We hujacheka kweliCheka tu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
We hujacheka kweliCheka tu
Lkn juzi ulisema kua ,mzungu tumepigwa.Mzungu anapongezwa na timu nzima,duuuh ❤❤❤❤
Hapana,ni kwa sababu ni goli nusuduara.Goli la mzungu limeshangiliwa sana inaonekana lilikuwa linasubiriwa kwa hamu Tanzania nzima, hata ndugu zangu wa uto naamini nao wameshangilia walikuwa wakimlilia mzungu...
Wanaonesha king'amuzi gani? Nataka nicheki mechi hii, kali sanaNaaam..Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo Agosti 20, 2022 ambapo Wataalamu wa kusakata Kabumbu la viwango vya CAF Simba SC, Wekundu wa Msimbazi wanatunishana misuli na Kagera Sugar Wanankurukumbi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.
Mbiringe hii huenda ikawa ya hatari na ya kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 hasa ukizingatia Simba anataka kuendelea na ushindi baada ya kutakata mchezo wa kwanza kwa ushindi murua wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold huku Kagera Sugar wakihitaji ushindi baada ya kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza 2-1 dhidi ya Azam FC.
Kocha Msaidizi wa Simba SC, Suleiman Matola amesema kuwa mchezo wa kesho (leo) utakuwa mchezo nzuri na bora zaidi, na watahakikisha wanafanya kitu ambacho wanasimba wanahitaji, timu inapreform na kupata matokeo ya ushindi.
Naye Kocha wa Kagera Sugar Francis Baraza amesema kuwa, Simba SC ni timu kubwa na wanawapa heshima yao, wao wanakwenda kwenye mchezo wa Kesho (leo) kama Underdog, lakini mwisho wa siku mchezo ni dakika 90 ndo zitaamua matokeo.
Anayecheka mwisho ndiye anayefurahi zaidi...Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 Usiku. Usikose Ukapata Simulizi.
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
00' Mpira umeanza Uwanja wa Mkapa | Simba SC 0-0 Kagera Sugar
05' Simba SC wamepata Kona ambayo haikuzaa bao, huku mashambulizi yakiwa makali kwa timu zote.
10' Free Kick kuelekea Kagera Sugar, inapigwa lakini golikipa Kipao anatokea na kudaka mpira ule.
15' mchezaji wa Kagera yupo chini akipatiwa matibabu, bado safari ya kusaka ushindi inaendelea kwa pande zote mbili
Meshack anapiga shutii lakini linapaa nje ya lango, mpira umechangamka
19' Sakho anashindwa kufunga baada ya mpira kumbabatiza golikipa Kipao, ilikuwa nafasi sana lango la Kagera
Mfuko anacheza maridadi kabisa kuokoa hatari langoni kwake, ilikuwa hatari nyingine lango la Kagera.
25' Hussein anapiga Krosi dhaifu, golikipa Kipao anatokea na kudaka bila wasiwasi.
32' Peter anapiga Krosi lakini Mohamed Ouattara anacheza Krosi na kuondosha hatari ile
34' Mbaraka anapiga shutii, linambabatiza Henock na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao.
31' Okrah anapiga shutii kali, lakini golikipa Kipao anasafiri na kupangua na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao.
Aziz anapiga dochi na golikipa Manula anaokoa na kudaka bila wasiwasi.
41' [emoji460] Phiri Goooooooooooooaaal gooal
Moses Phiri anahesabu bao la kwanza baada ya free kick iliyopigwa na Chama kugonga mwamba na Phiri kumalizia.
Banda anakosa nafasi nzuri ya kufunga ilikuwa Shambulizi kali kuelekea lango la Kagera, namna gani Simba
Ouattara anafanya Kazi nzuri ya kuhakikisha hakuna madhara langoni kwake, anaubetua mpira na kuondosha hatari ile
45+2' Kagera wanakwenda sasa, lakini mpira ni mapumziko ambapo Simba wapo mbele ya bao moja kwa moja dhidi ya Kagera Sugar.
HT: Simba SC 1-0 Kagera Sugar
Naaam kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Mkapa, hakuna mabadiliko kwa pande zote mbili
49' Mwijage anapiga shutii lakini linapaa nje ya lango la Simba, huku Sakho akipaisha shuti lango la Kagera.
54' Kona kuelekea Kagera, Ouattara anakosa bao, baada ya shutii lake kuchezwa na golikipa Kipao.
Mashambulizi kwa pande zote, Kagera wanapata Kona ambayo inaondoshwa na walinzi wa Simba SC.
