FT: Niger 0-1 Tanzania. Kufuzu Kombe la Dunia. Novemba 18, 2023

Naona uzi umepoooa na hiyo yote ni kwa sababu taifa stars amecheza ila zingekuwa timu zenu za kariakoo huu uzi ungekuwa na wachangiaji 1000+

Anyway ila ni vyema mjifunze kuupenda mpira kwanza kabla ya kupenda timu zenu za kkoo

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Taifa stars hawatii moyo kabisa kuwatazama, hapa usilaumu watu wakulaumiwa ni tff kushindwa kua na mipango ya kueleweka. mwisho wake timu imepoteza mvuto.
 
Ukuta wa Berlin wa Yanga umeonesha kiwango Cha juu Manula Yuko likizo Leo zile 5G kumbe ni beki mbovu

Timu ilikosa muunganiko wa katikati na mbele, viungo Wote watatu Fei, Mnoga na Bajana walikaba zaidi na kusahau kupandisha timu.

Timu iliishiwa pumzi dakika 20 za mwisho ikawa roho mkononi hivyo wafanye mazoezi sana ya mbio na fitness gym , Morocco sio Niger wasijetuaibisha 5G kwa Mkapa!

Ila timu yetu imekaba vizuri, ila nawapongeza sana Mbwana Samata na Simon Msuva kwa kujituma sana kukaba mwanzo mwisho kuliko wachezaji wengine , big up sana mmeonesha mfano wa kuigwa.

Manula na Mwamnyeto Kuna mpira walitegeana jamaa wa Niger akawa anaenda kufunga ila Nondo akawahi kuokoa Boko lake Hili wasirudie, waongee!!

Novatus ni majeruhi wamtibu haraka Leo alihangaika na msuli wa paja mara kwa mara kacheza kwa uzoefu tu Kuna saa alichuchumaa ikawa anacheki kama anaweza kuendelea.

Samatta alikuwa wa moto sana ila viungo hawakumlisha mipira vizuri Mudathir acheze next match japo kipindi kimoja.

Morocco tuwachezee kama jinsi tulicheza na Algeria timu nzima ikabe kwa nguvu kwa dakika 90 hatufungwi.

Otherwise hongera sana Taifa Stars jezi ya njano na blue inatubeba sana!
 
Wakuu hivi haiwezekani kuwe na timu ya taifa ambayo haitokani na wachezaji wa kwenye vilabu tofauti ili kuwe na mda wa kutosha wa kujiandaa,au club iitwe taifa stars inashiriki ligi pia ila wachezaji wa ndani tupu na gharama ya kuendesha itoke kwa TFF au wamtafute mdhamini, labda tutatoboa, kuliko kuleta sura jipya kila mechi
Huna akili mkuu
 
Kwa jinsi alivyopokea Ile pasi na ku dribble nikajua huyu hachezi soka Tanzania
Maji na mafuta hujitenga, mchezaji wa kibongo utamjua na wa mbele utamjua tu.

Kuna faida kubwa ya wachezaji kucheza nje ya nchi. Viwanja vyetu vingi vya ndani, nature ya wapinzani NBC pira papatu papatu kwa kiasi fulani halikwepeki.
 
tatizo huwa linaanza hapa mnaleta siasi kwenye mambo yanayotaka sayansi nasio porojo.
Kama ni siasa michezoni zimeletwa na hao hao waliopo madarakani, mambo ya sayansi michezoni yanahitaji kizazi kingine na sio kizazi hiki cha kununua magoli.
 
Ukuta wa Berlin wa Yanga umeonesha kiwango Cha juu Manula Yuko likizo Leo zile 5G kumbe ni beki mbovu

Timu ilikosa muunganiko wa katikati na mbele, viungo Wote watatu Fei, Mnoga na Bajana walikaba zaidi na kusahau kupandisha timu.

Timu iliishiwa pumzi dakika 20 za mwisho ikawa roho mkononi hivyo wafanye mazoezi sana ya mbio na fitness gym , Morocco sio Niger wasijetuaibisha 5G kwa Mkapa!

Ila timu yetu imekaba vizuri, ila nawapongeza sana Mbwana Samata na Simon Msuva kwa kujituma sana kukaba mwanzo mwisho kuliko wachezaji wengine , big up sana mmeonesha mfano wa kuigwa.

Manula na Mwamnyeto Kuna mpira walitegeana jamaa wa Niger akawa anaenda kufunga ila Nondo akawahi kuokoa Boko lake Hili wasirudie, waongee!!

Novatus ni majeruhi wamtibu haraka Leo alihangaika na msuli wa paja mara kwa mara kacheza kwa uzoefu tu Kuna saa alichuchumaa ikawa anacheki kama anaweza kuendelea.

Samatta alikuwa wa moto sana ila viungo hawakumlisha mipira vizuri Mudathir acheze next match japo kipindi kimoja.

Morocco tuwachezee kama jinsi tulicheza na Algeria timu nzima ikabe kwa nguvu kwa dakika 90 hatufungwi.

Otherwise hongera sana Taifa Stars jezi ya njano na blue inatubeba sana!
Leo Yanga imecheza na Niger...?
 
Back
Top Bottom