FT: NBC Premier League | Simba SC 2- 0 Kagera Sugar | Uwanja wa Benjamin Mkapa

Halafu niwatakie usiku mwema. Ila tu nawakumbusha watu kumtimiza ahadi yake Mayele ya ng'ombe wake wawili wa maziwa. Mtakosa ubingwa kimasihara jamaa atakuwa anapaisha tu mipira kuelekea Kizota.
 
Ngoja kwanza waendelee kuchukua ka point kamoja kamoja kama wanaokota shanga

Jumapili wanakutana na mbeya kwanza ambao ndio wa mwisho kwenye msimamo

Na hiyo ni moja ya mechi muhimu kwa mbeya kwanza ambayo ipo kwenye mahesabu yao kwasababu point tatu zinawatosha wao kupanda nafasi tatu xa juu.

Sidhani kama itakuwa tayari kupokea bahasha kwa hali waliyokuwa nayo
 
Sisi pia tunazihitaji hizo points
 
Halafu huyu Kagera kwanini asishule daraja tu... maana hata kumfuata huko kwao kucheza nae ni kama unaenda Afrika Magharibi kwa Asec.

Halafu akiwa kwao anakuwa mgumu kweli
Hata mechi hii ilikua ngumu
Goli lenu la kwanza ni uzembe wa kipa au labda alisharushiwa muamala..maana mpira unapita mbele yake taratibu anauangalia tu

Goli lenu la pi ni clear off side

Kwa umiliki mzuri waliokua nao kagera na leo pia mlikua mbalala,juhudi zenu za nje ya uwanja zimewabeba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…