FT: Niger 0-1 Tanzania. Kufuzu Kombe la Dunia. Novemba 18, 2023

Leo Yanga imecheza na Niger...?
Ni hesabu ndogo tu Yanga iliweka kikosini wachezaji 3 na Simba 1 Taifa Stars ikashinda nikasema ndo maana Simba walipigwa khamsa 5G🤪

Manula aliekula 5G Leo alikuwa likizo kwa ukuta wa Berlin wa Yanga kumlinda na kumuepusha na tuhuma za Mbumbumbu za kuuza mechi!!
 
Taifa stars hawatii moyo kabisa kuwatazama, hapa usilaumu watu wakulaumiwa ni tff kushindwa kua na mipango ya kueleweka. mwisho wake timu imepoteza mvuto.
Hiyo siyo ligi,ugenini unavizia walau point,siyo unakimbia tu Kama kuku alokatwa kichwa
 
Huyu haji Mnoga anakimbiakimbia na kuanguka hovyo Kama mtoto hajui Hata kukwepa poor stamina poor fitness inamfanya Achoke hoi Kama amekimbia maili 300!
Amemuangukia Job na kumuumiza bila sababu yoyote .
Shauri ngozi nyeupe ndiyo maana kocha anampanga lakini Kiwango kidogo kuliko wachezaji wa ligi ya Tanzania , nafuu Hata wachezaji wa Ihefu au kmc .
Inasemekana anachezea timu ya daraja la nne huko England .
Fei Toto mzito amenenepa hana speed na uchu wa mashambulizi na mashuti kama zamani
 
Acheni usimba na Yanga Kuna mchezaji yupi Kwa Sasa anamzidi Mnonga

Sent from my TECNO BF7 using JamiiForums mobile app
 
Pamoja na ushindi lakini hiyo timu inasikitisha sana kuna watu humo ndani ni viande kichizi yani hakuna mahali itafika inakatisha tamaa sana kuna wachezaji najiuliza walifikaje huko walipo

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Kina Ashraf Hakim, wameshafika Dar tayari
Tukiongeza mazoezi ya pumzi na kukaba tukashikilia bomba hatufungwi na Morocco, ila tukifunguka tutapigwa nyingi. Lazima tuwaheshimu, faulo nje ya box hazitakiwi kabisa. Hawa mpira wao kama waarabu wengine hawana jipya na hawajui tunachezaje itatubeba!

Feisal bado sio yule, hivi sasa ni mzito sana muda wote anawaza kurudisha mipira nyuma sijui mbele anaogopa nini , mechi ya Morocco inamhitaji Mudathir tu katikati.

Samatta aache utozi, goli alilokosa akiwa yeye na kipa ni la kijinga kabisa, ila bado ni tegemeo letu mpira anaujua na amebadilika hivi sasa anakaba sana na kusaidia sana timu kule mbele. Kipa wa Niger alisumbuliwa sana na Samatta big up!

Ushindi dhidi ya Morocco pia upo tukitulia mwarabu anakaa tu kwa Mkapa hatoki Mtu, namuona Msuva akipiga goli mbili safi. Point 3 za Morocco tuzipambanie zitatubeba sana. Hii timu iko vizuri sana kushikilia bomba lazima tuseme ukweli
 
Pamoja na ushindi lakini hiyo timu inasikitisha sana kuna watu humo ndani ni viande kichizi yani hakuna mahali itafika inakatisha tamaa sana kuna wachezaji najiuliza walifikaje huko walipo

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Hii ni timu ya Taifa kaka, hatuwezi kusajili twende nao hivo hivo.
 
Tupo kundi moja na DRC?
 
Haiwezekani. Yaani ili mchezaji akue anahitaji mechi mara kwa mara. Karibu kila week. Tena sio mechi tu. Mechi zenye ushindani. Sasa team etinikae tu ikisubiri game za kimataifa. Mtakuwa mnakula khamsa kila game.😅

Kwa kifupi hakuna kitu kama hicho kokote duniani.
 
Wewe hizi taarifa za best loser umezitolea wapi? Africa tunapeleka timu 6 tu na makundi yapo 6 tu.
 
Team yake mama ni potmouth iko league one England. Daraja la tatu.
Kapelekwa kwa mkopo. National league (daraja la nne) team ya Aldershot.
 
Kuna huyu beki wa kati kati sijui anaitwa nani yaani garasa tupu bute kabisaa kampasia mpira adui ndani ya box pia anachojua yeye ni kirudisha mpira kwa kipa kidogo achomeshe mara nne
haji mnoga,ni mchezaji mzuri sana ni makosa tu ya kimchezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…