FT: Mighty Wanderers 0-1 Simba SC | CAFCL-1st Leg | Wakali wa Kimataifa wafanya kweli | 06.09.2026

Hongera Simba kwa kupata ushindi lakini wachezaji na benchi la ufundi walikuwa na makosa mengi sana kiasi iwapo leo wangekutana na timu nzuri ingewagharimu sana. Kwa mechi ya leo ingekuwa ile Simba ya akina Bocco, Kagere, Chama na wengineo sasa hivi wangekuwa wameshajihahkikishia kusonga mbele. Ila Simba hii tia maji tia maji inajichelewesha yenyewe.

1. Kasali ana foot work mbovu sana lakini anajiamini balaa na chenga yake inatabarika. Ni basi tu ana bahati sio kwenye ligi ya ndani au kimataifa mpaka sasa hajatokea mchezaji wa kuweza kumsoma. Arudi akaangalie baada ya Roger Milla kumsoma Rene Higuitta nini kilitokea. Pia tabia yeke ya kupiga pasi usawa wa kati kati ya goli badala ya pembeni siku sio nyingi atatoa mlio.
2. Mligo naye ni mzigo tu. Huu msimu wa pili kwake lakini bado habadiliki kabisa. Anachojua yeye akipata mpira ni kuwapasia mabeki wake wakati au kiungo mkabaji basi kashamaliza kazi. Kuna muda anapata mpira mbele yake kuna nafasi wazi lakini hatembei kabisa na mpira kuisogeza timu juu. Kibabage sio mzuri sana lakini huwa ana take risk kwenda mbele kusaidia kuipush timu izidi kusogelea lango la adui.
3. Jabaar, Maema na Kagoma wote walikuwa wanacheza chini muda mwing wa mchezo kiasi ikawa shida kwa Simba kupeleka mashambulizi mbele. Mpaka Chama alipoingia ndio walau timu ilianza kusogea mbele.
4. Benchi la ufundi limezingua sana kwa sub ya Mpanzu. Doumbia alipoingia aliwaacha wale mabeki wa kati wa timu pinzani wafanya wanavyotaka kuanzisha mashambulizi kwa sababu walikuwa hawana mtu wa kuwakaba kama alivyokuwa Mpanzu mwanzoni mwa mchezo. Doumbia tatizo lake kubwa hajui kuwa yeye ni mtu wa mwisho anatakiwa asimame na wale mabeki wakati ili wasianzishe mashambulizi na hata ikitokea wamefanya makosa yeye afunge. Badala yake anarudi chini sana na kuwaacha mabeki wa timu pinzani watengeneze mashambulizi kuanzia nyuma.
5. Ni wakati sasa wa viongozi wa Simba kuwaeleza aina ya mkataba alionao Doumbia maana lazima acheze kila mechi wakati akiingia kazi yake kubwa ni kuanguka anguka, kukaba wenzake na kuzuia pasi zisiwafikie wachezajia wenzake. Ni kama vile Doumbia ana mkataba kama aliokuwa nao Saidoo Ntibazonkiza kila mechi lazima acheze.
6. De Reuck ni bonge la beki. Lakini ule upuuzi wake wa kukaa na mpira muda mrefu halafu anaanza kutembea nao anachelewesha sana mashambulizi na inawafanya timu pinzani ijipange. Sio kila mpira lazima uanze kwa build up kuanzia nyuma.
7. Kocha wa viungo hapo Simba aangaliwe vizuri. Timu haina utimamu kabisa wa mwili na hasa dakika za mwishoni timu inapoteana sana wachezaji wanabaki wanakaba kwa macho. Kama wamalawi wangekuwa makini leo kuna aibu ilikuwa inaenda kutoea dakika za mwishoni

Benchi la ufundi la Simba lazima libadilishe mfumo wa uchezaji. Haiwezekani timu inafika kwenye robo ya tatu ya uwanja halafu mpira unarudishwa nyuma. Ndio maana ushindi wa Simba siku zoteunakuwa wa shida sana na akishinda goli nyingi sana ni mbili hata kama wana uwezo wa kuipiga hiyo timu goli kumi. Na hapo utakuta viongozi, benchi la ufundi na wachezaji wanaridhika kabisa. Wachazeji wanaanza kutembea uwanjani na mpira na kupigiana vipasi vifupi vifupi. Hizi back pass na square pass wanaziweza tu Barcelona kwa sababu wao wanazipiga na timu ina move mbele sasa Simba wanazipiga halafu timu bado ipo inazunguka kwenye eneo lao. Ndio maana wakikutana na timu inayokabia kwa juu wanateseka sana.

Ukiacha Libase, Oura, Chama, Kapombe, Kibabage na Mpanzu wachezaji wote waliobaki wao kazi yao kubwa wakipata mpira kitu cha kwanza ni kugeukia nyuma kwenye lango lao hata kama wapo katikati ya uwanja au hata karibu na lango la adui.

