FT: Simba 1-0 Orlando Pirates | CAF CC quarter final | Benjamin Mkapa Stadium

FT: Simba 1-0 Orlando Pirates | CAF CC quarter final | Benjamin Mkapa Stadium

Hello Tanzania, Sawubona South Africa!

Karibuni katika Kindumbwe ndumbwe cha mtanange wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Africa (Total Energies CAF CC) kati ya wenyeji Simba Sc wa Tanzania na Orlando Pirates wa South Afrika unaochezwa katika dimba la uwanja wa Taifa, "Kwa Mkapa" leo tarehe 17.04.2022 saa 1 jioni kwa saa za Africa Mashariki (saa 12 jioni kule kwa Madiba Bondeni)

Ni mchezo muhimu kwa timu zote 2 hasa ukizingatia hatua hii ni ya mtoano na mechi ni 2 tu nyumbani na Ugenini, kuelekea nusu fainali. Wenyeji Simba wamefuzu hatua hii ya robo fainali baada ya kushika nafasi ya pili kwenye kundi lao D kwa Point 10 nyuma ya RS Berkane ambao nao walikuwa na point 10 pia ila waliwazidi Simba idadi ya magoli ya kufunga. Kwa upande wao Orlando Pirates wao walifuzu hatua hii ya mtoano baada ya kuibuka kidedea katika kundi lao B kwa kuondoka na point 13.

Ni mchezo unaotarajiwa kuwa wa kasi, nguvu, maarifa na akili nyingi kwani Simba wanahitaji kujihakikishia ushindi nyumbani kwa kutaka magoli mengi ili njia iwe nyepesi wanapoenda ugenini huku Orlando Pirates nao wakitaka kulinda heshima kwa Sare au ushindi ugenini ili wapate mtaji mzuri wa kuanzia wakiwa uwanja wao wa Nyumbani "Orlando Stadium". Ikumbukwe hii ni mechi yao ya kwanza kukutana, huko nyuma hawajawahi kuchuana katika mashindano yoyote.

Orlando Pirates yuko nafasi ya 4 kwenye msimamo wa Ligi yao huku Simba akiwa nafasi ya pili katika Msimamo wa Ligi kuu bara

Je, nani ataibuka kidedea? au itakuwa Suluhu/Sare?

Karibu na kaa nami kuanzia mwanzo, katikati na mwisho wa kipute hiki...

Vikosi huenda vikawa (Sio rasmi)

Simba vs Orlando Pirates Predicted XI
Simba (3-4-3): Aishi Manula (GK); Mohamed Husseini, Joash Onyango, Henock Baka; Bernard Morrison, Jonas Mkude, Peter Banda, Shomari Kapombe; Larry Bwalya, Pape Sakho, Chris Mugalu

KOCHA: Pablo Franc Martin / Suleiman Matola

Orlando Pirates (4-3-3): Richard Ofori (GK); Bandile Shandu, Thulani Hlatshwayo, Happy Jele, Bongani Sam; Abel Mabaso, Goodman Mosele, Kabelo Dlamini; Fortune Makaringe, Deon Kavendji, Kwame Peprah

KOCHA: Mandla Ncikazi / Fadlu Davids
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

Updates
1100 HRS

Mechi itaoneshwa kupitia
(ZBC 2 Channel namba 406)- AZAM TV
(Channel 225 FOOTBALL- DSTV )
TV3 (Startimes- channel #197 Dish na #131 antenna)

Streaming Links [emoji116][emoji116]

Watch Simba vs Orlando Pirates live 16:00 17/04/2022 | AMZfootball


1500 HOURS

-Washabiki kutoka sehemu mbalimbali wanazidi kuingia uwanjani

  • Mgeni Rasmi ni Abdulrahman Kinana
  • Teknolojia ya VAR ipo tayari imesetiwa kuhukumu mchezo wa leo, endapo panapotokea matukio 'tata'

1745
- Kikosi cha Simba kimefika Uwanjani

1800

Kikosi Rasmi cha Orlando pirates

Kikosi cha Orlando Pirates kinachoanza

Ofori Richard (GK) ,Jele Happy, Nyauza Ntsikelelo, Maela Innocent,Shandu Bandile, Mosele Goodman, Monare Thabang, Ndlovu Siphesihle, Hotto Deon, Dlamini Kabelo, Peprah Kwame

Subs: Mpontshane Siyabonga, Sam Bongani, Hlatshwayo Thulani, Mabaso Tshegofatso, Motshwari Ben, Makaringe Fortune, Mntambo Onassis, Lorch Thembinkosi, Lepasa Zakhele



- Kikosi cha Simba kinachoanza
Manula A. ,Kapombe S,Hussein M ,Henock I Wawa SP, Mkude J,Sakho PO ,Lwanga T, Mugalu CK, Morrison B, Banda P.

