FT: Ligi Kuu: Yanga S.C 1-0 Ruvu Shooting: Uwanja wa Mkapa, 23/01/2023

FT: Ligi Kuu: Yanga S.C 1-0 Ruvu Shooting: Uwanja wa Mkapa, 23/01/2023

babu onyango

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2023
Posts
378
Reaction score
984
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Nbc na mabingwa wa muda wote nchini Tanzania[emoji1241] Young Africans S.C[emoji617] almaarufu Yanga leo tena wanashuka dimbani kukabiliana na maafande wa Ruvu shooting katika mwendelezo wa ligi kuu ya Nbc...

Mchezo huo utakuwa mgumu Kwa timu zote kwani Yanga[emoji617][emoji617] wanataka kushinda ili kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi ya Nbc huku Ruvu shooting[emoji1949][emoji1949] nao wakiitaji alama zote tatu ili kujinasua kutoka mkiani mwa ligi.

Mchezo huu utapigwa kunako dimba [emoji2522] la Benjamini Mkapa mnamo saa1.00 usiku

Je ni Wananchi[emoji617][emoji617] au Mafande[emoji1949][emoji1949] ndio watakao ondoka na kicheko[emoji1][emoji1] baada ya dakika 90?? Kuwa nami mwanzo paka mwisho wa kipute

"" Wachezaji wa timu zote mbili wapo uwanjani[emoji2522] wakipasha misuli[emoji1732][emoji3571][emoji125]ili kujiweka sawa[emoji91][emoji91]

'''""""""""'''''"""""''""”"”""""""'"""""""""

00" Kipenga Cha mwamuzi kimepulizwa kuashiria Mpira[emoji460][emoji460] umeanza hapa kadika Dimba[emoji2522] la Benjamini Mkapa katika

02" Hatari langoni mwa Yanga [emoji617] ila mpira unaenda nje inakuwa ni goal kick

05" Ruvu shooting [emoji1949][emoji1949] wameanza vizuri mchezo wa leo huku utulivu ukiwa mkubwa

10" Kennedy Musonda yupo chini akipatiwa matibabu baada ya kugongana na goalkeeper wa Ruvu shooting

15" Mayele anaachia shuti kali lakini linapanguliwa na Mlinda mlango wa Ruvu shooting inakuwa Kona ambayo haikuzaa matunda

25" Bado milango ni migumu kwa timu zote

32" Gooooal[emoji460] Yanga [emoji617] wanatangulia Kwa bao Moja baada ya beki Mpoki Mwakinyuke kujifunga

40" Mayeleeeee....... Golikipa wa Ruvu anaokoa inakuwa ni kona. Hii ni Kona ya 5 Kwa Yanga wakati Ruvu hawajapa kona paka sasa

42" Moloko anapaisha akiwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga. What a miss!

45" Shambulizi lingine langoni mwa Ruvu shooting lakini mpira unakwenda nje.

HT" Naaam ni mapumziko katika uwanja[emoji2522] wa Benjamin Mkapa Wananchi [emoji617] wakiongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu shooting.

Tukutane kipindi cha pili

"Kipindi cha pili kimeanza

49" Mayele anapoteza nafasi ya wazi kufunga goli la pili Kwa Yanga akiwa yeye na goli

62" Mayele anapiga kichwa kikali langoni mwa Ruvu shooting lakini golikipa anatoa mpira nje inakuwa kona ambayo haikuzaa goli

65" Yanga wamefanya mabadiliko ya wachezaji watatu kwa mpigo, wametoka Musonda, Farid,Moloko na Nafasi zao zimechukuliwa ni Mzize, Ambundo pamoja na Aziz K
Mechi imechangamka sana

80" Bado Yanga anaongoza kwa goli 1-0

87" Yanga [emoji617] wanapata faulo eneo zuri, Aziz K anapiga gooal lah lah golikipa wa Ruvu shooting anadaka vizuri kabisa[emoji122][emoji122]

90+3" Naam mpira umekwisha hapa Uwanja[emoji2522] wa Benjamin Mkapa timi ya Yanga inaondoka na alama zote 3 na kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Nbc kwa kufikisha jumla ya point 56 huku Ruvu shooting wakisalia mkiani mwa msimamo wa ligi.

Mlikuwa nami Babu Onyango kwa Dak zote 90 za mtanange huu[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
hadi wakati mwingine[emoji1666][emoji1666]

20230123_181631.jpg
20230123_181803.jpg
 
Ni swala la mda bahasha nzianze kufanya kazi
 
Back
Top Bottom