sugar

.... Ghazwat...
Wanaonesha king'amuzi gani? Nataka nicheki mechi hii, kali sana
 
Yote kwa yote, Gharib Mzinga anatangaza mpira vizuri sana.

Watangazaji wengine wa Azam Tv jifunzeni.
Mkuu kwa upqnde wangu qzam hawana mtangazaji makini kama Gharib mzinga
Jamaa anawafaham wachezaj na anatangaza mpira, hana kelele kelele saut makin kabisa
Namkubal sana hata gem ya simba vs kagera nimeenjoy san jamaa kuitangaza leo
 
Mkuu kwa upqnde wangu qzam hawana mtangazaji makini kama Gharib mzinga
Jamaa anawafaham wachezaj na anatangaza mpira, hana kelele kelele saut makin kabisa
Namkubal sana hata gem ya simba vs kagera nimeenjoy san jamaa kuitangaza leo
Huyu ndie mtangazaji Bora wa boli Tanzania kwasasa..ukitaka kumuelewa subiri akianza kutajga a mechi za kimataifa..anajua wachezaji wote Tena vizuri Sana..
 
Kanoute ni injini isiyokuwa na makeke Unaweza kuifananisha Na Paul Scholes enzi zile Za Mzee Ferguson Man U, kimya kimya Lkn Wapinzani Moto Wanaupata.
Mimi namuelewa sana jamaa ana nguvu na anajiamini sana,asiuzweeeeeee
 
Screenshot_20220820-220503_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom