FT: Simba 0-1 Al Ahly | CAF CL Robo Fainali | Benjamin Mkapa Stadium | 29/03/2024

FT: Simba 0-1 Al Ahly | CAF CL Robo Fainali | Benjamin Mkapa Stadium | 29/03/2024

Friends of All Ahly tumeshamaliza Kazi yetu na sasa tunabadili uraia na kuwa Friends of mamelod
 
Hii Mechi bado mbichi.....

Zilizomalizika ni Dk. 90 , bado Zingine 90... !

Man of the Match Wao kipa Kawaokoa Leo, Sidhani kama ataendelea kuwa na bahati Second Leg....!

Kwaiyo Utopolo msifosi tufa8....
Acha kujipa matumaini, hatuna mchezaji wa kufunga goli zaid ya kanoute kwenye mipira iliyokufa basi, kwaiyo usitegemee chochote kwenye mechi ya marudiano wakati hatuna mchezaj wa kufunga goli
 
Ila hawa wasemaji pamoja na kuhamasisha ila wanachangia pakubwa kutuaminisha ujinga

Ukisikiliza tambo za Ahmed Ally na kilichofanyika uwanjani ni mbingu na aridhi [emoji23]

Ngoja tusubiri na kesho Yanga
Sasa ulitaka Ahmed au ali kamwe wafunge zile nafas za kina saidoo na wengine walizokosa[emoji16]
 
Leo mnamo majira ya saa 3 usiku Klabu ya Tanzania Simba Sports Club itakuwa nyumbani kumenyana na klabu ya Al Ahly ya Misri katika mechi ya mkondo wa kwanza (First Leg) wa robo fainali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Maandalizi ya timu zote mbili yameenda vyema, kinachosubiriwa ni mchezo rasmi leo 29/03/2024 saa tatu usiku.

Ungana nami katika uzi huu ili kupata matukio mbalimbali yatakayojiri kabla na wakati wa mchezo huo.

Karibu.


==============

Timu ya Simba inatarajia kucheza dhidi ya Al Ahly ya Misri katika Robo Fainali ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, leo Machi 29, 2024

Takwimu zinaonesha hakuna mbabe mpaka sasa, kila upande umeshinda mechi Tatu, hizi ni mechi zilizopita baina ya timu hizo:

24/10/2023 Al-Ahly 1-1 Simba

20/10/2023 Simba 2-2 Egypt

09/04/2021 Al-Ahly 1-0 Simba

23/02/2021 Simba 1-0 Al-Ahly

12/02/2019 Simba 1-0 Al-Ahly

02/02/2019 Al-Ahly 5-0 Simba

29/08/1985 Al-Ahly 2-0 Simba

22/08/1985 Simba 2-1 Al-Ahly
---
View attachment 2948421
Kikosi cha Simba kilichoanza
View attachment 2948432
Kikosi cha Al Ahly kinachoanza

Mchezo umeanza
3' Simba wameanza wakiwa na presha ya kushambulia, wamepata kona
5' Gooooooo Al Ahly wanapata goli baada ya safi ya ulinzi ya Simba kujichanganya
11' Kasi ya Mchezo imepungua, AlAhly wanalinda lango lao muda mwingi
13' Simba Wana Kona tatu, wageni Wana Moja
16' Al Ahly wanapata Kona ya pili na ya tatu ndani ya dakika moja
21' Al Ahly wanafanya mashambulizi ya kushtukiza na yanakuwa hatari
30' Mapumziko ya dakika moja
32' Mchezo unaendelea
40' Saido anakosa nafasi ya wazi
45 ' Mapumziko, Simba wapo nyuma kwa goli 1-0.

MAPUMZIKO

Kipindi cha pili kimeanza
49' Babacar anapata kadi ya njiano kwa kucheza faulo
55' Inonga anapata kadi ya njano kwa kucheza faulo
60' Mchezo bado ni mgumu kwa Simba wanatengenesa nafasi lakini haizitumiki vizuri
70' Simba wanaendelea kumiliki mpira lakini nafasi ya kufunga bado ni ngumu
75' Mapumziko ya dakika moja kwa timu zote.
77' Saido anapat nafasi kadhaa za wazi lakini hazitumii vizuri
80' Simba wanaendelea kutengeneza nafasi lakini wanashindwa kuweka mpira wavuni
90' Zinaongezwa dakika 5
Full Time
KWISHA HABARI YAKE.....
 
Timu gani iliyoshangalia match ya Robo fainali club bingwa Africa kwa muda mfupi zaidi?
FB_IMG_17117484480032766.jpg
 
N


Ndio, uliza Zamalek aliyekuwa Bingwa mtetezi Wakati huo,alifanywa nini Cairo ..

Watu Wana Historia zao Bwana...!

Hakuna Kitu Simba Hajawaifanya....Labda kuleta Kombe tu
Mara 800 angekua Yanga Ila Simba hamna kitu anaenda kupigwa km Ngoma
 
Mkimfunga Mamelody nipigwe Ban angalau ya Siku mbili hivi au Wiki
Wewe nitashikiria Bango mpaka YinYang apite na wewe na Mamelodi leo anachinjwa hakuna janja janja moto ni ule ule kijani na njano ngoja mufundishwe jinsi ya kushinda nyumbani sio kushinda na njaa mnaishia kufungwa na wabeba mapipa
 
Back
Top Bottom