Subs: Beno,Israel,Nyoni,Kennedy,Mzamiru,Kibu,Bwalya,Kagere,Mhilu


1850

Bado dakika kumi soka lianze hapa kwa Mkapa, mashabiki wamejaza uwanja tayari kusubiri kipute hiki huku wakihanikiza kwa Shangwe na Tochi za simu zao

1855

Timu zimeingia uwanjani tayari

00+1' KICK OFF Simba wameanzisha mpira hapa


2' Simba wanatengeneza shambulizi hapa ila Kapombe anatoa nje inakuwa goalkick

4' Simba wanapata kona wanaanza wanashambukia kidogo ila inadakwa..Orlando Bado hawajatulia

6' Orlando pirates wanaonana vyema wanafikavmbele ila plan yao inaharibiwa na mabeki wa simba

8' Peprah anashambulia pale anamchungulia Manula ila inakuwa nje

10' Simba 0 - Orlando Pirates 0 wakati huo Sakho yupo chini baada ya kuangushwa na Happy Jele

13' Pirates wanawa press Simba, mpira unatoka nje wanauwahi pale ipa wanacheza faulo


19' kuelekea 20 Simba wanawapress Orlando , Mugalu anafosi pale ila kipa Ofori wa Orlando anaanguka chini, madaktari wanamuona


23' Bado game ni 0_0 mpira bado ni wa kusomana


31' Pirates wanaonana vizuri wanazembea, wananyang'anywa..Peprah alichelewa kushambulia
wakati huo mkude anapiga shuti kubwa linaenda nje


35' Simba wanaanza kona wanapasiana vizuri wanashambulia pale ila Ofori anaidaka (0-0)

37' Pirates wanacheza kwa tahadhari ya hali ya juu sana wakionana kwa pasi fupifupi na kuzuia kwa umakini

45' Morrison anashambulia pale inakuwa kona wanaanziana ila hawajafanikiwa

bado dakika 3 kuelekea mapumziko

45' +3 Halftime Simba 0_0 Orlando Pirates... wanapumzika tumeshuhudia kipindi cha kwanza kikiwa na nafasi ndogo sana za utafutaji mabao
HT STATS:
POSSESSION SIMBA 59% Pirates 41%
Shots Simba 8(1) Pirates 3(1)
No Red and Yellow card
Fouls 5 Simba na 8 Pirates
corner 4 Simba na 1 Pirates


45' Second half mpira umeanza

46' Sub kwa Orlando pirates

Makaringe In, kabelo out

wakati huo Pirates wanapata kona inapigwa inatoka nje inakuwa ya kurushwa

50' Pirates wanapress wanapata faulu pale inapigwa na Hotto.. Pepra anaunganisha na kichwa unaenda nje



55' Mugalu anapiga shuti ila kipa analiona

sub kwa Simba

kibu in banda out


Bwalya In Taddeo out

58' Morison anaangushwa nje ya box wanapata faulu...anapiga Morison inagonga ukuta nje inakuwa kona

kona inapigwa na RB ila inadakwa na kipa ofori


60' Sakho anaangushwa chini inakuwa faulo, naona kwa mbali kuna mashabiki wanamulika kipa wa pirates na vitochi vya kijani

Morison anapiga faulu kuuubwa inaenda nje


63' Kapombe yupo chini baada ya kubabuliwa na mpira kutoka kwa Manula


64' Morison anaangushwa kwenye box refa anaamua penalti ila anawasiliana na VAR REVIEW kuangalia uhalali

66' Ofori anapewa kadi ya njano

67' Goooal Kapombe anaifungua simba kwa penalti

68' Simba 1 Orlando Pirates 0

70' Mandla Ncikazi kocha wa pirates anapewa Yellow card
huku Sakho nae anapewa kadi ya njano

75' Pirates wanapata kona
..inapigwa Manula anaokoa...kona tena

Sub kwa Simba Mzamiru In Morison out

Sub kwa pirates Lepasa in Pepra out

78' yellow card kwa Deon Hotto

80' Pirates wanapata kona inapigwa kule inaokolewa

81' Happy Jele anaoneshwa kadi ya njano kwa kumuangusha Kibu D.. Faulu unapigwa na Bwalya anaanza na Kapombe anapaisha juu ya mtambaa panya


85' Simba sub wanafanya

Kagere in Mugalu out

sakho out muhilu in


88' Bado Simba wanaongoza 1 bila wanajaribubkuonana ila mipango inatibuliwa bado wanashambulia lakini

90' Simba wanapress kwa pirates wanapata faulu wanaanza haraka ila Kagere anautoa nje...

