Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
We naye kumbe yanga?Kulikuwa na ulazima gani mechi hii kuchezwa usiku? Wanamaliza umeme wa bure....
Hawa wanatakiwa wacheze saa 2 asubuhi.
kutolewa raundi ya awali CAF CLYa kwenda wapi
Wewe ulitaka yakwenda wapi?Ya kwenda wapi
Ngap ngapi hapo??Ametoka Nonga na ameingia Joseph upande wa Mbeya City
Maji yanaanza kujitenga na mafutaWe naye kumbe yanga?
Mashabiki wengine ndio tumeanza kuwajua leo kumbe mpo wengi ila ule ukame wa miaka 4 uliwaficha wengi
Mods futeni huu uzi,hauna watu wala tija yoyote wanatujazia serverNimekuuliza, basi angalau stick kwenye swali kuhusu mipasho najua hiyo ni desturi yenu
Kwahiyo mnagombea nini hasa hapa?Sakho Goooooooooooooaaal gooal
Sakho anaipatia Simba SC bao la pili akipokea pasi ndefu kutoka kwa Mzamiru
Simba SC 2-0 Mbeya City FC
Hiyo Server ni ya baba yako?Mods futeni huu uzi,hauna watu wala tija yoyote wanatujazia server
Mbona hasira kolo wa kike? Taratibu 😂Wewe ulitaka yakwenda wapi?
Ubingwa mmepata Ila bado mnastressMods futeni huu uzi,hauna watu wala tija yoyote wanatujazia server
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo Juni 16 2022 ambapo Mnyama Mkali Mwituni, mtaalamu mbobezi wa kusakata Kabumbu lililothibitishwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF Simba SC kutoka viunga vya Msimbazi Jiji Dar es salaam, anashuka kwenye Dimba la Benjamin Mkapa kukipiga na Klabu ya Mbeya City, kutoka Jiji la Mbeya.
Je? Nani yupo tayari kuweza kuibuka na matokeo ya ushindi. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1: 00 Usiku.. Usikose Ukaadithiwa.
Kulitaka Mwana.......Kulipewa Mwana
Kikosi cha Simba SC
Beno
Israel
Hussein
Henock
Wawa
Mzamiru
Kanoute
Kibu
Bwalya
Sakho
Kikosi cha Mbeya City
Mandanda
Kunambi
Mwakinyuke
Maganga
Shemvuni
Andambwile
Ibrahim
Jamal
Nonga
Luzio
Ng'odya
Mwamuzi kwa kati ni Ramadhan Kayoko.
=========================
Naaam mpira umeanza Uwanja wa Benjamin Mkapa..Vita vya dakika 90 za jasho na damu.
00' Simba SC 0-0 Mbeya City
03' Kibu Denis anakosa nafasi nzuri ya kufunga baada golikipa mandanda kuuwahi mpira na kuudaka.
07' free kick kuelekea Mbeya City, Bwalya anapiga, lakini mabeki wa City wanacheza kwa kichwa na kuokoa
10' Hussein anapiga free kick nyingine, lakini mpira unaambaa ambaa pembeni ya uwanja.
15' Bado Milango ni migumu hakuna timu imeona lango, Luzio anapiga shutii la mbali lakini linapaa nje ya lango.
Kibu anapiga Krosi lakini inapotea baada ya kukosa mtu wa kupokea
Krosi ya Hussein Kibu anashindwa kutuliza na kuweka kambani, ilikuwa nafasi nzuri ya kufunga bao
21' Umiliki wa Simba SC mpaka sasa huku City wakiwa wamefanya mashambulizi machache.
Kibu yupo chini baada ya kuangushwa eneo la hatari, refa anakataa
27' Shemvuni anaonyeshwa KADI ya Njano kwa mchezo mbaya
32' Kibu anaweka kambani, lakini refa anasema ni Offside..Bado Milango ni migumu huku Simba wakitalawa dimba
Sakho anaangushwa ndani ya box na golikipa wa City ni Penalty, anakwenda kupiga Sakho
Goooooooooooooaaal gooal Simba SC 1-0 Mbeya City
43' Mbeya City wameamka sasa wanashambulia lango la Simba SC inapigwa kuleeeee Nje.
Golikipa wa City yupo chini baada ya kupata rabsha, ameinuka mpira unaendelea
45+2' kuelekea kuwa mapumziko
Simba wanakosa nafasi nyingine ya kufunga hapa, ilikuwa hatari eneo la City
Mpira ni mapumziko ambapo Simba SC wanatoka mbele kwa bao moja kwa bila dhidi ya Mbeya City
HT: Simba SC 1-0 Mbeya City FC
Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Mkapa
50' Simba wanajitahidi kutafuta mpenyezo kwa mabeki wa City, lakini City wanakaa imara
Andambwile anakwenda lakini golikipa Beno anadaka bila wasiwasi
Kibu yeye na lango lakini anapiga njeee, namna gani huyu Kibu Denis
City wanapata Kona inapigwa kulee lakini mpira unaokolewa.
55' Sakho anakwendaaa Goooooooooooooaaal gooal, Sakho anaipatia Simba SC bao la pili akipokea pasi ndefu kutoka kwa Mzamiru
Simba SC 2-0 Mbeya City FC
City wanapata Free Kick inapigwa kulee lakini unambabatiza ukuta na kuwa Kona ambayo haikuzaa bao
60' Simba wanakosa nafasi ya kufunga kupitia kwa Kanoute, ilikuwa nafasi nzuri ya kufunga
Nonga anatoka na anaingia Joseph upande wa City
63' Ametoka Sakho na Kibu na nafasi zao zimechukuliwa na Kagere na Banda.
Free Kick inapigwa kuelekea City inapigwa kulee lakini mpira unaokolewa na golikipa wa City
71' Almanusura City wapate bao baada ya mpira kugonga mlingoti na kuokolewa na mabeki wa Simba
Basi punguza hasira koloMods Kamwe hawawezi wakawasikiliza Wapunguami wa Akili