Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Morocco naona anafunzu kwenda hatua ya 32 bora ya Kombe la dunia 2026, labda wajisaliti wenyewe
=======
Suluhi ya 1-1 ambayo Morocco walipata dhidi ya Brazil kwenye mchezo wa kwanza inamaanisha kuwa kinara wa Kundi C anaweza kupatikana kwa kuangalia idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa (goal difference), endapo timu zote mbili zitashinda michezo yao ya mwisho ya makundi.
Hii ina maana kwamba Morocco hawawezi kabisa kulemba, kubweteka au kuingia uwanjani wakiwa wameregea dhidi ya Haiti. Wanahitaji kushinda, na ikiwezekana, washinde kwa idadi kubwa ya mabao ili kujihakikishia nafasi ya kwanza ikiwa Brazil nao watashinda mechi yao dhidi ya Scotland.

Historia ya Timu Hizi Kukutana (Head-to-Head)
Hii itakuwa mara ya kwanza kabisa kwa timu hizi kukutana ana kwa ana katika historia yao.- Morocco: Mchezo wao pekee wa Kombe la Dunia dhidi ya timu kutoka ukanda wa CONCACAF (Amerika Kaskazini, Kati na Karibiani) ulikuwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Canada katika hatua ya makundi mwaka 2022.
- Haiti: Mchezo wao pekee dhidi ya timu kutoka barani Afrika katika kipindi cha muongo mmoja uliopita ulikuwa ni ule wa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Tunisia mnamo mwezi Machi.