Unaonekana mbishi hatari, ajabu unaita uamuzi wa kocha foolish attempt wakati tulishinda!, ndio maana nakwambia una maneno mengi lakini hamna pointi.
Zaidi, unanipa mifano inayoonesha ubovu wa hoja zako, kama wa Yanga wanavyomtegemea Mayele, wakati unaona kila siku anafunga huyo pekee, asipokuwepo mambo yao yanakuwa magumu, kila siku wanashinda 1-0! huu ushamba ndio umeuweka kichwani kwako, ajabu kabisa..!!
Sasa nakupa na mfano uone vile kile unachotetea hakina maana, usipoelewa tena, OVER!.
Nimekwambia mpira wa siku hizi hautakiwi kumtegemea mtu mmoja, kusema mpira ni namba, lakini hizo namba lazima ziendane na ushirikiano wa timu nzima, sio timu haichezi ila inamtegemea mchezaji mmoja aamue matokeo kwa uwezo wake binafsi kama unavyoamini, huu ndio ushamba naokwambia na hautakiwi kuwepo.!
Mfano: Tuliona Simba siku za karibuni ikicheza bila Chama, alikuwa amepewa adhabu ya kufungiwa mechi tatu, kila mmoja hakuwa na uhakika na matokeo, performance ya timu ikawa mbovu, kisa Chama hayupo! huu ndio ushamba naokwambia ambao hautakiwi kuwepo, hapa sio suala la individual statistics au vinginevyo kama unavyodai, ni TEAM PERFOMANCE kwanza...sijui kwanini unakuwa mgumu kuelewa...!!
NB. Individual performance ije pale ambapo game imekuwa ngumu timu haitembei, as a secondary attempt, sio kwenda uwanjani kutegemea ubora binafsi wa mchezaji, vipi akiamka vibaya, na timu haichezi bila yeye na statistics zake kama unavyodai? that's nonsense.
Tchao..!
Ishu ya ubishi ni kweli mi ni mbishi tena sana tu hata mtaani niko hivyo, nimejaribu kuishi nje ya mfumo huo nimejikuta nashindwa.
Ebu tuondoke eneo hilo
Mkuu unanipa mashaka kama hizi hoja unazoziweka hapa zinatoka kwa mtu anayeujua mpira
Foolish attempt haiwezi kusawazishwa kwa kuangalia matokeo ya ujumla, foolish attempt inapimwa kwa kuangalia impact ya sub ilivyoingia ilifanya kitu gani kuinufaisha timu?
Kwasababu huo ushindi unaousema umechangiwa na huyo huyo unayefurahia kutolewa, na huyo mchezaji wako Kibu baada ya kuingia alifanya kitu gani cha maana kuisaidia timu i-maintain ushindi au kuiongezea mabao?
Zaidi tunaona ni muendelezo ule uoe ambao tumekuwa tukimuona akicheza hovyo na kuzidi kutuweka kwenye high risk kiasi tutamani mechi iishe ilihali wapinzani wapo outnumber.
Sasa Mkuu kupitia mfano wako wa Mayele hujaona kama unajitukana mwenyewe hapo?
Saizi unaonekana kufurahia Mayele kuendelea kucheza kwasababu yeye ndio mfungaji na ana machango mkubwa ndani ya timu
Wakati huo kwa Chama jambo kama hilo umeliita kuwa ni biashara kichaa
Tukuelewe vipi mzee?
Mpira hautakiwi kumtegemea mtu mmoja lakini ni jambo linalofahamika kuwa mchezaji bora mwenye kiwango bora ndiye mwenye nafasi kubwa ya kucheza muda mwingi kiwanjani kutokana na impact yake.
Kusema namba lazima ziendane na ushirikiano hili ni jambo ambalo wewe mwenyewe unatakiwa kutafakari kabla hujaandika. Kibu tangu ameanza kucheza ni lini uliona ananyimwa ushirikiano kiasi kwamba iwe ndio sababu ya yeye kuwa kwenye kiwango hiki kisicho ridhisha?
Kibu game ya Singida alikosa magoli zaidi ya matatu, zote ni pasi alizokuwa anapewa kupitia ushirikiano na timu mates wenzake
Sasa huo ushirikiano ambao hata mtu akipewa hawezi kuutumia, kuna haja gani ya kuendelea kumtoa mchezaji ambaye ana take advantage kwenye team work na kumuweka mchezaji goi goi ambaye anaigharimu timu?
Sasa mzee mbona unanichanganya??
Chama kukosa mechi tatu ni uzembe wa nani?
Mbona kama una generalize wakati inafahamika tatizo ni nani?
Uliangalia hizo mechi uzembe ulikuwa kwenye nafasi aliyokosekana Chama?
Huo ni uzembe wa mtu mmoja ambaye leo unamtetea ambaue ni Kibu aliyekuwa anakosa magoli ya wazi.