OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Wachezaji wamsikilize Mbwaduke Azam HD, ana madini sana anachambua vizuri na wenzie Duwa Saidi na Lunyamila
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamvi la wageni . Au vipi?Wale wa Orlando Pirates tukutane jukwaa kubwa. Ndugu zetu wa Songea msisahau kuwashangilia hawa brothers wetu.
Kila mtu anajipakulia au unamaanisha nini mkuu?Jamvi la wageni . Au vipi?
So so so much HATRAGEThere's hate in my writtings.
Kunywa chai mkuu, ni njaa ndo inakusumbua.So so so much HATRAGE
Hasa alipozungumzia ile mechi ya SAOURA na ORLANDO.Wachezaji wamsikilize Mbwaduke Azam HD, ana madini sana anachambua vizuri na wenzie Duwa Saidi na Lunyamila
Jamaa anatema takwimu sana,anafaa kuwa match analyst wa timu kubwaHasa alipozungumzia ile mechi ya SAOURA na ORLANDO.
Tofauti na wale jamaa wa instagram.Jamaa anatema takwimu sana,anafaa kuwa match analyst wa timu kubwa
Mkuu nenda kaangalie katika Tv ya reception ya hospitali ili kama kikitokea chochote basi utapata msaada wa haraka sanaHapa bado sijafanya maamuzi niende kwa Mkapa, Kibanda Umiza au Home.
Option zote naweza kuangalia mpira.
Wale hamna kitu hiyo hata mimi naweza,ila Mbwaduke anaenda live na anaonyesha connectivityTofauti na wale jamaa wa instagram.
Amesema hawajawahi kukutana katika mashindano yoyote, labda utuambie Wewe hiyo "Pre Season" ilikua ni mashindano labda.Uwe unawauliza hata mashabiki wa Simba walio karibu na wewe chura.
Simba ilikutana na Orlando Pirates Pre-season ya 2019 na walitoka sare huko kwa madiba
Mbwaduke Kwa Data tu yuko vizur.Wale hamna kitu hiyo hata mimi naweza,ila Mbwaduke anaenda live na anaonyesha connectivity
Wewe utakuwa Hospital gani tuje tuangalie wote ili na wewe ukipata shida usaidiwe kwa haraka.Mkuu nenda kaangalie katika Tv ya reception ya hospitali ili kama kikitokea chochote basi utapata msaada wa haraka sana
Makirikiri waliwafunga uwanja wa NamfuaKwa Mkapa sio hatoki mtu tu bali twahitaji goli nyingi kuanzia 3 ili twende na imani kubwa ya kusonga mbele S. Afrika. Viva mnyama, kesho tuko pamoja...
Umeshindwa kuwaambia wenye stars times pia kama wanapenda kuangalizia mechi majuumbani wasipate tabu kwenda vibandani mechi wanarusha pia.Hello Tanzania, Sawubona South Africa!
Karibuni katika Kindumbwe ndumbwe cha mtanange wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Africa (Total Energies CAF CC) kati ya wenyeji Simba Sc wa Tanzania na Orlando Pirates wa South Afrika unaochezwa katika dimba la uwanja wa Taifa, "Kwa Mkapa" leo tarehe 17.04.2022 saa 1 jioni kwa saa za Africa Mashariki (saa 12 jioni kule kwa Madiba Bondeni)
Ni mchezo muhimu kwa timu zote 2 hasa ukizingatia hatua hii ni ya mtoano na mechi ni 2 tu nyumbani na Ugenini, kuelekea nusu fainali. Wenyeji Simba wamefuzu hatua hii ya robo fainali baada ya kushika nafasi ya pili kwenye kundi lao D kwa Point 10 nyuma ya RS Berkane ambao nao walikuwa na point 10 pia ila waliwazidi Simba idadi ya magoli ya kufunga. Kwa upande wao Orlando Pirates wao walifuzu hatua hii ya mtoano baada ya kuibuka kidedea katika kundi lao B kwa kuondoka na point 13.
Ni mchezo unaotarajiwa kuwa wa kasi, nguvu, maarifa na akili nyingi kwani Simba wanahitaji kujihakikishia ushindi nyumbani kwa kutaka magoli mengi ili njia iwe nyepesi wanapoenda ugenini huku Orlando Pirates nao wakitaka kulinda heshima kwa Sare au ushindi ugenini ili wapate mtaji mzuri wa kuanzia wakiwa uwanja wao wa Nyumbani "Orlando Stadium". Ikumbukwe hii ni mechi yao ya kwanza kukutana, huko nyuma hawajawahi kuchuana katika mashindano yoyote.
Orlando Pirates yuko nafasi ya 4 kwenye msimamo wa Ligi yao huku Simba akiwa nafasi ya pili katika Msimamo wa Ligi kuu bara
Je, nani ataibuka kidedea? au itakuwa Suluhu/Sare?
Karibu na kaa nami kuanzia mwanzo, katikati na mwisho wa kipute hiki...
Vikosi huenda vikawa (Sio rasmi)
Simba vs Orlando Pirates Predicted XI
Simba (3-4-3): Aishi Manula (GK); Mohamed Husseini, Joash Onyango, Henock Baka; Bernard Morrison, Jonas Mkude, Peter Banda, Shomari Kapombe; Larry Bwalya, Pape Sakho, Chris Mugalu
KOCHA: Pablo Franc Martin
Orlando Pirates (4-3-3): Richard Ofori (GK); Bandile Shandu, Thulani Hlatshwayo, Happy Jele, Bongani Sam; Abel Mabaso, Goodman Mosele, Kabelo Dlamini; Fortune Makaringe, Deon Kavendji, Kwame Peprah
KOCHA: Mandla Ncikazi
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Updates
1100 HRS
Mechi itaoneshwa kupitia (ZBC 2)- AZAM TV NA (225 FOOTBALL- DSTV )
Sent from my M2101K6G using JamiiForums mobile app
View attachment 2190564
Ndiyo mkuu. Au kwa lugha nyingine ni maponeo ya wageni wakiwa bado hawajazoea mtaaKila mtu anajipakulia au unamaanisha nini mkuu?