Mwisho ushauri wa bure kwa benchi la ufundi la Simba. Wafundisheni wachezaji wenu counter attack. Simba imeshambuliwa halafu wamepoka mpira eti mchezaji anapooza kwanza wenzake wapate nafasi waanze taratibu nyuma kwenda mbele wakati mshambuliaji wao alikuwa amebakia na beki mmoja tu kule mbele au ameshafungua pembeni. Pia wachezaji wajifunze kuwa sharp kwenye kuanza faulo na mipira ya kurusha. Sio lazima mpira urushwe na beki wakati mshambuliaji yupo karibu na mwenzake anaomba mpira kwenye nafasi.

Ni mtizamo tu.
 
Timu inafundishwa kwamba inapaswa kubadirika , inatakiwa kureact haraka kwenye matukio na kushambulia kwa haraka mbele na kuzuia haraka pia...... Nimependa walivyocheza might wonderers sijui hao .......kuna kitu wanawafundisha Simba sema sijui kama wanaona hili .....same to Gaborone,Yanga etc
 
Mkuu Simba inabadilisha wachezaji na makocha lakini mfumo wao wa uchezaji haubadiliki. Mwaka wa nne sasa back pass na square pass za kutosha timu haisogei mbele kwa haraka. Wamegoma kabisa kubadilika. Timu inacheza kama keep left. Mpira unazunguuka kwa kipa, mabeki wa kati, mabeki wa pembeni na kiungo wa chini muda mwingi wa mchezo hata kama inakutana Kilimanjaro Wonders!!!

Steve barker na benchi lake walipofika walijitahidi kubadilisha huo mfumo na kiasi fulani walifanikiwa. Lakini sasa hivi naona na wao wamechoka wamebaki tu kukodoa macho pale kwenye benchi siku ziende waondoke. Maana hawaoni kama kuna dalili za mafanikio mbele ya safari hasa baada ya kusubiri mshambuliaji wa maana wakaletewa Doumbia.
 
Ni sahihi mkuu..
Na huu mfumo wao hata mimi kiukweli siupendi sana maana timu inasomwa kirahisi sana na ikikutana na timu ina watu wa mbele wenye quality wanaiumiza...
Kinachonichosha ...usajili wa mwaka huu ukimtoa Jabir ...wengine wameshindwa kupenya kikosi cha kwanza .....sasa hali ingekuaje kama Oura na libase wangeuzwa kama ilivyokua inasemekana ? ......ingekua huzuni .....maana ndo silaha za mwalimu so far..
 
Ukiacha Libase, Oura, Chama, Kapombe, Kibabage na Mpanzu wachezaji wote waliobaki wao kazi yao kubwa wakipata mpira kitu cha kwanza ni kugeukia nyuma kwenye lango lao hata kama wapo katikati ya uwanja au hata karibu na lango la adui.
ASANTE
 
Hiyo ndio imekua style ya uchezaji wa timu yangu pendwa kwa muda sasa tena hasa ikiwa katika majukumu ya kimataifa

Tunahitaji wachezaji wenye ubora zaidi wenye uwezo wa kuifikisha timu mbali
 
Hongera Simba kwa kupata ushindi lakini wachezaji na benchi la ufundi walikuwa na makosa mengi sana kiasi iwapo leo wangekutana na timu nzuri ingewagharimu sana. Kwa mechi ya leo ingekuwa ile Simba ya akina Bocco, Kagere, Chama na wengineo sasa hivi wangekuwa wameshajihahkikishia kusonga mbele. Ila Simba hii tia maji tia maji inajichelewesha yenyewe.

1. Kasali ana foot work mbovu sana lakini anajiamini balaa na chenga yake inatabarika. Ni basi tu ana bahati sio kwenye ligi ya ndani au kimataifa mpaka sasa hajatokea mchezaji wa kuweza kumsoma. Arudi akaangalie baada ya Roger Milla kumsoma Rene Higuitta nini kilitokea. Pia tabia yeke ya kupiga pasi usawa wa kati kati ya goli badala ya pembeni siku sio nyingi atatoa mlio.
2. Mligo naye ni mzigo tu. Huu msimu wa pili kwake lakini bado habadiliki kabisa. Anachojua yeye akipata mpira ni kuwapasia mabeki wake wakati au kiungo mkabaji basi kashamaliza kazi. Kuna muda anapata mpira mbele yake kuna nafasi wazi lakini hatembei kabisa na mpira kuisogeza timu juu. Kibabage sio mzuri sana lakini huwa ana take risk kwenda mbele kusaidia kuipush timu izidi kusogelea lango la adui.
3. Jabaar, Maema na Kagoma wote walikuwa wanacheza chini muda mwing wa mchezo kiasi ikawa shida kwa Simba kupeleka mashambulizi mbele. Mpaka Chama alipoingia ndio walau timu ilianza kusogea mbele.
4. Benchi la ufundi limezingua sana kwa sub ya Mpanzu. Doumbia alipoingia aliwaacha wale mabeki wa kati wa timu pinzani wafanya wanavyotaka kuanzisha mashambulizi kwa sababu walikuwa hawana mtu wa kuwakaba kama alivyokuwa Mpanzu mwanzoni mwa mchezo. Doumbia tatizo lake kubwa hajui kuwa yeye ni mtu wa mwisho anatakiwa asimame na wale mabeki wakati ili wasianzishe mashambulizi na hata ikitokea wamefanya makosa yeye afunge. Badala yake anarudi chini sana na kuwaacha mabeki wa timu pinzani watengeneze mashambulizi kuanzia nyuma.
5. Ni wakati sasa wa viongozi wa Simba kuwaeleza aina ya mkataba alionao Doumbia maana lazima acheze kila mechi wakati akiingia kazi yake kubwa ni kuanguka anguka, kukaba wenzake na kuzuia pasi zisiwafikie wachezajia wenzake. Ni kama vile Doumbia ana mkataba kama aliokuwa nao Saidoo Ntibazonkiza kila mechi lazima acheze.
6. De Reuck ni bonge la beki. Lakini ule upuuzi wake wa kukaa na mpira muda mrefu halafu anaanza kutembea nao anachelewesha sana mashambulizi na inawafanya timu pinzani ijipange. Sio kila mpira lazima uanze kwa build up kuanzia nyuma.
7. Kocha wa viungo hapo Simba aangaliwe vizuri. Timu haina utimamu kabisa wa mwili na hasa dakika za mwishoni timu inapoteana sana wachezaji wanabaki wanakaba kwa macho. Kama wamalawi wangekuwa makini leo kuna aibu ilikuwa inaenda kutoea dakika za mwishoni

