FT: Ligi Kuu Bara | Simba SC 7-1 Tanzania Prisons | Uwanja wa Benjamin Mkapa 30/12/2022

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Mbiringe au Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara[emoji1241] kuendelea kugombewa leo Disemba 30,2022 ambapo Wataalamu wa kusakata kabumbu lenye viwango vya CAF Wekundu wa Msimbazi Simba SC[emoji881] wanawakabili Wajelajela Tanzania Prisons🟢 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam[emoji2522]

Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 12: 15 Jioni[emoji354]..Usibonyeze Kitufe.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.


=========

00' Mpira umeanza Uwanja wa Benjamin Mkapa, dakika 90 za Jasho na Damu.

Timu zimeanza Kwa mashambulizi ya kasi huku kila timu ikijaribu kutafuta bao la mapema.

12' [emoji460] Goooooooooooooaaal gooal
John Bocco anaweka kambani bao la kwanza akipokea Krosi murua kutoka kwa Ntibanzokiza, Simba SC 1-0 Tanzania Prisons.

Samson Mbangula anaonyeshwa Kadi Nyekundu baada ya kuchelewa faulo Henock..Ametolewa nje Henock na ameingia Kennedy

29' [emoji460] Goooooooooooooaaal gooal
Jeremiah Juma anasawazisha bao kwa Tanzania Prisons, Simba SC 1-1 Tanzania Prisons.

45+3' Kuelekea kuwa mapumziko, timu zikiwa zimefungana bao moja kwa moja

Naaam mpira ni mapumziko.
HT: Simba SC 1-1 Tanzania Prisons

46' [emoji460] Goooooooooooooaaal gooal
John Bocco anaweka kambani bao la pili akipokea pasi murua kutoka kwa SAKHO

55' Kanoute anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa mchezo mbaya.

58' Sakho anawasha moto ile mbaya, anapangua mabeki, na kumpasia Ntibanzokiza naye anashindwa kufunga bao ilikuwa nafasi nzuri.

60' [emoji460]Ntibazonkiza Goooooooooooooaaal gooal, anaweka kambani bao la Tatu akipokea pasi murua kutoka kwa Chama.

Umiliki wa Simba SC, Wajelajela wameshikwa ile mbaya.

62' [emoji460] Bocco Goooooooooooooaaal
John Bocco anaweka kambani bao la nne, kazi nzuri ya Chama.

63' [emoji460] Ntibazonkiza Goooooooooooooaaal gooal, anaweka kambani bao Tano.

70' [emoji460]Ntibazonkiza Goooooooooooooaaal gooal, anaweka kambani bao la SITA, akipokea pasi ya Mzamiru.

Tanzania Prisons Uwanja umeinama upande wao, Simba wanakuja kama mvua.

87' [emoji460]Kapombe Goooooooooooooaaal gooal, Shomari Kapombe anahesabu bao la Saba, akipokea Krosi ya Gadiel.

Kuelekea kumalizika kwa mchezo ambapo Simba SC wapo mbele ya mabao Saba kwa moja.

90+3' Naaaaaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba SC [emoji881] wameibuka na ushindi mnono wa mabao Saba kwa moja dhidi ya Timu ngumu ya Tanzania Prisons🟢

FT: Simba SC 7-1 Tanzania Prisons

..... Ghazwat[emoji2424]....
 
00' Naaam mpira umeanza Uwanja wa Benjamin Mkapa | Simba SC 0-0 Tanzania Prisons
 
Hivi ni mimi tu nayeona Camera za Azam leo zinaomesha HD kuliko siku zote?
 
Henock yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kupata rabsha
 
Hiyo ndio njia pekee ya kumzuia Chama
 
08' Simba SC wamefanya Shambulizi, lakini halikuzaa bao, na kuwa salama lango la Prisons
 
10' Mbangula alijaribu kupenya ngome ya Simba, lakini Onyango na Henock wanakaa imara.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…