FT: Simba 0 - 1 Yanga | NBC Premier League | Benjamin Mkapa Stadium | Oktoba 19, 2024

FT: Simba 0 - 1 Yanga | NBC Premier League | Benjamin Mkapa Stadium | Oktoba 19, 2024

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Kariakoo Derby!

Simba Vs Yanga, mchezo wa kukata na shoka. Je, Simba atafuta Uteja wa kufungwa na Yanga mfululizo?

Kwa LigiKuu msimu huu, Simba imecheza michezo 5 ikikusanya alama 13 na Yanga michezo 4
ikikusanya alama 12.

Katika siku hizi za karibuni Yanga imeonekana kupata matokeo Chanya dhidi ya Simba na hii ni kutokana na Quality ya kikosi cha Yanga lakini haiondoi uhalisia kwamba Simba nao wana kikosi kizuri hasa msimu huu ambao wametamba Kusajili vizuri.

Mechi ni Saa 11:00 Jioni katika dimba la Benjamin Mkapa

Live kupitia Azam Sports 1HD, TBC Taifa kwa idhaa ya Radio.

Soma Pia: Refa wa Mechi ya Simba Vs Yanga ni Ramadhan Kayoko

IMG_4025.jpeg
IMG_4026.jpeg

===========================================
Updates:
1’ Yanga wanaanza mpira

4’ Mpira umeanza kwa kasi huku Yanga wakifanya faulo kadhaa kwa Simba

5’ Ateba akiwa yeye na kipa anapoteza nafasi ya kuipa uongozi Simba

10’ Simba 0-0 Yanga

12’ Simba wametawala mechi mpaka sasa huku Yanga wakiwa wanawasoma

15’ Yanga wanafanya shambulizi lakini ukuta wa Simba unakaa sawa na kuokoa hatari

20’ Simba 0-0 Yanga
Mvua imefanya uwanja usiwe vizuri leo

23’ Mpira ni 50/50 timu zote zinashambuliana kwa zamu

25’ Simba 0-0 Yanga

29’ Mechi imepoa bado timu zinaviziana huku zikicheza kwa tahadhari

33’ Mechi imekuwa ya mbinu nyingi sana bado 0-0

35’ Boka anapewa kadi ya njano baada ya kumchezea madhambi Ahoua

41’ Pinpin Camara anaokoa mkwaju uliopigwa langoni mwa Simba na Aziz Ki

45’ Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 3 zimeongezwa

45+2’ Jean Charles Ahoua anaonyeshwa kadi kwa mchezo usiokuwa wa kiungwana

HT’ Simba 0-0Yanga

45’ Kipindi cha pili kimeanza
Simba wamefanya mabadiliko, Okejepha ameingia na Yusuph Kagoma ameenda nje

47’ Dickson Job anapewa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Kibu D

48’ Goli la Kibu linakataliwa baada ya kuotea

50’ Hamza anapewa kadi ya njano kwa madhambi aliyomfanyia Dube

54’ Bacca anapewa kadi ya njano kwa faulo yake kwa Ahoua

60’ Simba 0-0 Yanga

62’ Yanga wanafanya mabadiliko
Dube na Pacome wanatoka huku Mzize na Musonda wakiingia

65’ Mchezo umesimama kupisha beki Hamza kutibiwa

68’ Simba wanafanya mabadiliko Hamza na Mutale wanatoka na nafasi zao kuchukua na Chamou na Balua

72’ Simba wanapata faulo nje, inapigwa na Ahoua lakini inadakwa na Diarra

75’ Yanga wanaongeza spidi kwenye mashambulizi lakini matokeo bado 0-0

79’ Aucho anapewa kadi ya njano baada ya faulo kwa Ahoua

83’ Chama anaingia kwa nafasi ya Aziz Ki

86’ Goaaaaaaaaaaaaallllllllllll
Kelvin Kijili anajifunga
Simba 0-1 Yanga

87’ Mukwala in, Kapombe Out

88’ Simba 0-1 Yanga

90’ Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 7 za nyongeza

FT’ Simba 0-1 Yanga
Kelvin Kijili akijifunga
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa.....

Baada ya kusubiri kwa miezi, wiki na siku kadhaa hatimaye leo miamba ya Soka la Tanzania Simba na Yanga wanakutana katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC (ukiwa ni mchezo namba 64 kwa mujibu wa ratiba ya TFF)

Mchezo huo utapigwa katika dimba la Benjamin Mkapa majira ya saa 11 kamili jioni

Mchezo wa kwanza msimu huu kukutana ni kwenye ufunguzi wa Ligi Kuu yaani Ngao ya jamii 8/8/2024 ambapo Yanga ilishinda bao 1 kwa sufuri

Kwa upande wa LigiKuu Simba imecheza michezo 5 ikikusanya alama 13 na Yanga michezo 4 ikikusanya alama 12


Katika siku hizi za karibuni Yanga imeonekana kupata matokeo Chanya dhidi ya Simba na hii ni kutokana na Quality ya kikosi cha Yanga lakini haiondoi uhalisia kwamba Simba nao wana kikosi kizuri hasa msimu huu ambao wametamba Kusajili vizuri

Je leo nani atatoka analia, anacheka au wote watatabasamu?
 
Back
Top Bottom