FT: Simba 1-0 Orlando Pirates | CAF CC quarter final | Benjamin Mkapa Stadium

Hivi mara ya mwisho Utopolo kuifunga timu ya nje ni lini ?

Na ilikuwa timu gani ?

Na kwanye mashindano gani ?

Goli la ushindi aliyefunga nani ?

NB
Hivi Utopolo ipo nafasi ya ngapi kwa ubora Africa ?
Unesahau waliwafunga Mabingwa wa Taleban
 
umejibu vyema na refa hakuona ulazima wa kwenda kuangalia kwa sababu wale waliokuwa studio baada ya kureview tukio wakaona ni penati na refa hakuwa na pingamizi nao kama wale jamaa wa studio wangemwambia sio penati basi refa lazima angeenda kuangalia kwenye screen VAR humsaidia tu refa kuona kwa vizuri na kujiridhisha tukio husika lakini refa ndiye mwenye maamuzi ya mwisho
 
Mechi ya Al Ahl na Raja refa alienda mwenyewe kutazama
 
Yaani wale Kaizer walikua wabovu kuliko hawa Orlando. Dakika ya 75 hadi 90 tumeona uhalisia wao, tukienda vibaya kunapigwa goli nyingi sana.
 
Ukweli uko wazi kua Simba msimu huu hatuko vizuri sana hasa eneo la umaliziaji na kidogo kwenye midfield hivyo kwa aina ya matokeo tuliyopata ni jambo lakushukuru kikubwa ni kwenda kupambana tu.

Na jambo lingine zuri nikua hatujaruhusu goli hivyo inaweza kuwajengea presha ya kiuchezaji wapinzani wetu kwakua tunanafasi ya kupata goli la ugenini ni mechi ambayo itakua wazi sana japo faida kubwa itakua kwa Pirates endapo watapata goli mapema.

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
 
Sasa kama VAR ya Afrika Ipo Kwa mtindo nilio uona Leo basi CAF Wana kazi kubwa ya kufanya.
Haijalishi tukio la Morrison kama ni penalty alali au sio halali ila namna VAR ilivyo tumika sioni na tofauti refa kumuuliza msaidizi wake
Kakate rufaa kama imekuuma...Au kafunge VAR yako.
 
Hongera unaujua mpira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…