FT: Nyasa Big Bullets 0-2 Simba | CAF Champions League (CAFCL) | Bingu Stadium

FT: Nyasa Big Bullets 0-2 Simba | CAF Champions League (CAFCL) | Bingu Stadium

Mchezo umeanza

Timu zimeshaingia uwanjani kuelekea kuanza kwa mchezo huu

Kikosi cha Nyasa Big Bullets

Kikosi cha Simba kuelekea mchezo dhidi ya Nyasa Big Bullets, leo Jumamosi Septemba 10, 2022, unatarajiwa kuanza saa 10:00 Jioni kwa Tanzania.


Klabu ya Wekundu wa Msimbazi, Simba SC, wapo ugenini wakitarajia kushuka katika Dimba la Bingu National Stadium nchini Malawi kukinukisha dhidi ya wenyeji Nyasa Big Bullets katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo unategemewa kuwa wa ushindani ndani ya dimba ambapo Nyasa Big Bullets ni timu ambayo ina wachezaji wenye uwezo kuuchezea mpira miguuni hivyo si timu rahisi, hivyo unatakiwa uwe umejiandaa vilivyo kuchuana nao.

Hivyo basi tunatarajia kuona burudani ya kukonga nyoyo, ambapo Simba SC wakiwa na wachezaji wao mahiri wenye vipaji na experience kubwa kwenye michuano mbalimbali ya CAF watakavyoingia na mbinu ngumu ya kuhakikisha wenyeji wanakuwa na wakati mgumu muda wote wa mchezo.

Kwa yote haya ni ndani ya kuamua...Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10:00 Alasiri..Usikose Ukapata Simulizi..Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

Karibu Jopo Zima la Lunyasi Mwifwa, OKW BOBAN SUNZU, Scars, Kinyungu, denooJ, Kalpana, Shunie, Mshana Jr, BRN, Mawawa, mpiga vichwa, koboG, Waminyato, Pettymagambo, SAGAI GALGANO, Troisième Ceil, 3ZOV, Proved, mkwepu jr, Satoh Hirosh, Elli, MTAZAMO, Designer_3434, TUJITEGEMEE, Mac Alpho, Kiweriweri, Donnie Charlie, CHIEF PRIEST, rodrick alexander, Chaliifrancisco, Mtoto halali na hela. Na wengine wana Lunyasi [emoji881][emoji881][emoji881] Nguvu Moja

===========

Vikosi vyote vya Nyasa Big Bullets na Simba SC vimefika katika Dimba la Bingu National Stadium [emoji2522] tayari kwa mchezo.


00' Naaam mpira umeanza Uwanja wa Bingu National Stadium | Nyasa Big Bullets 0-0 Simba SC

05' Mpira umeanza kwa taratibu huku kila timu ikimsoma mpinzani wake.

08' Simba wamemiliki mpira kwa dakika hizi za mwanzo huku wakipata Free Kick na Kona ambazo hazikuzaa mabao.

10' Nyasa wanakosa nafasi ya wazi ya kufunga bao kupitia Babatunde, ilikuwa hatari langoni kwa Simba

15' Timu zinaendelea kusaka ushindi kwa umakini.

20' Hussein anapiga shutii lakini mpira unatoka nje na kuwa goal kick

26' Sakho anaachia Krosi lakini Kibu anachelewa na mpira kuokolewa na mabeki wa Nyasa

29' Phiri Goooooooooooooaaal gooal

Moses Phiri anahesabu bao la kwanza kwa tikitaka | Nyasa Big Bullets 0-1 Simba SC

Simba watandaza Kabumbu, Nyasa wanautafuta mpira dakika hizi, Sakho anapiga Krosi inaambaa kule

39' Nyasa wanafanya mabadiliko, Kajoke ameingia kuchukua nafasi ya Nkhome

42' Phiri yupo chini akipatiwa matibabu, ameinuka mpira unaendelea, Simba bado wana Umiliki wa mpira.

45+2 kuelekea kuwa mapumziko

Anakwenda kwake Sakho, wanachukua Nyasa wanapiga mbele kule lakini golikipa Manula anadaka.

Naaam mpira ni mapumziko ambapo Simba SC wapo mbele kwa bao moja dhidi ya Nyasa Big Bullets

HT: Nyasa Big Bullets 0-1 Simba SC

Kipindi cha pili kimeanza kwa kasi kidogo, huku kila timu ikipoteza nafasi za kufunga bao.

50' Shutii la Phiri inatoka linapaa nje ya lango la Nyasa, ilikuwa nafasi nzuri

55' Nyasa wanapiga mbele kumtafuta Chirwa, lakini Ouattara anakataa maridadi kabisa

60' Idana anakosa nafasi nzuri ya kufunga ilikuwa Shambulizi kali kuelekea lango la Simba, golikipa Manula anadaka shuti lile.

62' Ametoka Kibu na Kanoute na wameingia Banda na Nyoni.

70' Nyssa wameamka sasa, unapigwa mpira mbele kuleee, lakini Israel anaokoa.

Ameingia Kabechi kuchukua nafasi ya mtu upande wa Nyasa Big Bullets

Ameingia Bocco, ametoka Phiri upande wa Simba SC

75' Nyasa wanakosa nafasi ya kufunga bao, ilikuwa nafasi ya kusawazisha, Manula anasema namna hapa

78' Wanakosa bao Nyasa Sambani anashindwa kuunganisha free kick ya Kabichi | Nyasa 0-1 Simba

81' Bocco anapiga kichwa lakini golikipa Chimbamba anatoka na kudaka

84' Bocco Goooooooooooooaaal gooal

John Bocco anaweka kambani bao la pili akipokea pasi murua kutoka kwa Chama | Nyasa Big Bullets 0-2 Simba SC

Nyasa wanapiga mbele lakini golikipa Manula yupo imaraimara

Ametoka Sakho ameingia Okrah upande wa Simba

90+4' Kuelekea kumalizika kwa mchezo Simba wakitawala mchezo



Matumaini ya Nyasa Big Bullets kupata ushindi yanafifia hapa, Mnyama yupo mbele ya mabao mawili.

Free Kick kuelekea Simba, unapigwa mpira mrefu lakini unatoka nje na kuwa goal kick

Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba SC wanaibuka na ushindi wa mabao mawili kwa bila dhidi ya Nyasa Big Bullets.

FT: Nyasa Big Bullets 0-2 Simba SC

..... Ghazwat....
giphy.gif
 
Sio kweli mimi ningekuwa kocha nisingempanga bocco,nyoni wala israel,hixo ingeathiri matokeo
Ile Sub ya Nyoni na Bocco ilileta wasiwasi kidogo japo imelipa kwa Bocco kuweka kambani bao la pili
 
Back
Top Bottom