Wakuu leo mechi nane zitapigwa za NBC Premeir league lakini Jambo kubwa ni kati ya Yanga dhidi ya Azam FC. Je, Yanga wataweza kujishikilia dhidi ya utofauti wa point mbili kati yake na Mnyama Simba.
Ikumbukwe Yanga ana majeraha baada ya kipigo kitakatafu dhidi ya Azam hao hao kwenye kombe la CRDB shirikisho. Hii inamaanisha bado hajapona majeraha.
Mechi nyingine ni;
Mechi za leo pia ni pamoja na
Dodoma Jiji Vs JKT Tanzania
Mtibwa Vs Simba
TRA United Vs Coastal Union
Fountain Gate Vs Mashujaa
Pamba Jiji Vs Mbeya City
Singida Bs Vs Tanzania Prisons
KMC FC Vs Namungo
Baada ya mechi za msimu kumalizika yanga inabidi ifanye usajili wenye tija. Wachezaji wengi wameizoa timu na wanacheza kwa mazoea sana. Ubunifu na kujituma vimepungua sana kwa wachezji wengi wa Yanga. Pia kuna wachezaji mizigo hasa hawa waliosajiliwa hvi karibuni kama Depu na Damaro.
Yanga imeonesha ina ufinyu wa wachezaji wenye ubora ukiachana na wanaonza kikosi cha kwanza basi benchi hakuna wachezaji wa maana wa kuweza kubadilisha mchezo. Azam wamefanya sub nyingi na kuielemea Yanga iliyokata moto kipindi cha pili.
Ni uthibitisho tosha kuwa Hersi kuvurunda usajili msimu huu