Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,267
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom Premier League VPL' kuvurumishwa leo Jumamosi Mei 29, 2021 ambapo Namungo FC wakiwa dimba lao la nyumbani kuwakabili Mabingwa Watetezi Mnyama Mkali Simba SC.
Mchezo huu VPL ni wa kiporo kutokana na timu ya Namungo FC na Simba SC kukabiliwa na kuwakilisha nchi katika michuano ya Kimataifa hivyo mchezo huu huenda ukawa mkali sana kwa muda wote wa dakika 90.
Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10: 00. Jioni. Usikose Ukasimuliwa
Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
=========
Wakati wowote mpira utaanza Uwanja wa Majaliwa.
Ni Vita kuwania alama tatu muhimu katika VPL.
00' Naaaam mpira umeanza, Namungo FC wakianza kusukuma gozi la Ng'ombe.
15' Hakuna timu imeona lango mwenzake huku mashambulizi yakiendelea kusaka bao kwa pande zote | Namungo FC 0-0 Simba SC.
22' Goooooooooaaal Gooooaaaaal
Nzigamasabo anawatanguliza Namungo FC kwa bao la kwanza akipokea pasi ya Lusajo | Namungo FC 1-0 Simba SC.
40' Namungo FC wanatibua mipango ya Simba kupata bao la kusawazisha ambapo Kagere na Mugalu wanashindwa kupenya gome ya Namungo.
45+2' Kuelekea kuwa mapumziko ambapo Namungo wapo mbele kwa bao moja kwa bila, mchezo ni wa ushindani na maarifa pia.
Naaaam mpira ni mapumziko Majaliwa Stadium | HT, VPL Namungo FC 1-0 Simba SC
Kipindi cha pili kimeanza huku Simba wakifanya mabadiliko. Ametoka Mzamir na ameingia Bernard Morrison.
55' Anakwendaa Mugalu anampasia Kagereeeee loooooo, anakosa nafasi ya wazi, ilikuwa nafasi nzuri kwa kusawazisha. Na salama lango la Namungo.
Ametoka Kagere na ameingia Bocco upande wa Simba SC huku akiingia Sey na ametoka Ibrahim upande wa Namungo FC.
Mchezo ni maarifa sana huku Simba wakimiliki na kutafuta bao kusawazisha, mabeki wa Namungo FC wamekaza.
78' Mugalu Goooooooooaaal Goooooooaaal
Chris Kope Mutshimba Mugalu anaisawazishia Simba SC bao akipokea pasi kutoka kwa Kapombe | Namungo FC 1-1 Simba SC.
Simba SC wanashambulia kujaribu kupata ushindi, Kocha Gomes anawacheki tu Namungo FC je wataweza kuinyima ushindi Simba SC.
Mashambulizi makali mno kuelekea upande wa Namungo.. anakwendaa sasa kwake Mugalu kwake Bocoo
83' Goooooooooaaal Goooooooaaal
John Bocco anaipatia Simba SC bao la pili kwa kichwa safi akipokea pasi kutoka kwa Mugalu..| Namungo FC 1-2 Simba SC
Namungo wanasakwa kila upande, mabadiliko yaliyofanywa na Kocha Gomes yanaipa uhai sana Simba SC upande wa mashambulizi, Namungo wameshikwa hasa kipindi hiki kuelekea kumalizika kwa mchezo.
87'Mpira upo katikati ya Uwanja Simba wanamiliki.... Kwake Bernard Morrison anapigaaaa Goooooooooaaal Goooooooaaal
Morrison anaipatia Simba SC bao la tatu kwa shutiiiiii kali la mbali sana, na kumuacha golikipa Nahimana akiruka bila mafanikio.
Namungo FC 1-3 Simba SC.
90+2' Kuelekea kumalizika kwa mchezo wa VPL Simba SC wapo mbele kwa mabao matatu kwa moja dhidi ya Namungo FC.
Naaaam mpira umekwishaaa | FT, VPL | Namungo FC 1-3 Simba SC
....... Ghazwat