FT: Simba 1 - 1 Asec Mimosas | CAF Champions league | Mkapa Stadium | 25.11.2023

FT: Simba 1 - 1 Asec Mimosas | CAF Champions league | Mkapa Stadium | 25.11.2023

Pale kati Simba kwa sasa kuna tatizo bila kujali ni la nani. kiungo mkabaji na kiungo mshambuliaji ni kama hawapo.

Hii ndo inasababisha mabeki wawe na kazi ya ziada kumlinda kipa na wakichoka ndo hivyo tunafungwa na huko mbele kina baleke na phiri wasionekane. Shida ni katikati hakuna ubora.

Ndo maana nikasema kwa Yanga niliyoitazama jana tusije tukakutana nao halafu tukacheza kwa kiwango hichi, tutanyanyasika mno.

Tusidanganyike na Yanga kufungwa na Waarabu, huenda wakafungwa tena ila Waarabu walicheza kwa nidhamu sana dhidi ya Yanga, nidhamu ambayo haipo Simba kwa sasa esp katikati.
Pamoja na hayo tuache kuwa mashabiki wa mafanikio tu, timu ikipata changamoto kidogo tunakata tamaa mno. Tukumbuke huwa kuna kipindi cha mpito baada ya mafanikio. Yaelekea tumeshasahau furaha tuliyoenjoy kwa miaka minne au mitano mfululizo. Mashabiki wa kweli husimama na timu muda wote, angalia Manchester, Liverpool na Chelsea. Ona sasa Mashabiki maandazi wanahamasishana kutokwenda uwanjani, hii si sawa.
 
Pira Papatu Papatu kazini wanasimba sijui tunaelekea wapi
Changamoto katika timu ni suala la kawaida wewe shabiki wa juzijuzi. Timu haiwezi kuwa kwenye peak muda wote. Kuweni wavumilivu, timu itainuka tena. Manchester, Liverpool, Chelsea zote zimepitia changamoto, lakini mashabiki wamebaki na timu zao.
 
Harusi ya kuingia Robo final tunayoo, lazima tugawe sare my [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
IMG-20231125-WA0077.jpg
 
Maboresho makubwa yafanyike kiufundi.

Kuja kocha mpya ni hatua moja, lakini idara nzima ya ufundi na hasa training facilities ikiwa na pamoja na aina ya CAMP...

Ona timu inavyokimbia ( ftness iiko chini )..
Hili ni tatizo la muda mrefu, na kocha mpya atarithi.

SIMBA fans itahitaji muda kusubiri wa kuirudisha simba ya kasi ...

Nina mashaka ktk team training and camp management...

Kuna msingi mbovu MR OBJECTIVE ameuacha na too late kwa management kushtuka.

Kama ni mimi CEO ( Kajula ) na chairman Mangungu ningejiudulu ili kupisha upepo mbaya ..
 
Back
Top Bottom