FT' Mauritania 0-1 Tanzania | Mechi ya kundi 'B' CHAN | Mkapa Stadium | Agosti 6, 2025 | Saa 2:00 Usiku

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Hii leo Katika Uwanja wa Taifa Benjamin Mkapa, Tanzania (Taifa Stars) itacheza na Mauritania kwenye mechi ya Kundi 'B' katika Michuano ya African Nations Championship (CHAN), ikiwa ni mechi ya pili ya Kundi baada ya kuanza kwa Tanzania kwa ushindi wa 2‑0 dhidi ya Burkina Faso siku ya Ijumaa, Agosti 2, 2025.
​
Your browser is not able to display this video.


Kikosi Cha taifa stars kinachoanza dhidi ya Mauritania katika mchezo wa pili wa CHAN kundi B

​
Your browser is not able to display this video.



Dakika ya 30' Shambulizi la Sopu linazimwa na mabeki wa mauritania

Dakika ya 34' Golikipa wa stars anatoa mpira nje mauritania wanapata Kona

Dakika ya 73' kijana Pipino anatolewa nje baada ya kuumia anaingia kijana Shekhani Khamis


Dakika ya 41' golikipa wa Mauritania anaigomea stars kupitia kwa golikipa wao Sarr

Kipindi cha kwanza kimekwisha Mauritania 0-0 Tanzania

Mabadiliko katika kipindi cha pili anatoka yusuph kagoma anaingia Ahmed Pipino ,anaingia Nassor Saadun kuongeza nguvu eneo la mbele anatoka Abdul suleiman (Sopu).

Dakika ya 60' Stars wanafanya shambulizi la maana kupitia kwa mzize hakuna goli Mauritania 0-0 Tanzania

Dakika ya 73' kijana mdogo Pipino anatoka baada ya kuumia anaingia Shekhan Khamis anachukua nafasi yake.

Mauritania wanafunga Booster Tetah anachukua nafasi ya Sidi Touda

Dakika ya 77' Mzize anaonywa kwa kadi ya Njano

Mauritania wanaitaka sare wameaanza kupoteza muda sasa kwa dakika 10 zilizobaki

Dakika ya 80'Kapombe anafunga goli kwa taifa stars

Mchezo umekwisha, Mchezo ujao wa Kundi B, Tanzania inatarajiwa kuivaa Madagascar mnamo Agosti 9, 2025, siku hiyo pia Jamhuri ya Kati itaivaa Mauritania.
 
Watu wamevurugwa aisee, yaani hadi matokeo yamewekwa wakati mechi ni saa mbili usiku
 
Haya wenye timu yenu mnakaribishwa kuitakia ushindi mnono. Mimi kwa sasa nimechukua kwa muda uraia wa Burundi. Kwa hiyo nitaendelea kubakia kuwa mpenzi mtazamaji.
 
Kwa vile Taifa Stars ilishinda dhidi ya Burkina Faso basi nina uhakika tutashinda pia dhidi ya hawa maponjoro wa baharini huku wachezaji wa Yanga waking'aa
 
Haya kwa bukinabe walibahatisha, Sasa leo madogo hawachomoki!
 
Mchawi ndugu😆

Mkuu wewe una uhakika wa kula na kunywa maji safi leo, huko vijijini watu huo uhakika hawana, ni bora hela za magoli zisaidie watanzania wenzetu.

Hata kuchimba visima inatosha.
 
Hawa Mauritania wana kocha haswa! Timu ipo very compacted

Leo taifa Stars wakaze la sivyo yatawakuta😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…