Sakho yupo chini baada ya kugongana na Beki wa Kagera Sugar.
61' Idd ameingia akichukua nafasi ya Mwijage, na Seseme akichukua nafasi ya mtu vile vile.
65' Phiri anapiga shutii linagonga mwamba na kumkuta Chama anaweka chini eneo la box refa anakataa.
Ametoka Phiri na ameingia Dejan Georgijevic, na ametoka Kapombe na ameingia Israel
Hamisi Kiiza ameingia, badala ya Makame, upande wa Kagera Sugar
Dejan Georgijevic anafanya balaa, anapiga chenga mbaya na kumpa Banda, Banda anapoteza
72' Mohamed Ouattara anaonyeshwa KADI ya Njano kwa mchezo mbaya.
Mbaraka anapoteza mpira, shutii lake linatoka sentimita chache ya lango.
Dejan, anatuliza kwa kifua kwake Banda, lakini anapoteza nafasi nzuri
78' Peter Banda anatoka na ameingia Mzamiru upande wa Simba SC.
Sakho anakosa nafasi nzuri ya kufunga ilikuwa Shambulizi kali mno, Kipao anatokea na kuokoa.
Dejan Georgijevic [emoji460]Goooooooooooooaaal gooal, Dejan anaipatia Simba SC bao la pili, bao murua kabisa.
84' ametoka, Okrah na Sakho na wameingia Kyombo na Okwa Simba SC.
89' Abeid anapiga shutii la chini chini, lakini golikipa Manula anadaka, huku Ouattara akiwa yupo chini baada ya kupata rabsha.
90+4' Kuelekea kumalizika kwa mchezo
Okwa anapiga Krosi lakini mpira unaokolewa na mabeki wa Kagera Sugar
Mpira upo Katikati ya uwanja kwake Chama anamtafuta Dejan Georgijevic
Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya Kagera Sugar
FT: Simba SC 2-0 Kagera Sugar
.... Ghazwat...
Nenda kampe zawadi hii 🌹Safi sana Mzungu wetu
Kanoute akishampiga mtu msasa wa kimya kimya hajawahi kumkubalia refa wala kuomba msamaha hahahaKuna misasa inapigwa kimya kimya
Mkuu kwa upqnde wangu qzam hawana mtangazaji makini kama Gharib mzingaYote kwa yote, Gharib Mzinga anatangaza mpira vizuri sana.
Watangazaji wengine wa Azam Tv jifunzeni.
Aaa sisi tenaa tufungwe tupo tufunge tupo drooo tupo kuitetea timu yetu,hii ndo maaana ya Simba guvu moyaSimba SC Ndo Wenye Hizi Kazi Yaani
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
Nguvu Moja [emoji881]
Huyu ndie mtangazaji Bora wa boli Tanzania kwasasa..ukitaka kumuelewa subiri akianza kutajga a mechi za kimataifa..anajua wachezaji wote Tena vizuri Sana..Mkuu kwa upqnde wangu qzam hawana mtangazaji makini kama Gharib mzinga
Jamaa anawafaham wachezaj na anatangaza mpira, hana kelele kelele saut makin kabisa
Namkubal sana hata gem ya simba vs kagera nimeenjoy san jamaa kuitangaza leo
Mimi namuelewa sana jamaa ana nguvu na anajiamini sana,asiuzweeeeeeeKanoute ni injini isiyokuwa na makeke Unaweza kuifananisha Na Paul Scholes enzi zile Za Mzee Ferguson Man U, kimya kimya Lkn Wapinzani Moto Wanaupata.
Mkuu MENEMENE TEKERI NA PERESI Tulibaki wacheche kuamini Dejan Georgijevic ana kitu cha kuonyesha uwanjani.Ghazwat where are you bro ? God katujibu asee[emoji120][emoji120]
Tena hawa mabint wapo motoo Simba rahaaa.Wana simbaaaaaa.....,,,,, SIMBA QUEENS IMENINGIA NUSU FAINALI KWA KUMTOA MTU 4 KWA SUFURI........,,,naaachaje sasa kushabikia Simba. Ni raha tuu kwetu ni furaha
Mnoooo yani kaka zao wakizingua tunaenda kule yani simba haiboi haipoiiTena hawa mabint wapo motoo Simba rahaaa.
SIMBA 1-2 KAGERA
Matokeo yasipokuwa hivyo mniite mbwa nimekaa pale. Leo kati ya kocha, wachezaji, au kiongozi wowote ataondolewa pale msimbazi.