Dakika 4 kuelekea Full time

90+1' Pirates wanaanzishiana faulu fupi ila Manula anaudaka

90+3' Pirates wanashambukia langonlabsimba kama nyuki..wanapanga mipango mingi mpira unaenda nje...Goal kick

90+4' Manula anapiga ndeeefu na mpira umeisha

FULL TIME SIMBA 1 ORLANDO PIRATES 0

Je Second Leg itakuwaje kule South Africa mnamo 24/4/2022? Tusubiri

Ahsanteni kwa kuwa nami... Adios Amigo!





Sent from my M2101K6G using JamiiForums mobile app
View attachment 2190564
Hongereni Simba ,Morrison kama asinge umia may mnengeongeza hata goli moja.

Out of Topic.

Hivi Qnet ni moja ya wadhamini wa hii michuoni daah, yaani kama naona kwenye lile file lao wanalo litumia kusaundisha watu picha ya mechi ya leo ya Simba lazima zitakuwepo.
 
Ambao hawaamini macho yao ni wale waliozoea kushinda goli 2+ kwa mkapa kwenye mechi za mtoano lakini leo hii wameambulia goli moja tu. Nikifikia historia zenu za away. Aisee Mungu awaepushie na kikombe maana mlishinda goli tatu dhidi ya red arrow kilichotokea kule kila shabiki alishika shavu kujiuliza ni hii timu yetu iliyoshinda tatu kule dasalama
ese ndeeefu,mmeanza kubadili gia leo. Tangu enzi za Red Arrows mpaka kutinga nusu fainali
 
Goli moja ni kubwa sana kawaulize fc bayern
Nisawa kwenye mpira lolote linawezekana ila tunajadili uhalisia wa mpira wetu.Sidhani kama simba ana mipango yakucheza mpira tofauti na anaouchezaga ugenini.kwahiyo mwenye advantage ya mechi ya mwisho niyule atakayekua nyumbani.ndo maana naona tulitakiwa kufunga magoli mengi zaidi ili kujihakikishia usalama zaidi.
 
Hongereni Simba ,Morrison kama asinge umia may mnengeongeza hata goli moja.

Out of Topic.

Hivi Qnet ni moja ya wadhamini wa hii michuoni daah, yaani kama naona kwenye lile file lao wanalo litumia kusaundisha watu picha ya mechi ya leo ya Simba lazima zitakuwepo.
😂😂
 
Nisawa kwenye mpira lolote linawezekana ila tunajadili uhalisia wa mpira wetu.Sidhani kama simba ana mipango yakucheza mpira tofauti na anaouchezaga ugenini.kwahiyo mwenye advantage ya mechi ya mwisho niyule atakayekua nyumbani.ndo maana naona tulitakiwa kufunga magoli mengi zaidi ili kujihakikishia usalama zaidi.
Nguvu moja
 
Ambao hawaamini macho yao ni wale waliozoea kushinda goli 2+ kwa mkapa kwenye mechi za mtoano lakini leo hii wameambulia goli moja tu. Nikifikia historia zenu za away. Aisee Mungu awaepushie na kikombe maana mlishinda goli tatu dhidi ya red arrow kilichotokea kule kila shabiki alishika shavu kujiuliza ni hii timu yetu iliyoshinda tatu kule dasalama

Angalia na timu ambayo Simba amecheza nayo. Mechi ilikuwa ngumu Sana. Hivyo usiwabeze na kuwachukulia kawaida. Kwa Sasa Simba wakienda South wasiende kwa pressure Bali waende Kama vile Ni fainali.
 
Ambao hawaamini macho yao ni wale waliozoea kushinda goli 2+ kwa mkapa kwenye mechi za mtoano lakini leo hii wameambulia goli moja tu. Nikifikia historia zenu za away. Aisee Mungu awaepushie na kikombe maana mlishinda goli tatu dhidi ya red arrow kilichotokea kule kila shabiki alishika shavu kujiuliza ni hii timu yetu iliyoshinda tatu kule dasalama
Ukimaliza utupe na rekodi zenu uto[emoji1].
 
Walio tengeneza mfumo wa VAR walitaka uwazi Ili kuondoa lawama zisizo na Sababu Ili baadae refa asije kusema Ali ingizwa Chaka.
Kusikiliza waliondani kwenye mtambo bila kuona video Haina tofauti na kumsikiliza mshika kibendera.
Labda waseme VAR ya Leo ilikua ya majaribio, OG itakuja.
Wewe kweli ni redio.
 
Back
Top Bottom