FT: Simba 1 - 1 Asec Mimosas | CAF Champions league | Mkapa Stadium | 25.11.2023

Mm nilianza kuangalia mpira Dk ya 60 ! Kwa namna Simba walivyokuwa wanapoteza mipira kirahisi na pasi pasipo macho... Ilikuwa ni miujiza pekee kuzuia ASEC wasisawashe! Na hii itafanya tusio hudhuria kuangalia Mazoezi tuwe na wakati mgumu kujua uwezo wa golikipa Ayubu!
 
Uko sahihi kabisa na mimi ndiyo maana nimekuwa nasema itachukua muda mrefu sana hii timu kukaa sawa maana hata wanaotakiwa kurekebisha nao ni chanzo cha tatizo.

Kuanzia wanaohusika na usajili, management inayoendesha shughuli za kila siku za timu, timu nzima ya ufundi na kambi huko kote kumeoza. Matatizo ya uwanjani ya Simba yanaanzia kwenye uwanja wa mazoezi. Unarudi Bodi ya Wakurugenzi unakutana na kina Asha Baraka na mifumo na taratibu zilizopitwa na wakati, zilizojaa siasa na ambazo haziruhusu uwajibikaji.

Baadhi ya haya mambo nimeshayasema sana.


 
Na hapo ndipo tofauti kati ya mashabiki wa Simba na Yanga
Mashabiki WA Simba wanafanya kosa kubwa Sana. Hata kama ni wewe umekosea mara moja Bosi wako akutukane na kukusimanga wakati huko nyuma ulifanya Vizuri utafurahi?Yanga wameona udhaifu WA Simba. Jana wamefungwa Ila Leo wanawajaza upepo Simba ili mivutano iendelee. Wachezaji wanaotakiwa kila siku washinde wakifungwa wanasimangwa Simba mtawatoa wapi?.
 
Mkuu unajua kuna watu wanazunguka na timu kuishangilia bila malipo, Yaani Wachezaji wanalipwa, kocha analipwa, management ina malipo ila Shabiki anavaa kinyago, anajipaka masizi, anabeba ungo kwenda kushangilia timu kama kichaa bila malipo jua lake, mvua yake.
Jaribu tu kuwa mwelewa mtu akiwa na hasira na timu yake anayoishabikia.

Kuhusu timu za wenzetu mifumo ni tofauti sana, kule hata timu ndogo daraja la kwanza zina viwanja na zinajaza mashabiki. Mechi inayochezwa miezi 2 mbele tiketi zimeshauzwa leo na kuisha. Kwa sasa tusijilinganishe kwani wametuacha mbali.
 
Wanakosa uvumilivu sisi tumevumilia sana, iwe wakati wa raha au shida, kifupi wengi wao tunajitambua
 

Kama hawawezi presha waombe kuvunja mkataba. Sisi kama mashabiki hatuwezi kuwasubiria haa kidogo. Simba ni timu kubwa muda wote tunahitaji matokeo. Poteana mechi moja inatosha.
 
SIMBA NDO INATIKA KWA MKAPA MUDA HUU NNE KASORO
 
Mashabiki wa 5imba acheni kujazwa upepo, ni Uto hao wanachochea Kuni.
Timu si mbovu to that extent (kwa maana wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na kadhalika), kilicholeta tafrani hapa ni kono la nyani tu kutoka kwa mtani, lakini kabla Nov 5 hakukua na haya mambo ukiacha watu wasiozidi watatu humu kwenye Jukwaa
Na hata Uto walivyokua wakiikandia timu ilikua na watetezi wengine sana, sasa hivi ni tofauti au ndio mnakubali kwamba NGAO ya JAMII na zile mechi 6 za mwanzo za NBC PL zilikua kwa hisani ya dada TATU & associates?
 
Kama hawawezi presha waombe kuvunja mkataba. Sisi kama mashabiki hatuwezi kuwasubiria haa kidogo. Simba ni timu kubwa muda wote tunahitaji matokeo. Poteana mechi moja inatosha.
Mimi naona wewe ndio ujitoe kuwa shabiki wa Simba. Mmezidi lawama, utafikiri mmewekeza Simba. Uongozi umefanya kama mlivyotaka. Mlitaka Chama na Miquissson warudishwe, wakafanya hivyo. Sasa wao wafanye nini? Kama mnataka timu isiyofungwa, basi sajilini malaika.
 
Matokeo yenu kule Algeria hatujasahau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…