Benchi la ufundi la Simba lazima libadilishe mfumo wa uchezaji. Haiwezekani timu inafika kwenye robo ya tatu ya uwanja halafu mpira unarudishwa nyuma. Ndio maana ushindi wa Simba siku zoteunakuwa wa shida sana na akishinda goli nyingi sana ni mbili hata kama wana uwezo wa kuipiga hiyo timu goli kumi. Na hapo utakuta viongozi, benchi la ufundi na wachezaji wanaridhika kabisa. Wachazeji wanaanza kutembea uwanjani na mpira na kupigiana vipasi vifupi vifupi. Hizi back pass na square pass wanaziweza tu Barcelona kwa sababu wao wanazipiga na timu ina move mbele sasa Simba wanazipiga halafu timu bado ipo inazunguka kwenye eneo lao. Ndio maana wakikutana na timu inayokabia kwa juu wanateseka sana.

Ukiacha Libase, Oura, Chama, Kapombe, Kibabage na Mpanzu wachezaji wote waliobaki wao kazi yao kubwa wakipata mpira kitu cha kwanza ni kugeukia nyuma kwenye lango lao hata kama wapo katikati ya uwanja au hata karibu na lango la adui.

Mwisho ushauri wa bure kwa benchi la ufundi la Simba. Wafundisheni wachezaji wenu counter attack. Simba imeshambuliwa halafu wamepoka mpira eti mchezaji anapooza kwanza wenzake wapate nafasi waanze taratibu nyuma kwenda mbele wakati mshambuliaji wao alikuwa amebakia na beki mmoja tu kule mbele au ameshafungua pembeni. Pia wachezaji wajifunze kuwa sharp kwenye kuanza faulo na mipira ya kurusha. Sio lazima mpira urushwe na beki wakati mshambuliaji yupo karibu na mwenzake anaomba mpira kwenye nafasi.

Ni mtizamo tu.
Uko sahihi asilimia kubwa kocha aache undugu apange wachezaji kulingana na uwezo wao.
 
Tokea Wawa kaondoka Simba haijawahi kupata beki mwenye uwezo wa kupiga pasi mita 20+ kwa usahihi kwa winga au mshambuliaji. Toure alipokuja mwanzoni alikuwa anajitahidi sana kufanya hiyo kazi japo hakuwa sahihi sana kama Wawa. Ila sasa hivi na yeye kaingia kwenye mfumo wa kucheza rede. Sijui alikatazwa au na yeye kajikuta tu kaingia kwenye mfumo huo wa pasi fupi fupi aka rede.

Mwamba Kante naye alipofika alikuwa anaweza kupiga pasi ambazo zilikuwa zinakata safu mbili mpaka tatu za wachezaji wa timu pinzani. Tena Kante alikuwa ana risk kweli kweli maana alikuwa anapiga pasi za chini na zilikuwa zinafika. Na yeye baada ya kuzoea tu akaingia kwenye mfumo wa kucheza rede na hapo ndipo alipopotea kabisa mpaka akawa kituko. Na hakuna aliyemshtua arudi kwenye aina yake ya uchezaji mpaka kaondoka Simba huku mashabiki wanaona sawa tu aondoke.

Kwa sasa viungo waliopo pale Simba karibu wote ni wa pasi fupi fupi kiasi timu haitembei kwa haraka wakati timu ina wachezaji wanne wenye kasi sana Mpanzu, Oura, Libase na Kaletso. Na mbaya zaidi viungo wote ukimuacha Chama wanaaangalia chini na kugeukia nyuma muda mwingi wa mchezo. Kwa kifupi Simba imeshindwa kunufaika na kasi ya mawinga wake.

Ni mtizamo tu.
 
Back
Top Bottom